Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Status
Not open for further replies.
Tusiangalie Kabila tuangalie mchapa kazi aweke Taifa na watu wake mbele. Na awe na taaluma na uwezo wa kuifanya kazi yake kwa ufanisi na kwa manufaa ya Taifa na watu wake basi!
 
A MODEST PROPOSAL

Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna vumbi la chuki, fitina, wivu, kisasi, na hisia za kibaguzi dhidi ya jamii ya Wachagga nchini. Kuna kila dalili kuwa jamii ya Wachagga nchini siyo tu inaanza kutengwa lakini uwepo wake katika nafasi mbalimbali za uongozi inazua hoja ya ukabila kwa haraka zaidi yawezekana kuliko kabila jingine lolote nchini. Katika Tanzania yetu, wachagga wameanza kunyoshewa kidole siyo kwa siri tena bali kwa wazi kabisa tena na watu ambao wakati mwingine hawapati hata kigugumizi.

Ubaguzi huo msingi wake mkubwa ni idadi ya wachagga katika nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kuhusiana na elimu yao. Kuanzia mara tu baada ya uhuru jamii ya wachagga mojawapo ya jamii ambayo watu wake wengi wamesoma sana na kufanikiwa kielimu na kiuchumi imekuwa ikinyoshewa kidole cha kupendelewa.

Mtu yeyote ambaye anaweza akafanya uchambuzi yakinifu hatoshangaa kukuta wataalamu wa kichagga katika nafasi mbalimbali za uongozi au taaluma nchini. Kwenye vyuo vikuu, kwenye idara za serikali na hata kwenye taasisi binafsi kumejaa watu wenye asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hususan watu wa jamii ya Kichagga.

Endapo itatangazwa nafasi yoyote ya kitaalamu usishangazwe ukiona kuwa waombaji wengi wana majina ya "Kichagga".

Ni kwa sababu hiyo basi kuna kila dalili kuwa kutokana na wingi wao katika nafasi muhimu na vyeo mbalimbali (hata ndani ya Jeshi la Polisi) Wachagga siyo tu ni wengi lakini wanaonekana kufanikiwa zaidi. Hili ni tishio kwa baadhi ya watu. Ni tishio kwa watu ambao hawako tayari kuangalia jitihada za watu katika kufanikiwa kwao na matokeo yake kushutumu ukabila kila idadi ya Wachagga kwenye kitengo fulani inazidi mmoja.

Ushauri wangu ni kuwa, kwa vile Wachagga wameshasoma sana na kuendelea katika biashara karibu mikoa mingi nchini. Na kwa vile wanaendelea kufanikiwa pia katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini, basi itakuwa vizuri kama watajitolea kuachilia nafasi hizo ili kuwapa nafasi watu wa makabila mengine.

Kwa vile ni wao wanaonekana kulalamikiwa kutokana na mambo ya kifisadi aidha kwa moja kwa moja au kwa kuashiria basi ni vizuri wawape watu wengine nafasi hizo hata kama watu hao hawajasoma sana. Hii yote itakuwa ni katika kudumisha mshikamano, umoja na udugu wa Taifa letu.

Endapo Wachagga wataachilia nafasi mbalimbali kama UCEO, Ukurugenzi, Ukuu wa Idara n.k watasababisha watu wawapende na kuwakubali kuwa ni wazalendo wa kweli. Sitoshangaa kuwa ndugu zetu wa Jamii ya Kichagga wakikaa pembeni, basi ufisadi utakoma serikalini, idara zitaongozwa na watu wazuri, na mara moja na daima Tanzania itaanza kukua katika uongozi.

Kwa kupendekeza nashauri wabunge wote ambao ni Wachagga au wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro kuachia ngazi mara moja ili watu wa makabila mengine wapewe nafasi hizo. Siyo wao tu bali pia wabunge ambao wameoa au kuolewa uchagani vile vile wafuate nyazo hizo.

Wakishamaliza hao, wakuu wote wa idara za serikali ambao wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hasa wa jamii ya kichagga (wamarangu, wamachame, wa Rombo, na wa Kibosho) na wao waamue kuachilia nafasi hizo kwa ndugu zao Wamakua, Wamwera, Wa Ndali, Wadigo n.k Katika hili Wapare hawahusishwi.

Tukishamaliza wakuu hao wa idara za serikali ningependekeza madaktari wote wenye kumiliki hospitali binafsi ambao ni wachagga au wameoa/kuolewa uchagani na wenyewe waamue kuingia ubia na watu wa makabila mengine kama wangengereko, wambuu, na wanjiro ili hayo makabila madogo na wenyewe wapate nafasi ya kujifunza fani hizi muhimu.

Zaidi ya yote, majaji na mahakimu wote ambao wana asili ya Uchaggani na wenyewe waamue kujitoa katika nafasi hizo kwani wingi wao pia unaonekana sana na hivyo kuwa kikwako kwa watu wa makabila mengine kufanikiwa zaidi katika nyanja ya sheria. Kwanza kabisa wale majaji wa Kichagga wa mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu wawe wa kwanza kuweka manyanga chini.

Katika kufanya hivyo jamii ya Watanzania ambao inaona ukabila wa wachagga katika sehemu nyingi itaridhika kwani kwa mara ya kwanza tutakuwa tumeshughulikia chanzo cha matatizo yetu mengi.

Mwanakijiji unapaswa kuitwa PHYLOSOPHER, Makala yako ya miaka mitatu iliyopita mtu akiisoma leo utafikiri imeandikwa jana kutokana na matukio yanayoendelea nchini kwetu leo. Katika sentensi zote zilizokuwa na neno"Wachagga" substitute with"Wakristo" and makabila mengine substitute with "Waislam". Wanaokubali kutumiwa kama TP na wanasiasa kwa kuwa tu wamepewa rupia na kusahau kuwa dunia ni mapito na kila mchunga ataulizwa jinsi alivyochunga wale walio katika mamlaka yake.
 
Very amazing thread!!! Lakini cha ajabu zaidi ni kwamba MODs wengi humu wameunga mkono!!!! Mmmmhhhhh huu mwendo sio kabisa!!! Anyway tuyaache hayo, tuje kwenye hoja..In my view, it's very asinine to believe in that!!!

Nadhani inabidi kina Mangi Mareale warejee harakati zao za kuomba uhuru wa Wachagga maana washaanza kunyanyapaliwa ndani ya nchi yao... Naogopa yanaweza kutokea yale waliyofanyiwa Wayahudi kule Ujerumani ya zama za Hitler. Ni kweli kwamba kuna hisia mbaya sana dhidi ya Wachagga sasa hivi tofauti na zamani kama MK anavyosema. Hii 'PREJUDICE AGAINST CHAGGA' ifanyiwe kazi haraka laa sivyo kunaweza kukatokea 'CHAGGA GENOCIDE' kama ile ya Bosnia.

Binafsi kuna vitu vinanishangaza sana kuhusu dhana hii ya UCHAGGA. Kuna wakati mwingine unaenda kufanya job interview hata kama unatumia surname ya kisukuma ( na pengine ndio kabila lako) bado unajengewa hisia kuwa wewe ni mchagga eti kwasababu una muonekano wa sura za watu wa kaskazini!!!!

Kuna makabila ambayo watu wake wana sura zenye muonekano wa Kichagga. Mfano ni Wapare, Wanyaturu, Wanyiramba, Wameru na baadhi ya watu wa makabila ya mkoa wa Tanga (kama Wasambaa). Wasiwasi wangu ni kwamba any Prejudice against Chagga itadhuru watu hao pia.

Lakini swali kubwa la kujiuliza ni Je kwanini chuki hii imeshika kasi sasa???

mkuu mm mwenyewe sio mchaga ila nimetoka kwenye hayo makabila lakini watu wananiita mangi. .mi naona kama vipi nchi igawanywe ..watu wa kaskazini tusepe zetu huku juu
 
Haki mwanajiji umefisika kimawazo na sio siri tena mwenzangu heshima yangu kwako imefikia kikomo kutokana na hizi pumba ulizo wakilisha hapo. Na muomba mungu akusamehe bure.

soma tena vizuri kijana... Naona umedandia mshale
 
Siamini unaweza kuandika thread kama hii yenye mtazamo potovu. Kwa bahati kwangu mimi nimekuelewa kuwa una "unfounded bitterness". Mungu alichokujalia usikitapanye ukawapa nguruwe au kunguru. Peleka watoto wako shule washindane na wachaga na wengine kwenye nafasi unazozitamani.

mwingine huyu naye kadandia mshale..jamani mnasoma na hamuelewi kilichomo??? JF--home of....??? Utajaza.lets go MM
 
A MODEST PROPOSAL


MMKJ
Mimi si Mchaga.
Lakini kwa hakika mawazo kama haya ni hatari kwako,kwa watanzania wengi na hasa wachaga unaowabagua
Matatizo ya kijami(Social inequality is every where in this world)Na kushauri utafute Sociologist akusafishe mawazo hayo.
Nawapa moyo wote wanaopiga vita hatred kama hii.

virseversa kijana
 
Nonsense. Stupid topic. Erase those hateful idea of yours frm inside u o,u wl hate Chagga' tu

pole! Ila soma tena hii thread you gonna understand it rather thn mixing maziwa mtindi with chai hapa
 
Sijui hii ni hoja ya nguvu au nguvu ya hoja. Kila mtu mwenye elimu ana nafasi ya kulitumikia taifa letu ninavyojua wachaga wanakitu cha ziada "Kuthubutu" tujifunze kwanza kutoka kwao. Mbali na nafasi za ajira Serikalini wachaga wamefanikiwa kuthubutu kwenye sekta ya biashara na wamesambaa Tanzania nzima hata nchi za jirani mfano ukienda soko la mitumba Nairobi 'Kikumbaa' utakuta wamo huko kwa wingi wanafanyabiashara tena ni maarufu, Je! ukabila unaingia je hapo? Ni vema wananchi waangalie chanzo ni nini kuachwa nyuma kama ww utakaa barazani kutwa hata bustani ya mchicha ufikiri kuanzisha kuna wa kumlahumu kweli. Hayati baba wa Taifa alisema 'hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa fikra'
 
Labda niwasaidie watu ambao wanakuja hivi karibuni na kukuta hii mada bila kuisoma katika context ya kile kilichokuwa kinaendelea mwaka 2008. Mara nyingi sipendi kufafanua sana maandishi yangu lakini nadhani kuna watu wataamka wakisoma hii madonge yanawashika kwani wananishangaa. Nitasema kwa kifupi:

a. Tulipoanza mtandao huu wa JF kulikuwa na sentiments ambazo zilikuwa zinaenezwa na kundi la watu fulani ambao miongoni mwao ni watu wakubwa na baadhi walikuwa kwenye balozi zetu. Sentiments hizo fundamentally zilikuwa ni anti-chagaism. Yaani, chuki ya wazi dhidi ya Wachagga.

b. Katika kueneza sentiments hizo kulikuwa na majaribio kadha wa kadha ya kuwabebesha Wachagga lawama za kila namna na nakumbuka kuna mtu ambaye nilipomuuliza swali la "sasa tufanye nini na Wachagga" alinijibu "Kwani Hitler alifanya nini na Wayahudi". Hadi leo bado kuna hizo hisia ambazo zinaendelea kuenezwa kiasi kwamba ninaamini kabisa kuwa kati ya jamii za Watanzania ambao wanatishiwa na chuki ya kikabila ni Wachagga.

Hivyo, makala hii iliandkwa as a parody ya logical progression ya wale wanaotaka Wachagga walaumiwe na wabebeshwe mzigo wa kila kitu kwa sababu wanaonekana wamefanikiwa na tayari wako katika nafasi nyingi. Na katika hivi mmeweza kuona watu ambao wanaunga mkono waziwazi hizo chuki na watu hao wengine bado wapo serikalini na wengine wanapangwa kushika nafasi mbalimbali za juu (wengine tayari wameshika) na ambao wakipewa nafasi ya kuajiri watu- wataangalia makabila ili kuhakikisha Wachagga "hawajazani". So, badala ya kusoma hiyo thread ya kwanza ukang'aka, take your time to read earlier posts ili uweze kuelewa ni kwanini tulizungumza hivyo.

Kama kila fasihi itahitaji kufafanuliwa na mwandishi itakuwa ni kazi kubwa sana.
 
Labda niwasaidie watu ambao wanakuja hivi karibuni na kukuta hii mada bila kuisoma katika context ya kile kilichokuwa kinaendelea mwaka 2008. Mara nyingi sipendi kufafanua sana maandishi yangu lakini nadhani kuna watu wataamka wakisoma hii madonge yanawashika kwani wananishangaa. Nitasema kwa kifupi:

a. Tulipoanza mtandao huu wa JF kulikuwa na sentiments ambazo zilikuwa zinaenezwa na kundi la watu fulani ambao miongoni mwao ni watu wakubwa na baadhi walikuwa kwenye balozi zetu. Sentiments hizo fundamentally zilikuwa ni anti-chagaism. Yaani, chuki ya wazi dhidi ya Wachagga.

b. Katika kueneza sentiments hizo kulikuwa na majaribio kadha wa kadha ya kuwabebesha Wachagga lawama za kila namna na nakumbuka kuna mtu ambaye nilipomuuliza swali la "sasa tufanye nini na Wachagga" alinijibu "Kwani Hitler alifanya nini na Wayahudi". Hadi leo bado kuna hizo hisia ambazo zinaendelea kuenezwa kiasi kwamba ninaamini kabisa kuwa kati ya jamii za Watanzania ambao wanatishiwa na chuki ya kikabila ni Wachagga.

Hivyo, makala hii iliandkwa as a parody ya logical progression ya wale wanaotaka Wachagga walaumiwe na wabebeshwe mzigo wa kila kitu kwa sababu wanaonekana wamefanikiwa na tayari wako katika nafasi nyingi. Na katika hivi mmeweza kuona watu ambao wanaunga mkono waziwazi hizo chuki na watu hao wengine bado wapo serikalini na wengine wanapangwa kushika nafasi mbalimbali za juu (wengine tayari wameshika) na ambao wakipewa nafasi ya kuajiri watu- wataangalia makabila ili kuhakikisha Wachagga "hawajazani". So, badala ya kusoma hiyo thread ya kwanza ukang'aka, take your time to read earlier posts ili uweze kuelewa ni kwanini tulizungumza hivyo.

Kama kila fasihi itahitaji kufafanuliwa na mwandishi itakuwa ni kazi kubwa sana
.

Sizungumzi kishabiki japo simnyimi mjumbe yeyote haki ya msingi kuwaza hivyo....kwa moyo wa dhati nikushukuru Mzee Mwanakijiji kwa kufunga safari toka mbali( kuendeleza mambo ya msingi,ya kuipua mada fikirishi) na kurudi nyuma kutfafanua Fasihi ambayo kimsingi ni andishi...Binafsi nimekua nikipita mbali na thread hii kwa kua sipendi kuona nachohisi wengi wenye chuki zao binafsi watakua wamechangia...
Kuna wakati nimejikuta nimeingi abila kupenda na mara chache katika hizi hua nakumbusha Chuki na matamshi yoyote yenye kuzalisha chuki/kujenga hisia za chuki kwa tabaka fulani(sio kabila tu) baba wa Taifa keishaliweka kando zamani! Usichoke mkuu pale unapohisi kueleweka ndivyo sivyo! Na nionavyo ni busara kujua wazo kuu kwa kukaa pembeni badala ya kurukia maada na kusababisha usumbufu usio wa lazima!
 
Mada imeweka kila kitu cha wachagga kweupe kabisa na kuonyesha juhudi za wachaga jinsi zimeleta mguzo kwa jamii ya Tanzania,kwa mujibu wa sheria na katiba yetu kila mtanzania ana wajibu wa kulitumikia taifa lake na ajira zikitangazwa hasisemi tunataka kabila gani ila zinataja sifa za mwombaji, kwa hiyo mimi nilikuwa natoa rai kwa kila mmoja toka kila kabila kujitahidi kadri ya uwezo wake na tutakuwa sawa na hawa wachaga maana wanaonekana kila kona ya Tanzania na baadhi wapo nchi za watu mfano kule kule Mbosi Mbeya wapo akina masswe wanalima kahawa na viazi,ukifika Guangzhou China utakutana na Massawe Lodge,Shirima Moto shop ,Hong Kong Massawe lodge na pande nyingine

Kwa ujumla wachaga wapo kishule kwa sana,biashara ndiyo usiseme,ni wakulima wajanja na pia nafasi kwa serikali pia wamejaa sasa,hospital binafsi ukiangalia majina yake karibu asilimia 75% majina ya kichaga,kwa hiyo mimi naona kupambana kwa kila njia kama wao kwenye fani zote hata kama upo naye ofisini fanya kazi mafanikio yataonekana na sio tunakimbilia mihela ya lawama kama Meremeta,IPTL,RITEs,Dowans chini ya Mkwere maana angewainua wakwere kwenye elimu na biashara wangeweza kuleta ushindani zaidi ila yeye anawainua watu wa kuja ambao hata sio wazawa
 
HIvi hakuna watu waliowahi kusoma the original "A Modest Proposal" ambayo ndiyo iliinspire hiki nilichoandika?
 
sasa naona mmeanza ukabila ambao hauna tija kwa taifa, kama watu hawajasoma kwa nini wawekwe madarakani?
 
Mwanakijiji
Naomba nionyeshe Chuki yangu Binafsi kwa yote nijuwayo juu ya uadui wa kikabila na kupendeleana.

Nimeshindwa kupata chanzo/sababu ya hadithi yako maana kila ulichokiandika siamini kama ndo sababu ya hitimisho lako. Mchango wako au swali lako la wazi ungeuliza wazi wazi kabisa kwamba ni kweli wachagga wanashika nafasi nyingi kiasi hicho? Ni kweli ni kwa kupendeleana.

Unaeleza wachagga walivyosoma sana, kitu ambacho siamini sana kwa kutojua ‘kusoma sana' ina maana gani, maana kama ni Masters, Ph.Ds, nk. hapo siyo kweli maana niliwahi kuona ktk gazeti moja likisema wanaoongoza kwa viwango vya juu ni Wakerewe. Ni wilaya inayoongoza kwa idadi ya professors kuliko hata mikoa mizima mingi.

Kama nikushika nafasi, kweli kabisa wachagga wanaweza kuongoza ingawa sina takwimu ila hiyo ndo tunavyoona. Hapo sasa ndo ungetoa nafasi tujadili ni kwa nini wanashika nafasi zote hizo kwa wingi kiasi hicho. Jibu langu liko wazi:

Hebu kumbuka NBC ya Amon Nsekela, Kumbuka tena NIC ya Mwaikambo.

Hapo ilibidi kuhalalisha usomi wa watu wa Mbeya.

Huko nyuma kumbuka Waziri aliyeitwa Elinawinga, akisafirisha wanafunzi toka Kilimanjaro kwenda kusoma Kigoma, Mtwara, nk. Wakati huo huo akiwa hatoi nafasi ya mikoa mingine kuingia shule za Kilimanjaro. Baada ya miaka ikawa ‘wachagga wamesoma sana'. Ndo chanzo cha Nyerere kuingiza hiyo ambayo JokaKuu kaitaja kuwa ni QUOTA SYSTEM.

Lipo suala la Wakurya kujaa Jeshini na hasa enzi zile za interview ya kushindana mbio. Hawa hawakupendelewa na huko wachagga wasingeweza mbio za Wakurya. Ikawa kazi ya wasiosoma.

TRA ipo siku nyingi mara baada ya kuingia mtu wa Kilimanjaro, ghafla wachagga ‘wakasoma sana' kuliko makabila mengine na kushika nyadhifa. Angalia Wizara ya fedha baada ya kumpata waziri mpenda wasomi wa Kilimanjaro.

Hebu ingia ktk idara ndogo ndogo kabisa na hata tabia za mitaani ujiulize kwa nini ni rahisi Wachagga kufungua biashara na kuteka mji kama Arusha lakini si rahisi Mkinga kufungua duka mjini Moshi. Je wajua kwamba soft drink inayouzika mjini moshi ni Coca cola tu na Pepsi cola wamefulia! Kisa? Coca ni ya Mengi, Mchagga!

Kuna njama nyingi za ajira kiasi kwamba usipoambiwa undani utadhani kabila Fulani ‘limesoma sana'. Kuna nafasi za ajira pale TRA ziliwahi kuzuiliwa kwa miaka miwili, sababu kubwa ikiwa ni watu wa kabila la Wachagga waliokwenda kusoma hawajarudi. Waliporudi zikatangazwa. Kwa kuwa hawa walitumwa wakasome kitu Fulani kwa kulenga ajira fulani, hawakuwa na mpinzani ktk usaili maana walikuwa ‘wameshasoma sana'!

Haya yote siyo ya TZ tu. Kenya hili linawasumbua sana kiasi kwamba enzi za Moi ilibidi amteue Dr Leakey (UK origin) ili amsaidie kufanya reforms za idara yao ya utumishi. Na alianza kwa kuwafukuza viongozi wakuu ambao waliongoza ukabila. Bado hawajalimaliza.

Tusidanganyane hakuna cha kusoma sana ila kuna kupendeleana sana manaa ajira za serikali hazihitaji digrii mbili, tatu, nk. Kwani nikitaka Wasukuma 1000 walio na vyeti vya uhasibu nitashindwa kuwapata ili waishike TRA? Ufumbuzi realistic ni reform na kuwa wawazi tu. Anayechukia achukie lakini atakuwa anafahamu kwamba tunao uwezo wa kuona.
 
Anyway, mwanakijiji mawazo yako ni mazuri sana, ila hebu weka tuu wazi hoja yako hapo ni nini...kwani tunashukuru wana JF wote ni waelewa wasije tuu wakabeba maneno yako yalivyo wakadhani ndiyo maana yako..kwani naona ulisahau kitu kimoja, ungesema pia na maduka, bar, na maeneo yote ya biashara yanayomilikiwa na wachaga yafungwe..ili kweli uone effect yake...Na mie nadhani pia ungesema wachaga wote warudishwe kwao... duh..hii ingekaa vema sana..kwani kungekua na Democratic Republic of Kilimanjaro (DRK). Ambapo nadhani kutokana na uhaba wa ardhi ambao ungetokea Kilimanjaro ingegeuka kua Singapore ...
 
MchunguZi, hebu weka vyanzo vya tuhuma zako, kwani imeonyesha tuu una chuki binafsi..sasa jamani na hizo bar huko mtaani nazo wachaga hao hao wanapendelewa? Maduka yaliyojaa kule Kkoo nayo wachaga wamependelewa kuyafungua?? Cha msingi hapo ni kufanya uchambuzi zaidi ni kwa nini wachaga wamekua wengi kwenye nafasi mbali mbali za maamuzi na kuweza kuona ni kwa nini wengine wameshindwa..then kuanzia hapo unaweza ukatoa ushauri..ila kwa kuzungumza kijuu juu wala hakuna maana ila kunajenga tuu chuki.

Kama alivyosema mwanakijiji...kuna watu ambao wakipewa nafasi wataonyesha ukabila wao waziwazi..na hao ndo wameweza kuonyesha chuki na wachaga hata huku kwenye forum....kaa fikiri kwanza..Kuna kitu kimoja watu hua tunajisahau sana... na hua ni hivi

UNAJIKUTA UNAMLAU MWENZIO KWA KUKUFANYIA UBAYA, HATA KWENYE NORMAL RELATIONSHIPS UNAKUTA MTU ANALALAMIKA KABISA KWA NGUVU ZAKE ZOTE YA KWAMBA MWENZIE NDIYO SIO MWAMINIFU NA AMEMFANYIA UBAYA, ILA SASA HUYO ANAELALAMIKA HAJAKAA AKAANGALIA NI KWA KIASI GANI AMECHANGIA YEYE KUFANYIWA UBAYA HUYO. HUENDA NDIYO ALIKUA CHANZO, KAMA NI MOTO BASI NI YEYE ALINUNUA KIBERITI CHA KUWASHA MOTO WAKATI PETROL IPO TAYARI.

Kwa hiyo ni bora kwa hao wanaofikiri bila kujiangalia mara mbili na kuwalaumu wachaga sasa wakae chini na kujiuliza ni kwa kiasi gani wamechangia hadi wachaga kufikia hapo walipo?? may be wakati wachaga wakienda shule hizo za awali wengine waligoma kupeleka watoto wao shule..sasa unajua tena mwenzio ameshatangulia kuja kumkuta inakua ngumu, badala ya kuangalia utamuangamiza vipi ni bora uangalie utafanyaje ili uweze kumfikia na yeye awe kama ngazi yako ya kufika pale. Hapo ndiyo tutajenga umoja wa kitaifa na kuondoa ukabila. Ila tusipojiangalia wenyewe..tutabaki tuu tunalia kila siku wachaga wanachukua nchi..
 
Ukitaka maendeleo mkimbize aliekuzidi, sio umrudishe nyuma akusubiri. Nyerere alijaribu kuwarudisha nyuma wachaga kwa kuwanyima elima kwa kisingizio cha quotas system lakini haikusaidia. Waliokosa shule waliingia kwenye biashara ndogo ndogo na maisha yakaendelea.

Tuliwafukuza wazungu na wahindi na kuwanyang'anya makampuni yao ati watanzania waendeshe wenyewe sererikali ishikilie njia kuu za uchumi, yakowapi sasa. Miaka 40+ tunawaomba tena warudi kwa masharti watakayo wao. Kama wachagga wamejazana kwenye nafasi za uongozi na biashara bai ujue wana uwezo na hizo kazi kuliko hao wengine. Mtizamo wao na kujituma kwenye kazi ni tofauti. Ukiwatoa ujue nchi inaporomoka. Kuwa na PHd au degree sio kipimo cha kwamba unaweza, ni entry qualification tu hiyo.

Hitler alijaribu kuwateketeza Waisrael lakini mpaka sasa ndio wameshikilia uchumi na utaalamu mkubwa duniani.

Hao wanaofikiri kuwa wamekosa kazi kwa sababu wachagga wamejazana maofisini wanatakiwa wabadili mind set zao na kujifunza kwa hao mnaowaita wachagga.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom