Unajuaje watakuwa wa ukanda huo? How sure are you? Hapo juu nimekuuliza kwa nini kila jamii Ina sense of an all powerful and eternal deity, hukunijibu. Nikuulize pia, kwa nini kila jamii inaona kuua ni vibaya, kuchukua mke/mume wa mwenzio ni vibaya, kutowaheshimu wazazi ni vibaya, kuiba ni vibaya, kuseng'enya ni vibaya...kwa nini kila jamii inaomboleza msiba na kuzika wafu, kuoa na kuolewa (kuzaana) na kuleta watoto, kwa nini kila jamii inawalinda hasa wanawake, watoto, wazee na watu wenye ulemavu, kwa nini katika kila jamii watu wanakuwa curious kujua jambo geni, etc? Unadhani hayo yote yalianzishwa na jamii gani na jamii gani ziliiga kwa wengine? Haya, hata ukiiangalia wanyama - nao wanazaliana, wanatoa ulinzi kwa watoto wao, wanaomboleza mwenzao akifa, etc. Wameiga kwa wanyama gani? Kuna baadhi ya mimea ukiigusa inasinyaa: Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro? Imeiga wapi?