Kuna kikundi kimekua kikisisitizia kauli ya marehemu mwendazake ya"mtakuja kunikumbuka",kana kwamba tulifanya kila liwezekanalo kumuondoa madarakani.
Mwendazake kachukuliwa na Muumba,na zaidi hata tulipotaka kuujua ukweli juu ya shida yake kama anaumwa ama vp,ili tumuombee apone maake tulikua tayari tushaamua kuishi nae ,bado tulifichwa.
Haina haja ya kutoa toa iyo kauli,sababu hatukua na uwezo wowote wa kupinga alichohitaji,hakuna chombo chochote cha habari ,wala mitandao ya kijamii iliyokua na ubavu wa kumuwekea kauzibe kwenye utendaji wake wa kazi.
Yaani katika marais waliofanya kazi bila presha basi mwendazake alikua free saaana,hapingwi na bunge,wananchi wala media.
So kusema kwamba tutakuja kumkumbuka ndio kweli tutamkumbuka kwa mema aliyofanya lakini hatujawahi kufanya jaribio loloooooote la kumuondoa mwendazake,aidha MAANDAMANO,BUNGE,kila aliyefanya hivyo nadhan inajulikana kilichomkuta.
Kusema kwamba tutakuja juta ni sawa na kuwa na mpenzi wako kila siku analalamika utakuja mkumbuka na wakati haumfanyii chochote kibaya unampa kiiila kitu anaishi kulalalama tu.
.........
Kwa kweli kifamilia atakumbukwa daima mana ni baba wa familia, ni mume wa mtu, ni mtoto wa mtu, ni kaka wa watu,ni mjomba wa watu na ni babu wa watu. Mungu ampe pumziko la milele.
Lakini Kama mtawala juu ya mamilioni ya watu kuna tatizo kuwalazimisha watu kumkumbuka. Hasa unapobaini kuwa kuna propaganda nyingi zilizokuwa zinatumika tangu mwanzo na zimekuwa zikitumika sana kuhalalisha uovu ndani ya CCM na serikali yake.
Udini,
Ukabila,
Ukanda,
Ujinga wa watu.
Vitisho,
Umaskini watu wanaitwa wanyonge.
Ulaghai
Rushwa ya madaraka.
Rushwa ya fedha.
Makada wa CCM walioko kwenye vyombo vya dola kutumia ukereketwa wao kuumiza watu na kuhujumu chaguzi.
Hivyo vyote ndio ngao ya CCM kuwatawala na kuwanyonga na kuwafanya watanzania kuwa wanyonge na kisha kuwaletea ibada za kuabudu watawala mpaka mizimu yao. Laana kubwa kwa Taifa.
Kuna watu wameanza kudanganya watu kuwa Marehemu amefanyiwa njama jambo ambalo ni hatari sana kwa usalama wa nchi.
Kwa nini hawa watu wasikamatwe ili watoe ushirikiano wa kujua ukweli.
Jeshi la polisi kuwafumbia macho ni kuhtarisha usalama wa nchi.
Jeshi la polisi sasa lirudi kwenye utendaji wake wa kulinda watu na mali zao na usalama wa nchi.
Kuwaacha wajinga waliolaaniwa na hulka zao za Ukabila kupotosha na kuvuruga usalama wa nchi kwa sababu tu ya madaraka ni jambo baya na la hatari kwa usalama wa nchi yetu.
Marehemu hata wakati wa Kampeni mwaka Jana alionekana kudhoofika kiafya.Ndio maana hasimu wake mkubwa alikua anazuiwa mara kwa mara kufanya kampeni. Ili waende sawa.
Hata hivyo kitaifa pia kuna watu wafuatao :-
Watu waliopata uenyekiti wa serikali za mitaa kwa dhulma.
Wapinzani waliohongwa uwaziri na ubunge,
Watu waliopata ubungwe kwa dhulma,
Watu waliopewa madaraka kikabila.
Watu waliopewa madaraka kwa vyeti feki.
Watu waliopewa fedha ili kuwachafua watu wengine na kumpamba mtu mmoja.
Watu wasiojulikana waliompaga risasi Lisu na kuachwa bila kukamatwa .
Watu waliowateka watu mchana kweupe bila kulamatwa.
Watu waliolewa madaraka na kuwa kama miungu watu.
Hakika hao watamkumbuka daima dumu.
Kila mmoja atamkumbuka kwa mazuri au mabaya. Ni binadamu yule sio mungu pamoja na kwamba mbinyo na njaa ziliwafanya watu wamfananishe na Yesu kristo wa Nazareti.