Wakati anaingia Ikulu Hayati JPM alisema kuwa kuna watu wanaishi kama Malaika. Alimaanisha matajiri na wafanyabiashara wakubwa, mafisadi waliojineemesha kwa migongo ya walipa kodi ambao asilimia kubwa ni masikini.
Kiuhalisia Hayati alipigwa sana vita na makundi makuu mawili , la kwanza ni la Wanasiasa na wafuasi, na kundi la pili ni la matajiri wakubwa. Niwe mkweli katika hili kundi la kwanza la wanasiasa ni kweli lilipata madhila makubwa, unyanyapaa na manyanyaso ambayo hawakustahili. Lakini kundi la pili ni la wafanyabiashara wakubwa na matajiri ambao ukweli mchungu ni kuwa walihodhi sehemu kubwa ya uchumi wetu kwa ulaghai, ufisadi, ukwepaji kodi, unyonyaji, n.k.
Tulimsema sana JK kwa kulikumbatia hili kundi la pili na ndo jambo ambalo lilimpa lawama kubwa sana sababu sehemu kubwa walikuwa ni marafiki zake wa karibu na wengine walineemeka kwa mgongo wake. Upande wa wanasiasa hawakupata kashkash nyingi sana kama wakati wa hayati. Alipoondoka JK , licha ya ubaya wa ufisadi na ukamuliwaji wa tabaka la chini katika utawala wake na kuingia JPM ambaye alianzakuwaminya wanasiasa ndipo hapo watu wakaanza kumkumbuka JK kwa mazuri yake. Mazuri yaliyokuwa yanasemwa ni kukubali kukosolewa, kuruhusu wanasiasa kufanya siasa n.k .
Ameondoka JPM ameingia mama ambaye alikuwa anaonekana anakuja kutibu maradhi yote ya awamu iliyopita. Watu walipata moyo wa kusikilizwa vilio vyao, utawala bora n.k katika miezi miwili au mitatu ya kwanza . Lakin ghafla bin vuu ni kama vile upepo umehama na inaonekana kama Mama ameanza kutia pamba masikioni. Jakaya inasemwa kuwa marafiki, wapambe na washauri walimuharibia basi nachelea kusema pia Mama waliomzunguka wanamuharibia. Dhana ya utawala bora ni kujua mahitaji ya wananchi kwa wakati uliopo pia lakini hii dhana ya kujenga na kuimarisha uchumi kwa njia ya kunyonya raia ambao sehemu kubwa ni masikini si katika sifa za uongozi bora. Huu utawala unarudi katika kipindi ambacho wachache wataneemeka sana, tunarudi awamu ya nne kiuchumi na ya tano kisiasa. Tayari kundi la wanasiasa limeashaanza kulalamika hasa baada ya kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa, lakini pia kurukwa kwa kihunzi cha katiba Mpya. Hili linaifanya ile Hiyena hiyena ya wanasiasa iliyoanza mwanzo kuondoka. Kundi la pili la Matajiri,, wafanya biashara wakubwa na wanyonyaji ambalo sitarajii kama litaguswa. Na hapa ndo itahitajikajika nguvu ya kuendelea kuwanyonya masikini kufidia haya Magap.
Tukumbuke kuwa kundi kubwa lilikuwa linamuunga Mkono Hayati ni kundi la watu wa chini ambao yeye mwenyewe alikwepa sana kugusa maslahi yao na alijinasibu kuwa ni Mtetezi wao. Hawa ndo walihuzunika sana wakati amefariki. Kwa haya mambo ya Kodi za kuumiza yaliyoanzishwa na Serikali ya SSH kupitia kwa wizara yake ya fedha na mipango chini ya Mh. Mwigulu Nchemba na kupata baraka za Bunge nachelea kusema kuwa soon Mama ategemee kupingwa vikali na kundi hili la tatu kwa sababu hata kundi la viongozi wa dini lipo nusu kwa nusu. Serikali ya Samia inaenda kukutana na Stunts za awamu iliyopita kuwa watu walikuwa wanamkumbuka JK. Nadhani wakati wa watu wa tabaka la chini kumkumbuka mtetezi wao linakuja.
Kundi la tabala la chini sasa limeanza kulalamika kuwa Serikali inatunyonya, mbona hakuna hela mitaani,n.k linaanza kuongezeka taratibu. Hili kundi likikubali kupata msukumo wa kundi la wanasiasa ambao tayari ni kama wameshavunja mahusiano na Mama basi SSH atapata lawama kubwa. Inasikitisha na kufikirisha sana Mama aliwananga TRA kwa kupiga kodi za kuumiza wafanyabiashara wakubwa lakini ameshindwa kuzuia kodi mara mbili "Double Taxation" kwenye huduma moja kwa kubadili lugha na kuita "TOZO" tena kwa mtanzania ambaye haingizi chochote kama mfanyabiashara.
Nini lengo la "VAT"? .
Kwa muktadha huu nadhani majuma machache yanayokuja tutaanza kusikia vilio vya watu kusema ni heri ya Mwendazake hakutubana sisi masikini, ama kweli alikuwa Rais wa wanyonge, Rais wa Mama Ntilie, Rais wa bodaboda, Rais wa wamachinga , n.k ambao na ni watumiaji wakubwa wa Miamala ya simu.
Tumeambiwa tusubiri fedha itaingia mtaani, Hivi aliyezungumza hili alimaanisha au alikuwa anatania?.
Huu ni muelekeo wa kumpa ahueni Mtanzania wa chini kiuchumi?.
Kwa staili hii ya SSH administration hakika nimemuelewa Jiwe aliposema "