Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
Mwanakijiji, Kubwajinga na wengineo...!
Kweli tokea nimejiunga na jambo forums, leo ni kati ya siku ambayo nimeona post ya ajabu na ya kushangaza mno. Kwanza nimejaribu kujiuliza ni nini madhumuni ya mwanakijiji kuweka post hii tena akiweka kichwa cha habari kinachosema "Viongozi wa Idara ambao ni wachaga waachie ngazi" Je ni nini hasa unataka kukitafuta hapa?
Je vyeo siku hizi vimekua vikigawiwa ka ukabila? kweli kama tumeshafikia mahali pa kuhoji hali hii, nahakika hata wachaga wakiondoka kwenye hivyo vyeo wakapewa watu wengine, kwa mfano WAKARA au WAFIPA nauhakika kuna siku utahoji pia hao WAKARA au WAFIPA nao waachie ngazi, tutaendelea kuhoji hali hio mpaka tutakuta taifa zima hamna anayeweza kutawala kwa sababu ya ukabila.
Kinachonishangaza zaidi, ni kwamba hoja yako imekuja wakati ambao Bw. Chacha wangwe akiwa ametimuliwa uongozi, hii inaashiria kwamba umetumwa uje kuwasilisha propaganda za Wangwe hapa.
Aidha, kama unaona kuna uzito kwenye hoja yako, uliombwa uipeleke kwenye gazeti halafu uichapishe huko ili kila mtu aione, lakini kwa vile unajua wazi kwamba hoja yako ni ya uchochezi wewe mwenyewe umebaini kwamba haiwezi kupokelewa wala kuchapishwa kwenye gazeti, tena hata ikichapishwa inaweza kufanya gazeti hilo kufungiwa kwa kuandika habari za uchochezi.
Kweli mimi sikufahamu kwa undani, lakini nauhakika hii post yako imekupotezea umaarufu na kukushusha sana hadhi yako kwani unaonekana ni mtu unaeyeendeshwa kwa propaganda za uchochezi, Aidha inaonekana wewe ni mtu wa kupenda mafanaikio kwa kutumia njia za mkato kama vile kulalamika na majungu ili uonekane unaonewa ili upendelewe.
Pamoja na hayo yote, hoja yako inaonekana hujaifanyia utafiti, kwani kama unalalamika hivyo, ungekuja na orodha au na data za kudhibitisha kauli yako ya kusema mambo ambayo yamefanywa na hao viongozi wachaga ambayo yanafanya wasiweze kuongoza hizo idara za serikali ukilinganisha na hayo makabila mengine, pia, ungetueleza kwa kina ni kabila gani lingine unalolipendekeza zaidi ya hao wachaga.
Mwisho, naomba nikushauri, hizi hoja za uchochezi ukiziendekeza kuna siku zitatufikisha pabaya, manake nauhakika tukimaliza kuhoji ukabila tuaanza kuhoji udini na jinsia.
Pendekezo langu ni kuomba thread kama hii itolewe mapema kabla hatujaanza kuibua hisia za chuki kati yetu watazania. Pia nakushauri uwe unajishauri mara mbili kabla ya kuweka post hapa jambo forums.
Mhafidhina,
Suala la ukabila kuwa discussed kwa nia ya kuboresha uhusiano wa waTZ sidhani kama ni jambo baya, unless utufahamishe ubaya wake.
Hilo la watu wa idara kutakiwa kuachia ngazi, sina uhakika kama tumeshafikia hapo, lakini busara inaweza kutumika kutatua yale yatakayoonekana kuwakera waTZ.
Kwa maoni yangu, hii thread ilikuwa very sarcastic and to an extent below per in terms of elaborated contents. May be it was intended to downplay the tribalism cries in CHADEMA, but to me, the general point of discussion was valid and very important.