Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Wewe unaelewa nini kama sio mihemko tu unaweza kumlamisha mtu kuhama chama? Mbona hamkuwalazimisha wasihame Hivi mtu smart kama Davd Silinde anaweza kubakiana na aina ya upinzani uliokuwepo.
Kwahiyo wale 19 walihama kwa kupenda? Mpaka yule aliyekuwa mahabusu nae alihama kwa kupenda? Wewe huna ujualo nyamaza...

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Facts are very stubborn, waTz wabishi kweli na matusi, government ya tz is very unprofessional we pray for a peaceful transition
Spana Bado zipo palepale buda
IMG_20210322_203919.jpg
 
Kushughulika na kero za miaka nenda rudi na kutuaminisha kuwa tunaweza.

Kujaribu kutuheshimisha wananchi wa kawaida mbele ya watumishi wa umma.

Ile mentality ya ujanjaujanja aliyoikuza JK na kuwa siasa/nafasi za siasa ziikuwa za kununua kufutika kwa kiasi kikubwa.
Wokee ila waliopewa nafasi za upendeleo kutoka upinzani baada ya kuunga mkono juhudi tusiwaseme maana mwendazake hatajwi kwa ubaya.
 
miungu watu maofisini walinywea! Heshima kwa watumishi wa chini na wa Kati ilirejea na kuimarika. Mishahara na pensheni ya mwezi kea wastaafu kutoka kea wakati.
 
Nitamkumbuka kwa kuhamishia makao makuu Dodoma! Huu ni mfupa uliokuwa uliokuwa umeshindikana kwa miaka nenda rudi!!
 
Kutukwamisha mtaani miaka 5 bila ajira sitomsahau kamwe Mana amenintoisha vya kutosha
 
Poleni Sana waombolezaji wenzangu.

Tunapomuaga aliyekuwa Rais marehemu JPM ,tukumbuke kwamba kumuenzi na kumkumnuka kiongozi au mtu yeyote ni lazima tuangalie pande zote mbili.

Tutamuenzi kwa mema yake kama ujasiri,uthubutu na kutenda anachokiamini bila kujali wengine wanataka nini.The no nonsense president.

Upande wa pili,tutakukumbuka kwa mabaya kwa kujifunza kutorudia makosa yake kama kauli za kugawanyisha jamii,ubabe ,kutoheshimu utaratibu na kutotaka kabisa kukosolewa iwe kwa nia njema au mbaya.Demokrasia ilikuwa ni matusi kwa utawala uliopita.Ni vyema haya mambo yasijirudie tena.

Kwa heri mwanakwenda zake,leo yako kesho yetu.
 
Tanzania ina watu 61.5M kati ya hao wenye zaidi ya umri wa miaka 35 ni asilimia 20% au 12.5M. Hii ndiyo sababu kubwa tunaona kama vile nchi yetu ni ya kishabiki ni kwasababu kuna madogo wengi ambao wengi wao bado hawana upeo wa kutosha kuangalia mambo kwa upana wake.

Swali langu linatokana na ukweli kwamba wanasiasa wanapenda kujibinafisisha miradi ili wasifiwe na ndiyo maana miradi mengi ya nyuma Raisi ajae anaifanya yake. Mfano kwenye treni tutaambiwa Magufuli alianzisha lakini mwingine ndiye kasimamia na kukamilisha. Hii imekuwepo kwa miaka yote na nchi zote hivyo sio sisi tu. Tofauti yetu tuna madogo wengi hivi ni vigumu wa wenyewe kujua umuhimu wa miradi iliyofanywa na Magufuli. Hivyo tunavyosema Watanzania wengi tuelewe tuna wengi ambao bado ni wa kufuata mkumbo.
 
1.Chato International Airport
2.Chato National Park
3.Trafic light Chato
4.3 star hotel Chato (TANAPA)
5.Bohari ya kanda madawa Chato
6.Hospital ya rufaa Chato
7.Stadium (proposa)
8.CRDB Chato
Kwani kuna ubaya gani hapo au ulitaka wajenge kwenu hayo ni mawazo finyu
 

This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti ( Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss , kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo..

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J.. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje , kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu , S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.


Itaendelea...

PIA SOMA>> TANZIA - Rais John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
Kwa mengi lakini funga kazi ni "baki na mavi yako nyumbani"!
 
Ninti wapinzani wa Tz ndiyo mnao mkataa lakini wa nchi za nje na zenye maendeleo wanamkubali waziwazi huo ni unafiki wenu tu.

Kiongozi atakae wachekea cdm watamtia dole akiwa amesimama kwani ni vigeugeu na ni watu wa kulialia tu.

Hakuna kama JPM na hakuna atakaefanya kazi na cdm ktk utawala wote wa Tz
Andiko lako lote linaonyesha wewe ni kama mlevi tu!

Huna uwezo wa kujadili lolote.
 
Nina shida huwa sikumbuki chochote aka kichwa cha panzi.
 
Hadi muda huu nshasahau ..nakula bia tu tunagonga cheers tu hapa
 
1.Kaondoka wakati hahitajiki.

2.Kuteka wapinzani wake kama akina Azory Gwanda.

3.Kutesa wapinzani wake.

4.Kuua wapinzani wake na wakosoaji wake kama akina Ben saanane na kuwapiga wapinzani wake risasi kama ilivyokuwa kwa Tindu Lissu.

5.Kuua vyombo vya habari.

6.Kuua uhuru wa kujieleza.

7.Kuiba kura.

8.Kuua biashara za watu kupitia sera mbovu za uchumi.

9.Kudanganya katika takwimu za uchumi wa nchi.

10.Kuweka mihimili yote mitatu mfukoni mwake.

11.Kuua uchumi wa nchi kupitia sheria mbovu za uwekezaji.

12.Kuua watu kwa Corona kupitia leadership negligence.

13.Kuhakikisha kuwa akina Ben Saanane na Azory Gwanda walikipata cha mtema kuni.

14.Ukabila kwa kuhamishia rasilimali nyingi za nchi Chato na kujaza wasukuma serikalini.

15 Ukanda kwa kupeleka SGR mwanza wakati siyo economic strategic zone.

16.Ubaguzi wa rangi kwa kuwakandia wanawake weusi.

17.Kugandamiza demokrasia kwa kukataza vyama vya upinzani kufanya siasa wakati CCM kufanya siasa ni ruksa.

18.Kunyanyasa malaika-watoto wa kike wasirudi shule wakipata mimba.

19.Ufisadi wa kutisha kwa kufanya miradi mikubwa bila budget kupita bungeni.

20.Wizi wa kutisha wa mali ya uma kupitia Mayanga constructions LTD.

21.Kubambikizia kesi za kuhujumu uchumi wapinzani wake nchi nzima
 
Magufuli kabadilisha makao makuu ya waislamu BAKWATA Kinondoni mbali na mambo mengine mengi. Hivi angetoa kanisa ingekuwaje? Hivyo, waislamu muombeeni sana Magufuli.
 
Back
Top Bottom