Je, wabunge 19 wa CHADEMA walijiteua? Je, CC ya CHADEMA ni Kangaroo Court? Je, Baraza Kuu litabariki ukangaroo ule?

Kwamba list ya Viti maalum alikua nayo magufuli? Duuuh
 
Alipofukuzwa Zitto Kabwe uliandika hivi. Leo hao hao walioamua kwa ZZK una wa question.
 
Halima Mdee bado mdogo sana,ni mwanasiasa mzuri ila ameteleza tuu, in general ana agenda nzuri za kutetea wananchi na kufichua mafisadi kitu ambacho ni muhimu, i hope atarudi na atakuwa amejifunza, na ukizingatia umafia na changamoto ya siasa za awamu iliyopita ni bora kumsamehe tuu, i hope CDM wana utaratibu wa kumrudishia mtu uwanachama baada ya kufukuzwa
 
Akiomba kurudishiwa lakini
 
Mayala maana yake njaaa
 
Kila mtu ana haki ya maoni, kwangu, kusimama na misingi ya chama iwe CCM, CDM etc ni kitu muhimu sana kuliko personality. Nilikataa wakati wa Maalim RIP na kila chama.
,[emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
mwengeso kwa kila changamoto CDM inayopitia inazidi kujiimaarisha na kuwa bora zaidi na kuimarika zaidi
Maoni ya Pasco yatabaki kuwa maonj kwakuwa naamini viongozi wa CDM kwa hakika wanajua wanachofanya kuliko mtu mwingine yeyote nje yake

Kuna wale vijana tunaowaita LUMUMBA BUKU7 ambao siku hizi wamepotea na kupoteana kabisa.. Hawa tulikuwa tunajua udhaifu wa hoja zao hasa linapokuja lolote linaloihusu CDM.. Lakini anapotokea mtu wa kaliba ya pasco kufanya hivyo inanitatiza kidogo
 
Mzee unayumba sana sijui kwanini, hivi hata kwa mtoto mdogo wa chekechea anaweza kuongea vitu vya maana kuliko unachofanya hapa Pasco

Sent from my M2103K19G using JamiiForums mobile app
 
Kuna sababu gani kutambulisha kazi yako katika jambo hili? Lakini kwa maandishi yako unaonekana kama umeshavuta mgao tayari.

Labda niachane na hayo, niseme hivi:

1: Kama shida yako kutaka kujua mbona ndani yake umekuwa na majibu na mitazamo ambayo ungependa ifanyiwe kazi? Hii inadhirihisha kutokana na lugha ya maudhi kuwa baraza kuu ni nyumbu. You really slagged off them in a way that wont be acceptable.

2: Kwa muda mrefu Zitto hakuwahi kuwa mpinzani, sijui kama unanielewa kwa kusema hivi.

3: Tumekuelewa lakini hayakuhusu!
 
Mkuu Mshana Jr nilitegemea hoja badala ya "personal attack" ya Paskali.

Hakuna ubishi kuwa hao wanaoitwa COVID-19 walisukumwa na uchu wa madaraka kujiteua. Pamoja na kuvuliwa uanachama na Kamati Kuu ya Chama hawakuona busara kuondokana na Ubunge waliojichagua.

Pia hakuna ubishi Kamati Kuu ya Chama haikufuata Katiba yake (Ibara ya 5.4, Toleo la 2016) kuwavua uanachama. Isitoshe Baraza Kuu halikuitishwa, katika muda mwafaka, kubariki uamuzi wa Kamati Kuu kwa suala nyeti kama hilo wakati CHADEMA ni Chama Kikuu cha upinzani chenye nia ya kushika madaraka.
 
nimeskia kumbe mkewe wa kwanza aalimuacha akaoa mwengine angekuwa mvumilivu angebembeleza maisha yende lkn uvumilivu umemshinda sasa leo anashauri chdm iwasmehe mbona yy hakusamehe mkewe wa kwanza
Mkuu MWALLA , usiamini kila unachosikia!. Sisi Wasukuma tunajuaga kuoa tuu, hatujui kuacha!. Tatizo letu ni huwezi kuwa peke yako, lazima msaidiane na wenzio!. Naomba tuheshimu the right to privacy za watu, tujadili mada iliyo mezani.
P
 
Hivyo hili ni bandiko la swali "Je Wabunge 19 wa Chadema Walijiteau?. Je CC-ya Chadema ni Kangaroo Court?. Je Baraza Kuu Litabariki Ukangaroo Ule?. Likibariki, Karma Itawatafuna!"
Nawatakia wana Chadema, kikao chema cha Baraza Kuu.

Paskali
tena ajabu zaidi ipo kule bungeni, ambapo kiongozi wa muhimili wa kutunga sheria anapoamua kuwakumbatia wanawake 19 wasiowakilisha chama chochote kinyume cha katiba, kwa manufaa ya chama na serikali yake.
Mkuu denooJ, mimi kama mwanahabari ni muelimishaji umma, nimeamua kuanzia mwaka huu, nianze kujitahidi kuwasaidia kuwaelimisha wana jf, na kutumia elimu yangu kuelimisha umma na kutumia uwezo wangu kusaidia taifa langu.

  1. Nakuomba sana nikuelimisha kuwa objective kwenye hili, wabunge wale wamepewa uteuzi na NEC, hivyo Bunge lina kosa gani?.
  2. Kwanini hamjishughulishi kabisa kujua barua ya uteuzi ilitoka wapi?, NEC sio vichaa!, Bunge halina kosa kabisa kwenye hili!.
  3. The right thing ni Chadema ilipaswa ifanye a due diligence, ikijiridhisha kuna jinai ya forgery, that is a police case!.
  4. Hata kama ni kweli wamefoji, then Chadema ilipaswa kufuata katiba yake kuwatimua!.
  5. Nashauri, kwa vile hii kesi iko mahakamani, nashauri tusubiri maamuzi ya mahakama ndipo niendelee kukuelimisha na sio maamuzi ya zile kangaroo courts 2!.
p
 
- Sheria inasema ili mtu awe mbunge, lazima awe anawakilisha chama cha siasa, hao wanawake 19 wamefukuzwa na chama chao, sasa hebu tuambie, wanawakilisha chama gani kule bungeni? kama hukijui hicho chama, basi hilo ndio kosa la bunge.

- Barua ya uteuzi ndio issue ya forgery inapoanzia, tatizo kule mahakamani unapopalalamikia kila siku, kumetawaliwa na watu wasioijua/kuijua sheria, lakini wanaofanya kazi kwa interest zao kama ulivyo wewe.

Sasa kama hiyo kesi ya forgery ikienda mahakamani, unadhani haki itakuwepo toka kwa wale majaji waliopewa ulaji na mwenyekiti wa CCM? [ hapa bahati nzuri nawe unaonesha mashaka kwenye uzi wako mwingine kuwa mahakama zetu hazipo huru]

Zaidi, kulazimisha kujua barua ya uteuzi ilipotoka, ni ujanja wako tu wa siku zote, najua unafanya hivyo pia kwa interest zako ili ku divert attention kwa manufaa yenu, au kama wewe una ushahidi wapi hiyo barua ilipotoka, basi tuwekee hapa tuione...
 
Hatimaye Chadema wamejitambua, keshokutwa Jumatano Siku ya Wanawake Duniani , Chadema itatangaza kuwasamehe mashujaa hawa hivyo sasa karma haitawashukia tena Chadema!, sasa ni baraka kwa kwenda mbele.
Update
Hatimaye Chadema wameacha kushupaza shingo na wamekubali matokeo!, kwa kuufuata ushauri wa bandiko hili CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Nimepokea taarifa, hii kutokea twitwani Kisha nikasoma na bandiko hili humu JF Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Chadema wameufuata ushauri wa bandiko hili, waneacha ujinga wa kujifanya hawayatambui matokeo ya uchaguzi wa 2020!, sasa wameacha kushupaza shingo, wameyatambua matokeo kimya kimya!, wamewasamehe mashujaa hawa kimya kimya msamaha ambao utatangazwa rasmi siku ya Jumatano tarehe 8 Machi na Mwenyekiti wa Chadema, mbele ya Rais Samia!.

Iliwa kusemwa kuwa hakuna mkate mgumu wowote mbele ya chai!, tayari Chadema imeisha anza kupokea ruzuku hivyo sasa ita survive!. Na ile kesi ya kina Halima Mdee na wale 19 iliyopo mahakamani itafutwa!.

Hongera sana Chadema, for doing the right thing!, mtabarikiwa, viongozi wenu watabarikiwa, chama chenu kitabarikiwa na Tanzania Itabarikiwa!.
Mungu ibariki Chadema
Mungu ibariki CCM kwa kukubali reconciliation
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 
Nakukubari comrade
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…