Kwa mbali nakumbuka ile siku nduli Idi Amin alipotushambulia na kuteka sehemu ya Jamhuri yetu huku akitishia kuongeza mashambulizi hadi Bandari yetu ya Salama. Jemadari wetu Mkuu wakati huo, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hakutafuta pa kukimbilia kujificha na kututaka tusali, hapana.
Baada ya kutangaza tu kwamba tuko vitani, aliingia kazini kuwahamasisha wananchi na kuliongoza Jeshi la wananchi, JWTZ, kwa kazi moja tu, kumpiga adui. Na kweli nduli alitandikwa. Alipigwa hadi akaikimbia si tu ardhi yetu na mambo yakaishia hapo, hapana, alizidi kutandikwa hadi akaikimbia na nchi yake Uganda.
Naam, hivyo ndivyo ilivyo, Kamanda na Jemadari Mkuu hakimbii uwanja wa vita akawaacha askari wake mikononi mwa wahuni kama Bashite.
Rais wa awamu ya kwanza wa Tanzania, Mwl. J.K Nyerere na makamanda wa Jeshi.
Hapa Kamanda wa kweli na Jemadari Mkuu, Mwalimu Nyerere, yupo juu ya tanki la jeshi, kifaru, uwanja wa vita!
Tukumbuke tunapomchagua Rais, tunamchagua Kamanda na Jemadari Mkuu ambaye atakuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya adui anayeonekana na asiyeonekana na si anayejificha mapambano yakipamba moto...ni hayo tu!