Je, Vyoo vya Shule za Serikali vinajengwa hivi?

Je, Vyoo vya Shule za Serikali vinajengwa hivi?

View attachment 1957636
WATOTO WETU WOTE WATAINGIA FORM 1 MWAKA HUU HATUNA SECOND SELECTION TUMEJENGA MADARASA YA KUTOSHA RAIS AMETOA 842 BILIONI alisikika kiongozi mmoja akinadi kwa bashasha na masham sham sera za Chama
" Tumieni false account, tafuteni mafundi wa hukohuko mtaani wajenge ili pesa irudi mtaani"
Hakika tunauona mzunguko wa fwedha
 
Na nyumba zao wanazojenga hao walimu, maafisa elimu na wakurugenzi zinasimamiwa na nani?
Na wewe kwa mawazo yako wote hao wamejijengea nyumba? Watu wengi ni wapangaji.
Wewe mtaalam wa kwenye mtandao tuambie hapo ungejenga chamber ngapi kwa ajili ya vyoo tisa vilivyo juu hivyo! Na ungeunganisha vipi kwenye septic tank.

Amandla...
 
Hiv watu ni makusudi au
Jf waongeze emojis maana nilikua nataka nioneshe kicheko cha kujigalagaza hapa hamna😂😂😂😂
images - 2021-09-30T012452.079.jpeg
 
Tubalance stori basi kwa kuweka mchoro/ picha ya choo chenye sifa stahiki. Maana wengine hapo tunaona ni sahihi.
 
Ndio shida ya force account. Wote hao hawajui lolote kuhusu miundo mbinu ya maji taka kwenye vyoo na mabafu mengi. Kuwatumbua itakuwa sio haki. Ni kuwaletea mtaalamu atakae waelekeza namna ya kujenga inspection chambers, septic tanks, soak pits au French drains. Sio makosa yao. Na michoro mengi inakosa michoro ya hii miundo mbinu.

Amandla...
Hata Engineers au Wataalamu wa ujenzi hawana/hawapo kwenye hiyo halmashauri!?
 
Hata Engineers au Wataalamu wa ujenzi hawana/hawapo kwenye hiyo halmashauri!?
naona wengi hamuijui Tanzania. Kuna sehemu mwalimu hataki kuishi itakuwa mhandisi? Kuna sehemu hawana hata mfumo wa maji ya bomba kwa hiyo hawatumii vyoo vya ku flush. Hii michoro wamepewa bila kuangalia ujuzi wa mafundi na hali halisi ya eneo husika. Hapo mwalimu Mkuu kaletewa mchoro na pesa ambazo hana uhakika hata kama zitatosha.

Then kuna tatizo/uzembe/mipango mibovu mahali hususani kuhusiana na suala la ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi kwa ujumla.
 
Then kuna tatizo/uzembe/mipango mibovu mahali hususani kuhusiana na suala la ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi kwa ujumla.
Ndio hali halisi. Na kwa sababu wengi wanajiona wataalam wa ujenzi baada ya kujijengea kibanda chao basi wanaidharau taaluma ya ujenzi. Kwanza kabisa Force Account haitakiwi kutumika kwenye miradi kama hii ambapo kosa dogo linaweza kusababisha madhara makubwa kwa wanafunzi na walimu wao. Force account ni kwa ajili ya miradi ya dharura na midogo midogo ya vijijini ambako kupata mkandarasi ni tatizo.

Amandla...
 
Mnachanganya. Kujenga nyumba binafsi ambayo ina choo kimoja au viwili ni tofauti sana na kujenga yenye vyoo tisa vilivyojipanga. Sio sehemu zote Tanzania zenye uzoefu wa manholes, septic tank na soak pit. Hata wale ambao wana vyoo vinavyotumia maji wengi hawajui namna vilivyounganishwa kwenye septic tank maana mabomba yanakuwa yamefikiwa. Na sio wote wanaojenga nyumba zao. Wengi tuu ni wapangaji.
Huyo mtu atakayejenga hivi kwa makusudi ili apige fedha atakuwa punguani kweli. Hapa ni ignorance tu na sio ufisadi.

Amandla...
Na Wala hakuna ignorance, ila sis wachangiaj tunaignorance kwenye Hili.,,hatujui Sababu lakn tunalaumu.. kiufupi vyoo vingi katika shule nyingi za umma ambazo hazina maji au uhakika wa kupat maji ya kutoshaa ndo vinajengw hivi.. huwez ukawwka chemba wakati maji Hamna utasababisha Maafa zaidi... Chukuen hilo
 
Ndio shida ya force account. Wote hao hawajui lolote kuhusu miundo mbinu ya maji taka kwenye vyoo na mabafu mengi. Kuwatumbua itakuwa sio haki. Ni kuwaletea mtaalamu atakae waelekeza namna ya kujenga inspection chambers, septic tanks, soak pits au French drains. Sio makosa yao. Na michoro mengi inakosa michoro ya hii miundo mbinu.

Amandla...
Hiyo design ni practicle oriented.
Wame boresha vyoo vya kutumbukiza kulingana na mazingira yao.
Huu ni ubunifu tu.
Hizo chemba hazifanyikazi kwenye mazingira yao.
 
Na Wala hakuna ignorance, ila sis wachangiaj tunaignorance kwenye Hili.,,hatujui Sababu lakn tunalaumu.. kiufupi vyoo vingi katika shule nyingi za umma ambazo hazina maji au uhakika wa kupat maji ya kutoshaa ndo vinajengw hivi.. huwez ukawwka chemba wakati maji Hamna utasababisha Maafa zaidi... Chukuen hilo
Huo muinamo wa hizo bomba unadhani zinaweza kutiririsha uchafu mzito! Haziwezi.
 
View attachment 1957636
WATOTO WETU WOTE WATAINGIA FORM 1 MWAKA HUU HATUNA SECOND SELECTION TUMEJENGA MADARASA YA KUTOSHA RAIS AMETOA 842 BILIONI alisikika kiongozi mmoja akinadi kwa bashasha na masham sham sera za Chama
Ndio mafanikio ya sera za Force Account.
Serikali inamuamini fundi Maiko, makandarasi ni wezi kabisa.
 
Back
Top Bottom