Je, wabunge 19 wa CHADEMA walijiteua? Je, CC ya CHADEMA ni Kangaroo Court? Je, Baraza Kuu litabariki ukangaroo ule?

Tatizo ni serikali kulikalia shauri mahakamani kwa kuhofia mahakama ikiwaondoa basi kamati ya Bunge ya Fedha itakuwa imevunja mkataba na wafadhili Chadema haikuwahi kufikiria kuiondoa kesi mahakamani, pia kongamano la wanawake liko wazi kwa wanawake wote wa Tanzania bila kujali vyama, kama ni mfuatiliaji utakuwa unalijua hilo.
 
Leo hukumu imetoka
Nimeisoma hukumu, 1. Mahakama zetu zinarudia makosa yale yale ya ukosefu wa kutenda haki kwa sababu ya legal technicalities, kuwa Mahakama haiwezi kutoa uamuzi wa kitu ambacho hakikuombwa!.
2. Wabunge hawa 19 wa Chadema, walivuliwa uanachama wao kinyume cha katiba ya JMT na kinyume cha haki kwa kutokusikilizwa, kinyume cha katiba ya Chadema kwa kukiuka sheria, taratibu na kanuni!.
3. Kikao cha CCM ya Chadema, kilichowatimua kilikaa kama a kangaroo court na kutoa maamuzi ya kikangaroo!.
4. Katiba ya Chadema inasema mwanachama kabla hajafutwa uanachama, kwanza atatumiwa hati ya mashitaka kwa maandishi by despatch, kisha atapewa siku 14 za kujibu mashitaka. Chadema hawakuandaa hati zozote za mashitaka!. Hili Mahakama ilipaswa ilione!.
5. Baada ya watuhumiwa kupewa hati ya mashitaka, ndipo kikao cha CC kinaitishwa kama mamlaka ya nidhamu, kusoma majibu ya mashitaka, na ndipo kinawaita washikiwa na kuwasikiliza. Hili halikufanyika!.
6. Baada ya wabunge 19 wa Chadema kuapishwa, hapa Chadema waliposwa kufanya kitu kinachoitwa a due process ya nidhamu na sio zile Zimamoto za kikangaroo!. There was no emergency of whatsoever!. Mahakama ilipaswa ilione hili!.
7. Uthibitisho wa hakukuwa na any emergency ya kuitisha CC, ni the time taken, kuitisha kikao cha Baraza Kuu!.
8. Baada ya kuitishwa kikao cha Baraza Kuu, kitu cha kwanza kwa Baraza Kuu Chadema kuangalia ni uhalali wa kikao cha CC, pili jee katiba, sheria, taratibu na kanuni za mamlaka ya nidhamu ya Chadema zilifuatwa?.
8. CC ya Chadema ni mamlaka halali ya nidhamu ya wabunge wa Chadema, lakini CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Bawacha!, Mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu!, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtimua Halima Mdee?!. Kikao cha Baraza Kuu kilipaswa hili kukuona!.
9. Japo kikao cha Baraza Kuu Chadema kiliitishwa kihalali kama mamlaka ya rufaa ya wabunge wa Chadema, lakini kitendo cha kikao hicho kubariki uamuzi wa CC kuwatimua bila kufanya mapitio yoyote, ni uthibitisho wa Chadema bado ni chama kichanga, mfano kingechukua nchi ile 2015!, it would have been disastrous!.
10. Kitendo cha Baraza Kuu kubariki maamuzi ya kikangaroo ya CC ya Chadema, kilifanya niyaite maamuzi yale pia ni ya kikangaroo, na kitendo cha Mahakama Kuu kuyabari maamuzi ya kikangaroo, Mahakama Kuu yetu nayo has joined the team!.
A Way Forward
1. Kwa vile Chadema imefanikiwa kuwatimua hao 19 sasa Chadema isikate tena rufaa, kupinga uamuzi huu, bali iitishe kikao cha Baraza Kuu , ASAP, kifanye a due process, hili la wabunge 19 liishe, wabunge hao 19 wavuliwe ubunge wao, Chadema wapeleke majina 19 mengine, wateuliwe waapishwe, tuwe na Bunge la vyama vingi!.

2. Chadema wakifanya tuu dillydalling kukaa rufaa, inakula kwao!. By the time rufaa inasikilizwa, ndipo kifuate kikao cha Baraza Kuu, I'm afraid the time left before the next election is too little too late, ikibaki muda wa chini ya miezi 12 kabla ya muda wa uhai wa Bunge kuisha, hakuna uchaguzi wowote wala uteuzi wowote wa wabunge wapya!.
3. Tena nashauri kikao hicho cha Baraza Kuu, pia sasa ndio kimtimue Halima Mdee, kikifuatiwa Mkutano Mkuu kuthibitisha. Hapa najua changamoto ni fedha!, kule kwenye kile chungu, zilikopatikana zile fedha za kugharimia Baraza Kuu lile, kile chungu bado kipo, kitagharimia vikao vyote viwili, na Chadema inaweza kupiga ndege wawili kwa jiwe moja kwa mtu kupumzishwa kwa heshima na dereva mpya kupatikana!.
Paskali.
 
Hayakuhusu
 
"Chadema inaweza kupiga ndege wawili kwa jiwe moja kwa mtu kupumzishwa kwa heshima na dereva mpya kupatikana!".
Paskali.
Paskali kwa uandishi huu wewe si mwandishi wa habari, wewe ni collaborator(enzi hizo mrusi au mchina akikuambia hivyo basi umekwisha), unaandika kisha unampa msomaji wako uamuzi wako aukubali atake asitake! Hata hivyo uandishi wako dhidi ya Chadema ni hasi. Nirudi kwenye hoja yako (MBOWE), ni wazi mhe. wakili haumpendi kwa sababu zako ambazo pamoja sizijui lakini naziheshimu kwa kua ni haki yako. Mbowe si kikwazo kwako tu ni pamoja na kwa CCM kwani imejaribu kila njia lakini pia hanunuliki na haufyati mkia! Chadema itauawa vipi mtu huyu akingali yupo? Jiulize, Chadema ikifa wewe binafsi utafaidikaje? Raha yako ni kuona wafuasi wake wanakosa walichokipenda! Huo ni ukatiri.
 
Mkuu pamoja na makala yako nzuri , nipo na jambo langu kwako ikikupendeza nipe ufafanuzi

Inasemekana umekua moja ya mtumishi katika balozi zetu nje ya nchi ,je ni kweli au sio kweli mkuu
 
Mkuu pamoja na makala yako nzuri , nipo na jambo langu kwako ikikupendeza nipe ufafanuzi

Inasemekana umekua moja ya mtumishi katika balozi zetu nje ya nchi ,je ni kweli au sio kweli mkuu
Si kweli, sijawahi kuwa mtumishi kwenye balozi yetu yoyote, ila kupitia fani yangu ya uandishi wa habari, nimezifanyia kazi za kihabari, Balozi zetu nyingi huko nje kwa kuzitembelea na kuwafanyia mahojiano mabalozi wetu, kazi ya mwisho ni Nchini Burundi hapa juzi kati!
View: https://youtu.be/66hraWlv_Bw?si=q8Svwk0j2E37Fwmp
Ila niliajiriwa na taasisi ya FCO ya Uingereza kuwa mshauri wa Siasa wa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania.
P
 
Fani ya uandishi wa habari wa kuegemea upande mmoja ni fani ya hovyo kabisa na hakuna chuo kinachojitambua kinafundisha jambo la hovyo hivyo, mwandishi ambaye anakwenda kwenye tukio huku tayari kesha andika kwa kusikia hajaona na anahitimisha habari ya tukio! Haufai ndugu, hata uwakili haukufai kwa sababu watu tayari wanajua upande wako hivyo utawahudumia watu wa upande wako tu huku wengine ukiwafungisha kwa makusudi.
 
😃😀
 
Kwenye uandishi kuna sub sectors nyingi, kazi ya media ni zaidi ya kuhabarisha,hizo sifa ulizoweka hapo ni sifa za reporter, mimi sio reporter media ni mhimili wa nne hivyo mimi nafanya kazi ya uhimili,trends setting,critical opinions na editorials hivyo tunaruhusiwa kuwa na upande。Wakati wa uchaguzi, media tunawajibu wa kuuelimisha umma kufanya informed decision。 Mfano,kwenye huu uchaguzi wa mwenyekiti wa Chadema,kuna mgombea mmoja ni nazi na kuna koroma,ni jukumu la media kuonyesha nazi ni ipi koroma ni lipi Japo Lowassa Alikuwa a Liability CCM, Akawa Asset Chadema. Lissu is a Very Bad Liability, but is The Only Asset Chadema Has Kuwangiza Ikulu!. Je... ? nimebahatika kupata good exposure kwenye media za wenzetu wakati wa uchaguzi hivyo。sii mara moja wala mbili nimeshauri
hata uwakili haukufai kwa sababu watu tayari wanajua upande wako hivyo utawahudumia watu wa upande wako tu huku wengine ukiwafungisha kwa makusudi.
Kuna wengi wanadhani kazi ya wakili ni kuwatetea tuu watu mahakamani,Mimi sio wakili wa kesi za mahakamani litigations,mimi ni wakili wa legal opinion huku nikiwaelimisha watu elimu ya katiba,sheria na haki,ambacho ni kitu kikubwa,kizuri na chenye manufaa kuliko kutetea kesi mahakamani Kipindi cha TV, Kutoa Elimu ya Katiba, Sheria na Haki, Kuanza Jumapili Hii Kupita Channel Ten
 
Wanabodi.
  1. Hivyo hili ni bandiko la swali "Je Wabunge 19 wa Chadema Walijiteau?. Je CC-ya Chadema ni Kangaroo Court?. Je Baraza Kuu Litabariki Ukangaroo Ule?. Likibariki, Karma Itawatafuna!"
Paskali
Huu ni mwaka wa uchaguzi,Chadema wasupokuwa makuni,baadhi ya madudu yao yatakuja kuwagharimu,moja ya madudu hayo ni hili dudu la wabunge 19。

CC ya Chadema iliwatimua kwa kuteuliwa wabunge wa viti maalum,nikailiza humu je wamejiteua?, sikiliza jibu la Mhe。Ester Bulaya
Mimi mwenzenu jamani huyu mdada,sio tuu namkubali kichizi,bali kiukweli, 。。。,, naomba nisimalizie!,, ila nimeanza kumzimikia long time toka yuko CCM Mbunge wa CCM, Esta Bulaya, ni mbunge pekee aliyesaini petition ya Zitto ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu! Chadema ikomppteza itakuwa imepoteza kitu kikubwa,na wasipoamua mapema kuwasamehe,hawa watatu,Halima Mdee,Ester Bulaya na Ester Matiko,watagombewa kama mpira wa kona na majimbo yao,wakosimama kupitia chama chochote,wana tusua!。
P
 
mgogoro mkubwa sana unakuja kuibuka hapa hao wakina mama 19 hawakuenda bungeni kwa kujiteua hapo mwenyekiti na katibu mkuu wanahusika na hawakufoji kama walifoji wangeqwakomalia kuwashitaki mbona hawakuwashitaki?chadema ni kundi la kihuni tu bado hatuna chama cha upinzani makini
 
Pumbavu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…