Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Hata huyu mama azingue vipi tutamuhukumu kama yeye, lakini yule dhalimu hatuwezi kumkumbuka kwa lolote zaidi ya ulevi wake wa madaraka.
Mi sijasoma chochote kile ila nachojua atakumbukwa na watu watatu tu hapa nchini Kabudi,MAKONDA,NA SABAYA
 
Alikuwa mpika data mkubwa!!kila siku alituambia uchumi unakuwa kwa 6.7% hadi hao IMF, WB, Wakawa wanapinga akaja na sheria yake ya takwimu, kuwa ni marufuku, kwa taasisi yoyote kutoa takwimu zake, alipopigwa biti ndio wakaibadirisha!!baada ya kifo chake ndio tunaambiwa ukweli kuwa uchumi ipo kwenye 4%!!!Jamaa alikuwa muongo sana, hata huo uchumi wa kati wa chini, ukiangalia alichokiongeza ni kidogo sana kufikia hapo!!!
 
Investment zilishuka kutoka dola milion 2000 mwaka 2015 hadi dola milion 800 tu mwaka 2019 kabla hata ya korona.

Na deni la taifa lilikuwa linakua kwa kasi ya airbus
Investment kama Richmond, Dowans and Symbjon! Haya si makampuni yakinyonyi tu hayo yote tuliyapigia kelele weeee
 
Wakati anaingia Ikulu Hayati JPM alisema kuwa kuna watu wanaishi kama Malaika. Alimaanisha matajiri na wafanyabiashara wakubwa, mafisadi waliojineemesha kwa migongo ya walipa kodi ambao asilimia kubwa ni masikini.

Kiuhalisia Hayati alipigwa sana vita na makundi makuu mawili , la kwanza ni la Wanasiasa na wafuasi, na kundi la pili ni la matajiri wakubwa. Niwe mkweli katika hili kundi la kwanza la wanasiasa ni kweli lilipata madhila makubwa, unyanyapaa na manyanyaso ambayo hawakustahili. Lakini kundi la pili ni la wafanyabiashara wakubwa na matajiri ambao ukweli mchungu ni kuwa walihodhi sehemu kubwa ya uchumi wetu kwa ulaghai, ufisadi, ukwepaji kodi, unyonyaji, n.k.

Tulimsema sana JK kwa kulikumbatia hili kundi la pili na ndo jambo ambalo lilimpa lawama kubwa sana sababu sehemu kubwa walikuwa ni marafiki zake wa karibu na wengine walineemeka kwa mgongo wake. Upande wa wanasiasa hawakupata kashkash nyingi sana kama wakati wa hayati. Alipoondoka JK , licha ya ubaya wa ufisadi na ukamuliwaji wa tabaka la chini katika utawala wake na kuingia JPM ambaye alianzakuwaminya wanasiasa ndipo hapo watu wakaanza kumkumbuka JK kwa mazuri yake. Mazuri yaliyokuwa yanasemwa ni kukubali kukosolewa, kuruhusu wanasiasa kufanya siasa n.k .

Ameondoka JPM ameingia mama ambaye alikuwa anaonekana anakuja kutibu maradhi yote ya awamu iliyopita. Watu walipata moyo wa kusikilizwa vilio vyao, utawala bora n.k katika miezi miwili au mitatu ya kwanza . Lakin ghafla bin vuu ni kama vile upepo umehama na inaonekana kama Mama ameanza kutia pamba masikioni. Jakaya inasemwa kuwa marafiki, wapambe na washauri walimuharibia basi nachelea kusema pia Mama waliomzunguka wanamuharibia. Dhana ya utawala bora ni kujua mahitaji ya wananchi kwa wakati uliopo pia lakini hii dhana ya kujenga na kuimarisha uchumi kwa njia ya kunyonya raia ambao sehemu kubwa ni masikini si katika sifa za uongozi bora. Huu utawala unarudi katika kipindi ambacho wachache wataneemeka sana, tunarudi awamu ya nne kiuchumi na ya tano kisiasa. Tayari kundi la wanasiasa limeashaanza kulalamika hasa baada ya kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa, lakini pia kurukwa kwa kihunzi cha katiba Mpya. Hili linaifanya ile Hiyena hiyena ya wanasiasa iliyoanza mwanzo kuondoka. Kundi la pili la Matajiri,, wafanya biashara wakubwa na wanyonyaji ambalo sitarajii kama litaguswa. Na hapa ndo itahitajikajika nguvu ya kuendelea kuwanyonya masikini kufidia haya Magap.

Tukumbuke kuwa kundi kubwa lilikuwa linamuunga Mkono Hayati ni kundi la watu wa chini ambao yeye mwenyewe alikwepa sana kugusa maslahi yao na alijinasibu kuwa ni Mtetezi wao. Hawa ndo walihuzunika sana wakati amefariki. Kwa haya mambo ya Kodi za kuumiza yaliyoanzishwa na Serikali ya SSH kupitia kwa wizara yake ya fedha na mipango chini ya Mh. Mwigulu Nchemba na kupata baraka za Bunge nachelea kusema kuwa soon Mama ategemee kupingwa vikali na kundi hili la tatu kwa sababu hata kundi la viongozi wa dini lipo nusu kwa nusu. Serikali ya Samia inaenda kukutana na Stunts za awamu iliyopita kuwa watu walikuwa wanamkumbuka JK. Nadhani wakati wa watu wa tabaka la chini kumkumbuka mtetezi wao linakuja.

Kundi la tabala la chini sasa limeanza kulalamika kuwa Serikali inatunyonya, mbona hakuna hela mitaani,n.k linaanza kuongezeka taratibu. Hili kundi likikubali kupata msukumo wa kundi la wanasiasa ambao tayari ni kama wameshavunja mahusiano na Mama basi SSH atapata lawama kubwa. Inasikitisha na kufikirisha sana Mama aliwananga TRA kwa kupiga kodi za kuumiza wafanyabiashara wakubwa lakini ameshindwa kuzuia kodi mara mbili "Double Taxation" kwenye huduma moja kwa kubadili lugha na kuita "TOZO" tena kwa mtanzania ambaye haingizi chochote kama mfanyabiashara.

Nini lengo la "VAT"? .

Kwa muktadha huu nadhani majuma machache yanayokuja tutaanza kusikia vilio vya watu kusema ni heri ya Mwendazake hakutubana sisi masikini, ama kweli alikuwa Rais wa wanyonge, Rais wa Mama Ntilie, Rais wa bodaboda, Rais wa wamachinga , n.k ambao na ni watumiaji wakubwa wa Miamala ya simu.

Tumeambiwa tusubiri fedha itaingia mtaani, Hivi aliyezungumza hili alimaanisha au alikuwa anatania?.

Huu ni muelekeo wa kumpa ahueni Mtanzania wa chini kiuchumi?.

Kwa staili hii ya SSH administration hakika nimemuelewa Jiwe aliposema "
Hao wanyonge nao wachangie maendeleo ya nchi yao, sio tu kutegemea kubebwa na tabaka la kati na la juu wenye kulipa kodi!
 
Kwanini investment zishuke halafu uchumi upae mpaka kufikia uchumi wa kati. Umeshawahi kujiuliza hizo investment zilikua zinachangia nini kwenye uchumi? au zilikua zinanufaisha investors wenyewe. Nakushauri usiangalie numbers of investment, bali ni namna zina contribute to the economic growth. Na hili unaweza kulifanya kwa kuweka chuki zako binafsi pembeni ili uwe neutral.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
Hivi mkuu huo uchumi wa kati wa chini uliofikiwa na awamu ya tano, unafahamu ni tsh.ngapi?zimeongekeza kutoka kwenye awamu ya nne?kwani unaonekana kama kidogo unaufahamu na mambo haya lakini kinachonishitua ni eti uchumi upae hadi kufikia uchumi wa kati?ingekuwa uchumi wa kati wa juu sawa!!awamu wa tano kazi yao ilikuwa ni kuweka propaganda kwenye uchumi tu hakuna lolote!!eti uchumi tuko kwenye 7% kumbe ni 4% yaani dunia nzima uchumi ulikuwa unashuka ni TZ, tu ndio ulikuwa unapanda kipindi chote cha corona!!eti tumefikia uchumi wa kati kabla ya muda 2025!!ndio yalikuwa malengo hayo ya uchumi wa kati wa chini?!!au ilikuwa wa juu?!!
 
Alikuwa mpika data mkubwa!!kila siku alituambia uchumi unakuwa kwa 6.7% hadi hao IMF, WB, Wakawa wanapinga akaja na sheria yake ya takwimu, kuwa ni marufuku, kwa taasisi yoyote kutoa takwimu zake, alipopigwa biti ndio wakaibadirisha!!baada ya kifo chake ndio tunaambiwa ukweli kuwa uchumi ipo kwenye 4%!!!Jamaa alikuwa muongo sana, hata huo uchumi wa kati wa chini, ukiangalia alichokiongeza ni kidogo sana kufikia hapo!!!
Kwaiyo ndege zilizokuwa zinaletwa azikuwa zinanunuliwa cash,zahanati azikujengwa, Dodoma city azikujengwa,CGR, aikujengwa wakati wa utawala wa Magufuri,Bwawa kubwa la umeme alikuanzishwa na Magufuri,Jamani hata kama ni uongo,mambo mengi nyamaze tu,kama alikuwa anapika data hiyo ela ya kufanya haya alikuwa anaitoa Wapi?
 
Sijawahi tafuta ridhki yangu kiujanja janja, JPM atabaki kuwa rais wangu bora kwa miaka yote, na sidhan kama atatokea kama yeye, nitawa adithi wanangu na wajukuu na vitukuu vyangu mema ya JPM kama YEHOVA atanijalia maisha marefu.
 
Kwaiyo ndege zilizokuwa zinaletwa azikuwa zinanunuliwa cash,zahanati azikujengwa, Dodoma city azikujengwa,CGR, aikujengwa wakati wa utawala wa Magufuri,Bwawa kubwa la umeme alikuanzishwa na Magufuri,Jamani hata kama ni uongo,mambo mengi nyamaze tu,kama alikuwa anapika data hiyo ela ya kufanya haya alikuwa anaitoa Wapi?
CGR, ndio mdudu gani?sasa mkuu labda utuambie nini maana ya kulipa kitu kwa CASH!!ina maana kama unakopa kutoka A, unaenda kumlipa B, kwa cash hapo ki uchumi utasema wewe una pesa??alichokuwa anakifanya ndio hicho!!kama aliyoyafanya yote hayo na deni la taifa likawa ni lile lile alilolikuta 2015 la trilioni 25, hapo ningekuelewa na angetakiwa pongezi!!lakini kama ndani ya miaka mitano tu aliweza kukopa trilioni 35 na huku kila kitu anasema ni pesa za ndani tuelewe vipi?kama sio ulaghai tu?
 
Wote ni wale wale,yule alitengeza tabaka la chini Ili alitumie kisiasa.
Aliuwa sekta binafsi akazalisha machinga Ili wampigie kura.
Mwingine ajuacho ni kurembua tu
 
Mi sijasoma chochote kile ila nachojua atakumbukwa na watu watatu tu hapa nchini Kabudi,MAKONDA,NA SABAYA
Bila kusahau Musiba.
Musiba hadi anaumwa siku hizi kwa kukosa ruzuku,tangu mfadhili wake amekufa ajaweza tena kulipa mishahara wafanyakazi wake anaburuzwa mahakamani.
 
Hakika.....

Na Magufuli ndiye aliyemchagua Kipenzi chetu mh.SSH na wakaja na slogan ya "HAPA KAZI TU".....

Leo awamu ya 6 ni mwendelezo wa AWAMU YA 5...."KAZI INAENDELEA"......

Kisichofanana ni kimoja tu ,kuwa TAIFA halirudi nyuma....

Njia za kutatua changamoto za taifa hubuniwa Kila uchao....na awamu hii imebuni njia zake....

JANA SI LEO.....

Makosa ya LEO hayatokuwa ya KESHO.....

Najitayarisha KISAIKOLOJIA kuiona AWAMU YA 7 ikiwa na njia MSETO ama TOFAUTI kidogo na AWAMU HII YA 6 hata kama Rais atakuwa ni Kipenzi cha Watanzania mh.SSH!!

#RipJPM
#MunguMbarikiNaKumlindaSSH

TUSEME....

Aaaaaaaaamin
Aaaaaaaaamin
Aaaaaaaaamin🙏
 
Ndo maana ataki katiba mpya Ili kuhalalisha ujambazi huu kwa tozo hizi za dhuluma za kuwaibia masikini,sijui muislamu gani huyu anashiriki dhuluma Hakuna tozo kama hizi duniani kote.
 
Back
Top Bottom