CHESEA INGINE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2010
- 200
- 48
Tusiangalie Kabila tuangalie mchapa kazi aweke Taifa na watu wake mbele. Na awe na taaluma na uwezo wa kuifanya kazi yake kwa ufanisi na kwa manufaa ya Taifa na watu wake basi!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
A MODEST PROPOSAL
Na. M. M. Mwanakijiji
Kuna vumbi la chuki, fitina, wivu, kisasi, na hisia za kibaguzi dhidi ya jamii ya Wachagga nchini. Kuna kila dalili kuwa jamii ya Wachagga nchini siyo tu inaanza kutengwa lakini uwepo wake katika nafasi mbalimbali za uongozi inazua hoja ya ukabila kwa haraka zaidi yawezekana kuliko kabila jingine lolote nchini. Katika Tanzania yetu, wachagga wameanza kunyoshewa kidole siyo kwa siri tena bali kwa wazi kabisa tena na watu ambao wakati mwingine hawapati hata kigugumizi.
Ubaguzi huo msingi wake mkubwa ni idadi ya wachagga katika nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kuhusiana na elimu yao. Kuanzia mara tu baada ya uhuru jamii ya wachagga mojawapo ya jamii ambayo watu wake wengi wamesoma sana na kufanikiwa kielimu na kiuchumi imekuwa ikinyoshewa kidole cha kupendelewa.
Mtu yeyote ambaye anaweza akafanya uchambuzi yakinifu hatoshangaa kukuta wataalamu wa kichagga katika nafasi mbalimbali za uongozi au taaluma nchini. Kwenye vyuo vikuu, kwenye idara za serikali na hata kwenye taasisi binafsi kumejaa watu wenye asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hususan watu wa jamii ya Kichagga.
Endapo itatangazwa nafasi yoyote ya kitaalamu usishangazwe ukiona kuwa waombaji wengi wana majina ya "Kichagga".
Ni kwa sababu hiyo basi kuna kila dalili kuwa kutokana na wingi wao katika nafasi muhimu na vyeo mbalimbali (hata ndani ya Jeshi la Polisi) Wachagga siyo tu ni wengi lakini wanaonekana kufanikiwa zaidi. Hili ni tishio kwa baadhi ya watu. Ni tishio kwa watu ambao hawako tayari kuangalia jitihada za watu katika kufanikiwa kwao na matokeo yake kushutumu ukabila kila idadi ya Wachagga kwenye kitengo fulani inazidi mmoja.
Ushauri wangu ni kuwa, kwa vile Wachagga wameshasoma sana na kuendelea katika biashara karibu mikoa mingi nchini. Na kwa vile wanaendelea kufanikiwa pia katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini, basi itakuwa vizuri kama watajitolea kuachilia nafasi hizo ili kuwapa nafasi watu wa makabila mengine.
Kwa vile ni wao wanaonekana kulalamikiwa kutokana na mambo ya kifisadi aidha kwa moja kwa moja au kwa kuashiria basi ni vizuri wawape watu wengine nafasi hizo hata kama watu hao hawajasoma sana. Hii yote itakuwa ni katika kudumisha mshikamano, umoja na udugu wa Taifa letu.
Endapo Wachagga wataachilia nafasi mbalimbali kama UCEO, Ukurugenzi, Ukuu wa Idara n.k watasababisha watu wawapende na kuwakubali kuwa ni wazalendo wa kweli. Sitoshangaa kuwa ndugu zetu wa Jamii ya Kichagga wakikaa pembeni, basi ufisadi utakoma serikalini, idara zitaongozwa na watu wazuri, na mara moja na daima Tanzania itaanza kukua katika uongozi.
Kwa kupendekeza nashauri wabunge wote ambao ni Wachagga au wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro kuachia ngazi mara moja ili watu wa makabila mengine wapewe nafasi hizo. Siyo wao tu bali pia wabunge ambao wameoa au kuolewa uchagani vile vile wafuate nyazo hizo.
Wakishamaliza hao, wakuu wote wa idara za serikali ambao wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hasa wa jamii ya kichagga (wamarangu, wamachame, wa Rombo, na wa Kibosho) na wao waamue kuachilia nafasi hizo kwa ndugu zao Wamakua, Wamwera, Wa Ndali, Wadigo n.k Katika hili Wapare hawahusishwi.
Tukishamaliza wakuu hao wa idara za serikali ningependekeza madaktari wote wenye kumiliki hospitali binafsi ambao ni wachagga au wameoa/kuolewa uchagani na wenyewe waamue kuingia ubia na watu wa makabila mengine kama wangengereko, wambuu, na wanjiro ili hayo makabila madogo na wenyewe wapate nafasi ya kujifunza fani hizi muhimu.
Zaidi ya yote, majaji na mahakimu wote ambao wana asili ya Uchaggani na wenyewe waamue kujitoa katika nafasi hizo kwani wingi wao pia unaonekana sana na hivyo kuwa kikwako kwa watu wa makabila mengine kufanikiwa zaidi katika nyanja ya sheria. Kwanza kabisa wale majaji wa Kichagga wa mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu wawe wa kwanza kuweka manyanga chini.
Katika kufanya hivyo jamii ya Watanzania ambao inaona ukabila wa wachagga katika sehemu nyingi itaridhika kwani kwa mara ya kwanza tutakuwa tumeshughulikia chanzo cha matatizo yetu mengi.
Very amazing thread!!! Lakini cha ajabu zaidi ni kwamba MODs wengi humu wameunga mkono!!!! Mmmmhhhhh huu mwendo sio kabisa!!! Anyway tuyaache hayo, tuje kwenye hoja..In my view, it's very asinine to believe in that!!!
Nadhani inabidi kina Mangi Mareale warejee harakati zao za kuomba uhuru wa Wachagga maana washaanza kunyanyapaliwa ndani ya nchi yao... Naogopa yanaweza kutokea yale waliyofanyiwa Wayahudi kule Ujerumani ya zama za Hitler. Ni kweli kwamba kuna hisia mbaya sana dhidi ya Wachagga sasa hivi tofauti na zamani kama MK anavyosema. Hii 'PREJUDICE AGAINST CHAGGA' ifanyiwe kazi haraka laa sivyo kunaweza kukatokea 'CHAGGA GENOCIDE' kama ile ya Bosnia.
Binafsi kuna vitu vinanishangaza sana kuhusu dhana hii ya UCHAGGA. Kuna wakati mwingine unaenda kufanya job interview hata kama unatumia surname ya kisukuma ( na pengine ndio kabila lako) bado unajengewa hisia kuwa wewe ni mchagga eti kwasababu una muonekano wa sura za watu wa kaskazini!!!!
Kuna makabila ambayo watu wake wana sura zenye muonekano wa Kichagga. Mfano ni Wapare, Wanyaturu, Wanyiramba, Wameru na baadhi ya watu wa makabila ya mkoa wa Tanga (kama Wasambaa). Wasiwasi wangu ni kwamba any Prejudice against Chagga itadhuru watu hao pia.
Lakini swali kubwa la kujiuliza ni Je kwanini chuki hii imeshika kasi sasa???
Haki mwanajiji umefisika kimawazo na sio siri tena mwenzangu heshima yangu kwako imefikia kikomo kutokana na hizi pumba ulizo wakilisha hapo. Na muomba mungu akusamehe bure.
Siamini unaweza kuandika thread kama hii yenye mtazamo potovu. Kwa bahati kwangu mimi nimekuelewa kuwa una "unfounded bitterness". Mungu alichokujalia usikitapanye ukawapa nguruwe au kunguru. Peleka watoto wako shule washindane na wachaga na wengine kwenye nafasi unazozitamani.
Thanks.
A MODEST PROPOSAL
MMKJ
Mimi si Mchaga.
Lakini kwa hakika mawazo kama haya ni hatari kwako,kwa watanzania wengi na hasa wachaga unaowabagua
Matatizo ya kijami(Social inequality is every where in this world)Na kushauri utafute Sociologist akusafishe mawazo hayo.
Nawapa moyo wote wanaopiga vita hatred kama hii.
virseversa kijana
Nonsense. Stupid topic. Erase those hateful idea of yours frm inside u o,u wl hate Chagga' tu
Labda niwasaidie watu ambao wanakuja hivi karibuni na kukuta hii mada bila kuisoma katika context ya kile kilichokuwa kinaendelea mwaka 2008. Mara nyingi sipendi kufafanua sana maandishi yangu lakini nadhani kuna watu wataamka wakisoma hii madonge yanawashika kwani wananishangaa. Nitasema kwa kifupi:
a. Tulipoanza mtandao huu wa JF kulikuwa na sentiments ambazo zilikuwa zinaenezwa na kundi la watu fulani ambao miongoni mwao ni watu wakubwa na baadhi walikuwa kwenye balozi zetu. Sentiments hizo fundamentally zilikuwa ni anti-chagaism. Yaani, chuki ya wazi dhidi ya Wachagga.
b. Katika kueneza sentiments hizo kulikuwa na majaribio kadha wa kadha ya kuwabebesha Wachagga lawama za kila namna na nakumbuka kuna mtu ambaye nilipomuuliza swali la "sasa tufanye nini na Wachagga" alinijibu "Kwani Hitler alifanya nini na Wayahudi". Hadi leo bado kuna hizo hisia ambazo zinaendelea kuenezwa kiasi kwamba ninaamini kabisa kuwa kati ya jamii za Watanzania ambao wanatishiwa na chuki ya kikabila ni Wachagga.
Hivyo, makala hii iliandkwa as a parody ya logical progression ya wale wanaotaka Wachagga walaumiwe na wabebeshwe mzigo wa kila kitu kwa sababu wanaonekana wamefanikiwa na tayari wako katika nafasi nyingi. Na katika hivi mmeweza kuona watu ambao wanaunga mkono waziwazi hizo chuki na watu hao wengine bado wapo serikalini na wengine wanapangwa kushika nafasi mbalimbali za juu (wengine tayari wameshika) na ambao wakipewa nafasi ya kuajiri watu- wataangalia makabila ili kuhakikisha Wachagga "hawajazani". So, badala ya kusoma hiyo thread ya kwanza ukang'aka, take your time to read earlier posts ili uweze kuelewa ni kwanini tulizungumza hivyo.
Kama kila fasihi itahitaji kufafanuliwa na mwandishi itakuwa ni kazi kubwa sana.
Ukianza kuzungumzia kabila mojamoja nadhani tutarudi kulekule kwenye dhana ya ukabila.So watch out!!!Proposal yako imewasahau Wahaya pia!!