Kuna clip moja ambayo vyombo vya habari wanairudia rudia mara kwa mara.
Clip yenyewe ni moja ya hotuba ambazo hayati Magufuli alizitoa wakati wa uhai wake.
Maneno yanayosemwa kwenye clip hiyo ndiyo ambayo ni mada yangu kuu, kwenye uzi wangu huu.
Anatamka kuwa "Mtanikumbuka kwa mema wala si kwa mabaya yangu, nawasihi tusibaguane kwa vyama vyetu vya siasa, wala ukabila na udini na kamwe tusiache kumwabudu Mungu wetu" mwisho wa kunukuu.
Kwa maelezo hayo na namna alivyokuwa akiiendesha nchi hii vina umbali kama kutoka mbinguni hadi duniani!
Hebu turudie baadhi ya matamshi yake wakati akiwa hai.
Mkinichagulia mpinzani mtakuwa mnajichelewesha wenyewe maendeleo yenu!
Nyinyi wenyewe ndiyo mlifanya makosa safari iliyopita kwa kuchagua mbunge wa upinzani, safari hii msirudie kosa hilo!
Kaskazini (hususani mkoa wa Kilimanjaro) mlipendelewa sana katika awamu zilizopita, hivi sasa na nyinyi subirini, wakati maendeleo ninapopeleka kwingineko(akimaanisha mikoa ya kanda ya ziwa)
Wakati akiyatamka maneno hayo, alijua fika kuwa nchi yetu toka tupate Uhuru, imejengwa katika misingi ya umoja wa kitaifa, ambayo hatubaguani kwa vyama vya siasa, ukabila wala dini zetu, kwa maana nyingine ni yeye aliyetaka kuligawa Taifa hili.
Vile vile akifahamu kuwa tokea mwaka 1992, nchi yetu iliandika ndani ya Katiba ya nchi kuwa nchi yetu itakuwa ya mfumo Wa vyama vingi, jambo ambalo hayati Magufuli, alionekana wazi wakati Wa uhai wake kuwa anauchukia mfumo huo na alikuwa akitamani nchi yetu irejee kwenye mfumo wa chama kimoja!
Lakini haishangazi kwa hayati Magufuli kutamka maneno hayo, kwa kuwa tunajua fika kuwa alkkuwa ni mtu wa "double standards"
Anatamka Leo kuwa maendeleo hayana chama, wakati kesho yake anawaambia wapiga kura kuwa msinichagulie betri na gunzi!