Kuna kikundi kimekua kikisisitizia kauli ya marehemu mwendazake ya"mtakuja kunikumbuka",kana kwamba tulifanya kila liwezekanalo kumuondoa madarakani.
Mwendazake kachukuliwa na Muumba,na zaidi hata tulipotaka kuujua ukweli juu ya shida yake kama anaumwa ama vp,ili tumuombee apone maake tulikua tayari tushaamua kuishi nae ,bado tulifichwa.
Haina haja ya kutoa toa iyo kauli,sababu hatukua na uwezo wowote wa kupinga alichohitaji,hakuna chombo chochote cha habari ,wala mitandao ya kijamii iliyokua na ubavu wa kumuwekea kauzibe kwenye utendaji wake wa kazi.
Yaani katika marais waliofanya kazi bila presha basi mwendazake alikua free saaana,hapingwi na bunge,wananchi wala media.
So kusema kwamba tutakuja kumkumbuka ndio kweli tutamkumbuka kwa mema aliyofanya lakini hatujawahi kufanya jaribio loloooooote la kumuondoa mwendazake,aidha MAANDAMANO,BUNGE,kila aliyefanya hivyo nadhan inajulikana kilichomkuta.
Kusema kwamba tutakuja juta ni sawa na kuwa na mpenzi wako kila siku analalamika utakuja mkumbuka na wakati haumfanyii chochote kibaya unampa kiiila kitu anaishi kulalalama tu.
.........