Je, utumiaji wa kiyoyozi(AC) unaongeza matumizi ya mafuta kwenye gari?

Upo mwingine wa kero za madereva jijini sijaona mchango wako na amekuita.

Natumia tab hapa mobile version sipati nitification ngoja niende kaka!!!!

Naona mnashambulia hii kitu sawia!!!!
Congrats
 
Hapana, haijachoka kihivyo; ndio ina mwaka wa pili barabarani; bado iko njema sana.

room kubwa sana ndio maana nguvu nyingi inatumika kupooza.....imagine 2000cc yako inapooza room mara mbili ya gx 110 lazima gari yako kwenye mlima gari itafeel strain...
 
Hizi mada zina wenyewe bwana...mimi naperuzi tu wala sihitaji kudadisi maana hata gutta sina
 
OLESAIDIMU, MANI, RRONDO: Thanks very much, uzi haukunilenga lakini nimepata mwanga wa tatizo langu; nitafuatilia na nadhani kitasomeka.
 
OLESAIDIMU, MANI, RRONDO: Thanks very much, uzi haukunilenga lakini nimepata mwanga wa tatizo langu; nitafuatilia na nadhani kitasomeka.

karibu.
 

Hii uliyousema ni sahihi ukiwa safarini. Lakini AC inaongeza ulaji wa mafuta gari ikiwa sailensa( kiswahili). Fanya majaribio gari hizi mbili: Noah na RAV4( chukua Old model na Medium Model/ Kill time) . Jumamosi saa6 mchana wiki ya kwanza washa RAV4 model yoyote ukiwasha AC ukitokea mfano Magomeni na Mafuta ya elfu20, lengo uende Kigamboni. Ukifika ferry kule foleni utakuta inaanzia fence ya Ikulu. Hadi unavuka na gari kwenye Pantoni angalia mafuta yako. Rudia zoez hilo bila kuwasha AC kwa RAV4 na pia Rudia kwa NOAH utaratibu uleule halafu uje utupe majibu. Kwa magari madogo yenye cc less than 1998(say 2000) unaweza usione ulaji wa mafuta. Ila kwa NOAH, RAV4 AC kwenye foleni usipime, ila ukiwa safarini ni poa tu, adui nkubwa ni foleni yaani gari kuunguruma, mafuta yanaenda sana tena sana!
 

Nkubwa haha ha! Mkubwa! Keypad heruf N na M ziko jirani! SOORRRY!
 
Hizi mada zina wenyewe bwana...mimi naperuzi tu wala sihitaji kudadisi maana hata gutta sina

Kaka vitu vingi tu huna na unavijua na unavitumia!!!!!

Unahitaji mifano???!!!!
Una mke au mpenzi???!!!
 
OLESAIDIMU, MANI, RRONDO: Thanks very much, uzi haukunilenga lakini nimepata mwanga wa tatizo langu; nitafuatilia na nadhani kitasomeka.

Pamoja sana kaka nawe ukituletea unayojua itakuwa safi sana haswa utayogundua kwa mafundi!!!!
 

uliyosema ni sahihi kabisa, lakini hata usipowasha AC kwenye foleni mafuta yanaenda bila wewe kusogea. hapa tunawalenga wale WANAOENDESHA VIOO WAZI WAKIAMINI WANA-SAVE MAFUTA....hatuzungumzii gari imekaa masaa mawili kwenye foleni.

gari ikiwa idle bila AC rpm itakuwa 500-600 hivi....ukiwasha AC inapanda hadi 800-1000 hivi...hapo inaonyesha gari inatumia extra energy lakini ukiwa unamove hata usipowasha AC rpm itakuwa lets say 3000 na ukiwasha AC inakuwa hapo hapo 3000....sasa ukizima na ufungue vioo kisa AC inakula mafuta utakuwa unajidanganya.
 

Tatizo wewe gari umeweka vioo vya giza wakati mwenzio anataka aonekane yumo ndani ya mkoko!!
 
Mi nimeona nikiwashs AC wakati wa kupanda milima gari hupungua nguvu, nikizima inakuwa na nguvu kawaida. Sijui hii ni kwa gari yangu tu au wengine nanyi mmeliona hilo? Naomba uzoefu wenu tafadhali.

Kuna uwezekano compressor ina shida. Peleka kwa fundi wakuchekie. Nina uzoefu na hilo
 
Kaka vitu vingi tu huna na unavijua na unavitumia!!!!!

Unahitaji mifano???!!!!
Una mke au mpenzi???!!!

Anaweza kuwa ana mke/mpenzi lakini anavyovitumia toka kwao nina hakika sio vya kwake!!
 
Kwa kweli mimi manufaa au faida za kuendesha gari na ac ni kubwa kuliko hayo madai ya consumption! Unakuwa ndani ya gari majasho kila mahali hapa Dar kisa extra consumption ambayo ni almost negligible!

Unakuta gari mavumbi kila mahali. Ukipita kidogo kwenye njia ya vumbi ukapishana na gari nyingine unafanyaje?

Mwingine ni ubahili tu
 

Asante sana kwa taarifa hii kwani page inayofuata kwenye ile link inaonyesha kwa uwazi kabisa kwamba spidi ndogo ni windows down.
 
♥Katika vitu ambavyo sitokuja kufanya ni kuendesha gari huku nimeshusha vioo sio kwamba napenda a/c la hasha naogopa vumbi kuingia ndani ya gari maana impact yake ni kubwa kuliko kuwasha a/c

♥kuna wadau wanasema ukiwa kwenye speed kama 100 weka Neutral(free) iende yenyewe ili kusave mafuta sijui kuna ukweli hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…