Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Nawasalimu kwa jina la JF.
Angalizo la uchangiaji, hili ni moja ya mabandiko yangu ya kuwaanda Watanzani kisaikolojia kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu, nakushauri, ukiusoma uzi huu, ukijiona kama huuelewi elewi, jipitie zako tuu kwa amani, usiparamie kuchangia, ila kwa vile jf ni ukumbi wa wote, simple, mind, ordinary mind na great mind, kwa simple mind, wataliona bandiko hili kama bandiko la kichawa, kwa great mind watajikita na the motive behind!. Hivyo kwa wale mtakao niona nimekuwa chawa, niko ok, nioneni chawa, ila ma GT, tunaelewana!, karibuni.
Kila mtu anayesema chochote, au kuandika chochote, anakuwa na kitu kinachotwa drive, msukumo wa kusema ua kuandika, msukumo huo unaitwa causative agent, inaweza kuwa umeulizwa swali hivyo unasema kwa kujibu, au mtu ameandika kitu ukaguswa ukajibu, au kuchangia, ila katika hicho ulichokisema au ulichoandika, unakuwa na kitu kinachoitwa the motive behind, yaani unayasema hayo au unaandika hayo ili iweje?.
Huu ni mwaka wa uchaguzi, mwaka huu, mimi na PPR yangu tumeamua kujikita katika utoaji elimu kwa umma kuhusu siasa, uchumi na jamii, kuwaelimisha Watanzania, elimu ya demokrasia, katiba, sheria, haki na wajibu, ili wakati wa kufanya maamuzi, Watanzania wafanye informed decisions.
Naomba kukiri, nimehamasika kulizungumzia hili jambo, la mtu ambaye ni mwanamke, ni mama , na anaitwa mama, kumbe, sii mama tuu, ni mamababa!, kwa kuhamasishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, wakati akiitolea ufafanuzi, kauli yake ya "no reforms, no election", na kusema huo ndio msimamo wa Chadema, na kuufafanua kwa wale wana Chadema wanaotaka kugombea uongozi, kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, wajiulize "unagombea uongozi, ili iweje?", jibu la hilo swali la ili iweje, ndio the motives behind. Bandiko hili pia lina the motives behind, ila hiyo motives behind, naomba nisiiweke kwenye bandiko hili, tutakuja kukumbushana huko mbele ya safari, muda muafaka ukiwadia!.
JF ilianzishwa mwaka 2006, mwakani tunasherehekea miaka 20 ya JF, kuna sisi baadhi yenu tulijiunga na jf tukiwa vijana, tumeoa tukiwa jf, sasa tunazeeka tukiwa jf, mfano mwana jf yoyote under 20, ajijue tangu anazaliwa watu tuko humu jf, lazima wajifunze kuwa na heshima.
Kufuatia long experience ya uzoefu wa muda mrefu, mara moja moja, nitakuwa napandisha makala elimishi za mambo yoyote ya busara, kwa jina la Busara za Mzee P.
na kwa vile mimi ni story teller, mabandiko haya yatakuwa ni marefu na story story kibao!.
Busara ya leo ni kuhusu majukumu ya kifamilia kwa mujibu wa dini kuu mbili, Ukristo na Uislamu, na mila nyingi za Kiafrika, zinazo fuata mfumo dume, patriarch, zimelelewa kwa malezi ya ubaguzi wa mfumo dume kuwa Baba ndio kichwa cha nyumba na mama ni kiwiliili. Kiwiliwili bila kichwa, ni hakuna kitu, lakini kichwa bila kiwiliwili, kinaweza kuchukua kiwiwili kingine chochote, maisha yakaendelea, ndio maana dini na mila za Kiafrika, zimeruhusu mwanamume kuwa na mke zaidi ya mmoja, lakini kwa mwanamke ni mume mmoja tuu, ukiondoa uongo wa mke mmoja kwa Wakristu, na mila za baadhi ya makabila ya matriarch, ya makabila machache ya Afrika, Asia na Latin America, mke ndie anaoa hivyo kuwa huru kuoa zaidi ya mume mmoja!
Ubaguzi huu huanzia kwenye ngazi ya familia na malezi kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu, dhalili, hivyo mtoto wa kike analelewa kiulaini laini na mtoto wa kiume analelewa kiugumu ugumu. Mtoto wa kike anafunzwa kuegemea na kumtegemea mwanaume, ni mtu wa kubembelezwa kuletewa na kupokea, na mtoto wa kiume anafunzwa kugangamala, ni mtu wa kutafuta, kutoa na kukomaa.
Hali hii huanzia tangu katika ujenzi wa familia, mtoto wa kike, anafundishwa kusubiri kuchaguliwa, kutongozwa, kuhongwa, kupendwa, kuchumbiwa, na kulipiwa mahari, ndipo apende, na ndani ya nyumba, mwanaume ndie kichwa cha nyumba, ndiye mtafutaji, anayepambana kutafuta, mke akiwa golikipa, akisubiri kuletewa.
Hata process ya uumbaji, procreation, kwa binadamu na viumbe wote, ukiondoa nyuki, ni mwanaume hukaa juu, mwanamke chini, ni mwanaume ndie anatoa mbegu, mwanamke anapokea, na kubeba, na kwa hapa Tanzania Bara, ni kosa la mwanaume kumpa mwanafunzi ujauzito, lakini kwa Zanzibar kosa ni la mwanamke kupokea ujauzito, kwasababu ni mwanamke ndie anayeruhusu!.
Na hata kukitokea msiba wa familia, akifa mama, japo baba huitwa mgane, lakini hakuna ajabu kwa baba kuoa tena, ndio maana ni aghlabu sana kusikia matatizo ya wagane, akifa mama, familia haitetereki, kwasababu baba ni the breadwinner, lakini akifa baba, mke huitwa mjane na familia nyingi hutetereka, kidini na kiafrika mjane hutakiwa kurithiwa, na familia kutegemezwa.
Lakini japo baba ndie kichwa cha nyumba, si wengi wanajua kuwa kunapotokea mazingira kama kufiwa na baba ambaye ni kichwa cha nyumba, mama akiamua kusimama na nyumba yake, hahitaji kurithiwa, huyu mama anakuwa amegeuka kichwa!, hivyo anageuka baba, hivyo kuna wanawake wengi tuu, japo ni wanawake na wanaitwa mama, lakini ni actual fact, wanawake hawa ni Baba!. Nyumba ikifiwa na mama, baba hawezi kugeuka mama, bali anatafuta mama mwingine, maisha yanaendekea, lakini nyumba ikifiwa na baba, mama anaweza kukomaa na kugeuka baba na maisha yakaendelea!.
Huu mfumo dume tumeurithi kwa wakoloni na kwenye mila zetu, kuna majina ya posts fulani fulani, ni majina ya kiume, mfano gavana ni post ya kiume, mwanamke anaitwa governess. Amiri Jeshi ni posti ya kiume, mwanamke ni Amirati. Chairman ni post ya kiume, mwanamke ni Chairwoman, hata president ni post ya kiume. Mwanamke anaposhika nafasi ya mwenyekiti wa chama, yaani Chairmanship, japo ni mwanamke, anageuka mwanaume na ataitwa Chairman , na sio chairwoman, hata mwanamke anapokuwa Amiri jeshi mkuu, anageuka mwanaume, anaendelea kuitwa amiri jeshi na sio amirati!, hivyo hata mwanamke akiwa ni president wa nchi, japo ni mwanamlke na wengi wanamuita mama, lakini in actual fact huyu ni baba!.
Kila awamu, rais wa nchi ndie baba wa taifa husika, na mke wake japo huitwa first lady, lakini sio mama wa taifa, bali mke wa rais, vivyo hivyo rais wa nchi anapokuwa ni mwanamke, rais huyo ni bado ni baba wa taifa hilo ambaye ni mama, na mume wake sio baba wa taifa, ni mume wa rais.
Leo nimeone niwafundishe hili somo, kuwa japo Rais Samia ni Mwanamke, na wengi humuita Mama Samia, ila ki nchi, kitaifa, ki madaraka na ki mamlaka na ki utawala, Rais Samia ndie kichwa cha nchi yetu, ndie Baba wa Tanzania ya leo kwa sasa, yeye ndiye kichwa cha nyumba yetu, ni Baba!.
Naomba kumalizia kwa ahadi nilowaomba kwa leo, mjifunze kuweka akiba ya mabandiko kama unavyoweka akiba ya fedha, mliweke akiba bandiko hili la Samia ni Baba, siku ya siku ikifika, nitalirejelea kwanini nimesema Rais Samia, japo ni mwanamke, ni mama, lakini sii mama tuu, ni ... ni MamaBaba!.
Mzee Pasco.