Uchaguzi 2020 Je, utampa Magufuli kura yako uchaguzi ujao?

Uchaguzi 2020 Je, utampa Magufuli kura yako uchaguzi ujao?

Hizi ni kula za Jf na wengi huwa hawapigi kura, ila mwenyewe anaweza asijipigie kura maana Corona sio mchezo.

Msifanye kosa tena mwez wa 10, ili kelele za Jf zipungue.
 
Corona kaingia mpaka Bungeni BAADA ya KUSHINDWA KUZUIA MIKUSANYIKO ISIYOKUWA YA LAZIMA.

SASA KUCHAPA KAZI NI KUCHAPWA NA KAZI.
Usiogope kwani hao ndo walitakiwa waupate ili watutetee tupate msaada hata wa chakula cha lockdown
 
Nani anawadanganya? Huko maambukizi yamedhibitiwa. Rwanda na Uganda wamesha anza ku relax taratibu kali za lockdown kurudi kwenye maisha ya kawaida.

Rwanda na Uganda pia hadi sasa hawana vifo vya Corona.

Nani anawadanganya mnamwamini?
Acha uvivu mnataka chakula cha bure. Nenda chapa kazi
 
Acha uvivu mnataka chakula cha bure. Nenda chapa kazi

Umegundua kuwa wakiwamo kina askofu Niwemugizi, Zitto, askofu Bagonza nk tunataka chakula cha bure? Looh! Utakuwa unajitambua wewe?

Usisahau kuja kufuta bandiko lako hili la kijinga jinga, tusubiri ugonjwa uchanganye. Mkiambiwa ugonjwa utachanganya mnakuja tena kijinga jinga mkidai tunaombea ugonjwa uwe mkubwa.

Ugonjwa utaacha kuwa mkubwa kwa kutokuwa na hatua madhubuti za kuudhibiti? Mnapanda bangi kisha mnataka kuvuna maharage?

Mnalipwa pesa ngapi kuunga mkono huu upuuzi wa kuwa mnapuliziwa virus vya Corona na mabeberu kwa sababu wanataka kuwakwamisha? Wawakwamishe kitu gani? Mbona kujimwambafai kijinga mno?

Elimu zenu ndiyo hizi za ma PhD ambazo hata mmasai asiye soma ana nafuu?

Wakuu upuuzi wenu una kera na hatutawaacha kutuletea vifo tukiangalia kama wana kondoo wapelekwao machinjoni.
 
Habari za mda huu.
Corona ni hatari kufata taratibu zilizoweka na wizara ya afya kujilinda na kuwalinda tuwapendao.

Niende kwenye mada chap chap.
Kumpa kura yangu ni Big No!

Vipi wewe ndugu yangu utampa kura yako?
Majukwaa ya kijamii yanatumiwa na watu wachache tabaka la wasomi na wenye nafuu ya maisha ambao kimsingi walio wengi hawaikubali ccm na viongozi wake kwa hiyo kutumia kipimo cha humu sio sahihi
Unfortunately watu wengi maskini au wanyonge na wasio na elimu ndio mtaji mkuu wa ccm na wao hawana uwezo wa kupata habari nyingi na kuzichambua hao watampigia kura na ndio huwa wanafurahia kuitwa wanyonge kwa vitu vidogo vidogo serikali ikifanya wanaona ni hisani.
 
Back
Top Bottom