Je, uvaaji kofia ni kinyume na maadili ya mtanzania?

Je, uvaaji kofia ni kinyume na maadili ya mtanzania?

Wazee sugu
FB_IMG_1554630916427.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka niliwahi kuvaa cap, Niko Taifa getini nasuburi kuingia uwanjani kucheki mpira, mama yuko kwenye gari kanicheki naludi home siku alisema ile sikuwahi kuvaa tena ila napenda mno.
Achana na maswala ya mama, cha msingi uwe na kinywele cha kutolea nyuma ya cap 😍😍😍
 
Kuna kipindi hubby alinunua cap..nikamwambia mbn unavaa kofia unakuwa km mhuni mhuni vile..akaniambia ninaficha upara...sasa sk 1 kaivaa..boss wake akamu0na akamwambia na ww ushakuwa mhuni sasa kwann unavaa kofia..???toka pale akaacha..kwakweli mwanaume anayevaa kofia awe btn 30 -50 mimi kwangu namchukulia MUHUNI..hana tofauti kbs na mdada anayechomekea dera kwa nguo za ndani!
Jitafakari bestundefinedundefinedundefinedundefinedundefined
huu mtazamo wako aiseee kwamba ni uhuni naona umekaa kikoloni sana
 
Habari ya 'weekend' wakuu?

Mimi nimekuwa mpenzi sana wa uvaaji kofia. Na kofia ninayoipendelea zaidi ni zile wazungu waziitazo Ivy Caps.

Lipo jambo moja ambalo nimelishuhudia tangu ninakua, ni kuwa ukikutana na mtu aliyekuzidi umri then ukawa unamsalimia basi ile kofia unaivua, baada ya salamu unaivaa. Nami kwa kufuata mazoea basi huwa nafanya hivyo pia.

Basi leo nimemsaliamia mzee mmoja nikajisahau kuivua, yule mzee hakuonesha kukwazika, kinyume na nilichokitegemea.

Swali ninalouliza, je uvaaji kofia ni ishara ya uhuni kwa mila zetu watanzania? Au ni baadhi ya makabila tu?

Na kutovua kofia wakati wa salam je nao ni uhuni?

View attachment 1056316View attachment 1056317View attachment 1056318

Sent using Jamii Forums mobile app

HAPANA, kuvaa kofia si uhuni ni kama vazi lingine, ISIPOKUA unaposalimiana na mkubwa unapaswa kuvua kofia, hii ni alama ya utii. Ni mambo ya kistaarabu tu!

Nakumbuka nikiwa mdogo maza alininunulia kapelo sema mzee wangu alikua anaishi town so ilikua nikiwnda kumsalimia kabla ya kusalimia maza alikua ananiambia vua kofia!
 
Mpaka leo nchi kama Uingereza unapokutana na mtu anayekuzidi cheo au rika, ukimsalimia unavua kofia na baadaye unavaa. Nadhani hii ni ile tumerithi toka kwa waingereza au kama ilikuwepo sijui maana sisi wa mikoani kuondoa waislam, wazee wetu huoni picha yoyote ambayo walivaa kofia.

Wanaonekana wamevaa kofia mara baada ya kuathiriwa na kasumba ya waarabu, wajerumani na waingereza. Hii si mila ya kitanzania ila ni mila ya kuletwa. Kama kuna kabila lilivaa kofia naomba lije linikosoe. Tusihusishe dini na mila zetu za asili.

British civilization!
 
Back
Top Bottom