Ralphryder
JF-Expert Member
- Nov 16, 2011
- 5,599
- 1,801
Kobaz hawataki hata kushauriwa wala kutumia akili za kdg kufikiri nje ya mavutabu yaliyoletwa kwenye majahazi, ukiwaambia wanakwita kafir wakati wao kwa 100% ndio hasa hasa wenyewe!!Chizi kivipi mkuu! Kutaka kujua Aya za Quran tukufu ya Allah na mtume wake Muhammad ni uchizi!? Acha kutukana Imani za watu mzeebaba
Your grasp of things seems inaccurate and inconsistent with the name you claim to bear Mr. Clever.Ungetuliza akili na kutaka kuelewa ungeelewa wala usingeona kama nachekesha.
Jamaa hapo juu niliyemjibu alisema maana ya hiyo aya ni kumtakia Rehema mtume. Ndo nikuhoji, Allah anamtakia Rehema mtume kutoka kwa nani? Yeye ndo mwenye hizo Rehema Kisha anamtakia mtume Rehema inaingia akilini hiyo? Yaani wewe una pesa kisha unamuombea mtu pesa kutoka kwako, sio kichekesho hicho?
Expert wangu relux sawa, unazungumzia tu kunyenyekea lakini huzungumzii kufuata maamrisho yake na kuacha makatazo yakeErtugrul Bey nakusihii kasome Tena dini yako ,ni wazi huijui na kama unaijua basi umefundishwa uongo mwingi
Unapokuja kujadili na Mimi ,kwanza jipange ,
Hii hoja kwamba mitume wote walikuwa Waislamu kwa sababu walijinyenyekeza kwa Mungu mmoja ni dhaifu na ya kulazimisha, ni hoja ambayo hata kina Mazinge walishaiacha ,nimeshangaa wewe Bado umekaririshwa .
Hakuna ushahidi wowote wa kihistoria wala wa maandiko unaothibitisha kuwa dini ya Uislamu, kwa jina, mfumo na mafundisho yake (kama Shahada, Swala mara tano, Saumu Ramadhani, Hija, n.k), ilikuwepo kabla ya Muhammad katika karne ya 7 A.D. Wala hakuna maandiko ya Biblia yanayomwita Ibrahim, Musa au Yesu kuwa Waislamu. Hawa wote walikuwa Wayahudi, waliomwabudu Mungu kwa mujibu wa agano la kale, na Yesu akafundisha Agano Jipya.
Kujinyenyekeza kwa Mungu mmoja si kigezo cha kumfanya mtu kuwa Muislamu. Kama ni hivyo, basi hata Wakristo na Wayahudi wote ni Waislamu, jambo ambalo halikubaliki kiimani wala kihistoria. Yesu hakuwahi kufundisha Shahada ya Kiislamu, hakuswali kwa rakaa tano, wala hakufunga Ramadhani.
Hata Qur’an inasema wazi katika Surah Al-Ma’idah 5:3 kwamba
“Leo nimekukamilishieni dini yenu...”,
ikimaanisha kwamba Uislamu haukuwa umekamilika kabla ya Muhammad.
Kwa hiyo, kusema mitume wote walikuwa Waislamu ni tafsiri ya kulazimisha isiyo na msingi wa kweli. Ni sawa na kumpachika mtu uraia wa nchi ambayo haikuwepo wakati wake.
Uelewa wako ni mdogo! Hili suala tangu awali nilishakujibu.Ok nakuelewa,
Kwani ni wapi mi nimetoa tafsiri yangu binafsi? Mi nimeleta mada kwa kusoma Quran yenu ambayo ipo kwa kiswahili. Sijaongeza chochote wala kupunguza,
Uelewa wako ni mdogo zaidi.Kama ni watu tu ambao walikuta Quran tayari ipo na wakaamua tu kutafsiri kwa maoni yao, why tuwaamini bila kuhoji? Tafsiri ilibidi itolewe na mtume mwenyewe ila kama wanatoa watu ambao hata hawakuwa na ukaribu na mtume ni wazi kwamba wametafsiri kwa matakwa YaoYao
Ok twende polepole ndugu,Your grasp of things seems inaccurate and inconsistent with the name you claim to bear Mr. Clever.
Kwani nini maana ya rehma kwa muktadha wa hiyo aya? Maana yake ni Allah kumsifu mtume wake mbele ya malaika Wake.
Kusanya ufahamu wako ili uelewe vyema kwa kila kinachoandikwa. Kwa sababu si kila kinachoandikwa kinakuhusu, vingine vina wenyewe. Ikiwa kama mahali hujapaelewa ni vyema kuuliza kuliko kukosoa kwa kutaka kuonekana mjuaji kumbe unadhihirisha una ufahamu mzito kwa namna gani!
Rehema ni nini kwa muktadha upi?Ok twende polepole ndugu,
Rehema ni nini?
Mzeebaba unaweza kujadili kwa amani au huwezi?Uelewa wako ni mdogo! Hili suala tangu awali nilishakujibu.
Wewe hujaleta tafsiri kwa lugha ya kiswahili! Wewe umeleta tarjuma.
Tarjuma ni kuhamisha Qur'an kutoka kwenye lugja ya kiarabu kupeleka kwenye lugha isiyo ya kiarabu.
Mfano:
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
Tarjuma ya Kiswahili:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma mwenye kurehemu.
Tafsiri yake ni nini? Maana ya hiyo aya ni nini?
Tafsiri yake ni, kwa jina la Mwenyezi Mungu mwenye kuneemesha wema na waovu duniani na mwenye kuneemesha wema pekee siku ya malipo.
Wewe hukuleta tafsiri, wewe ulileta tarjuma.
Uelewa wako ni mdogo zaidi.
Wapi nilipoandika kuwa wanatafsiri Qur'an wao wenyewe?
Nimekuambia elimu ya kiislamu ina sanad, ulimwengu mzima ndiyo ipo hivyo hivyo!
Na mlolongo wa mapokeo ya dini ynapokelewa kama yalivyotoka kwa Mtume kwenda kwa maswahaba, kwenda kwa wanafunzi wa maswahaba waliyotapakaa mpaka kufika kwetu.
Na kwa mlolongo huo nikakuambia Qur'an inatafsiriwa kwa nyenzo 3.
1)Qur'an bi Qur'an
2)Qur'an kwa sunna za Bw. Mtume
3) Qur'an kwa kupitia maswahaba ambao ni wanafunzi wa Mtume
Wapi nilipoandika Qur'an inatafsiriwa kwa uelewa wao?
Mbali na ufahamu wako mdogo, au najadiliana na mtu ambaye amelewa?
Wewe si muislamu na hujaisoma hii dini!Mzeebaba unaweza kujadili kwa amani au huwezi?
Weka uelewa wako wa jinsi umeelewa hii mada ili tujadiliane kulingana na maelezo yako. Kama huwezi kuleta uelewa wako leta maoni ya hao unaowaamini ili tuendelee na mada. Naona umekazania uelewa wangu mdogo, ndo nipo hapa kuukuza uwe makubwa kwa hiyo tuvumiliane.
NB. Inawezekana umetoa maoni yako kuhusu unavyoielewa hii Aya, naomba nikumbushe.
Mimi nazungumza kulingana na nilivyoelewa, wewe ndo muislam mwenye kuzifata hizo Aya, utakachokifanya ni kunielekeza kulingana na Imani yenu ilivyo.Wewe si muislamu na hujaisoma hii dini!
Sisi ni waislamu na tumeisoma hii dini!
Ajabu wewe ambaye si muislamu na hujaisoma hii dini unaona mtazamo wako upo sahihi juu ya masuala ya elimu yahusiyo dini ya uislam.
Jipime wewe mwenyewe, tukufafanuaje?
Kuzaliwa katika uislamu sio hoja,kuna waislamu wengi wana majina ya kiislamu lkn hawajui uislamu waoNdugu Uislamu sio dini ya amani huo ni UPOTOSHAJI ,umetoa maelezo ya uongo ,
hoja yako kwamba Waislamu hawakupigana bila sababu ni upotoshaji mkubwa ,labda unadhani hatuujui uislamu ,binafsi nimezaliwa kwenye uislamu,nimesoma uislamu,kwahiyo naongea ninachokijua,kwa sababu historia na Qur’an yenyewe zinaonyesha kwamba si kila vita ilikuwa ya kujilinda kama unavyosema ,
Kwa mfano, vita ya Khaybar, Banu Qurayza, na vita zingine nyingi zilikuwa ni za kushambulia na kueneza Uislamu kwa nguvu jambo linalopingana moja kwa moja na dhana ya AMANI unayosema hapa ..
Tukirudi kwenye Qur’an, kuna Aya nyingi ambazo hazihusu kujilinda bali zinachochea mashambulizi ya wazi. Mfano nitakupa Aya kadhaa hapa👇👇
Surah At-Tawbah 9:29
"Piganeni na wale wasioamini katika Mwenyezi Mungu... mpaka walipe kodi kwa unyenyekevu nao wakiwa wanyonge."
Hii ni amri ya wazi ya kushambulia wasiokuwa Waislamu na kuwafanya kuwa chini ya utawala wa Kiislamu kwa kulipa Jizya si kwa kujilinda, bali kwa kutawala.
Surah Muhammad 47:4
"Basi mnapokutana na wale waliokufuru wapigeni shingoni mwao..."
Hii pia si hoja ya kujilinda, bali ni amri ya vita dhidi ya wasiokuwa Waislamu kwa sababu tu ya imani yao.
Hata mtume wenu Muhammad alikiri kwamba ametumwa kwa upanga.
Tafsiri za hadithi maarufu zinaeleza
Sahih al-Bukhari (Hadith 2948)
"Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka washuhudie kwamba hakuna mungu ila Allah..."
Hii inapingana na hoja yako ya kwamba vita zilikuwa kwa kujilinda tu.
Viongozi wengi wa Kiislamu baada ya Muhammad waliendeleza utawala wa upanga: Mashambulizi dhidi ya Uajemi, Byzantine, India, Afrika Kaskazini haya yote hayakuwa kujilinda, bali ni kueneza Uislamu kwa nguvu. Hilo linaelezwa hata na wanazuoni wa Kiislamu kama Ibn Khaldun aliyekiri kuwa jihadi ni njia halali ya kueneza dini kwa mujibu wa Sharia.
Na kuhusu hoja kwamba “Mitume wote walikataliwa,” ni kweli walikumbana na upinzani, lakini hakuna kati yao aliyepiga vita kwa ajili ya kueneza ujumbe wake kama Muhammad alivyoagiza.
Yesu alisema
“Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi...” (Mathayo 5:44)
Yesu alikataa kutumia upanga (Mathayo 26:52), tofauti na Muhammad ambaye alisema:
"Nimekuja kwa upanga." (Ibn Sa’d, Kitab al-Tabaqat al-Kabir)
Kwa hiyo si kweli kwamba Uislamu ni dini ya amani .
Uislamu unaruhusu mapigano ya kimwili kwa sababu ya dini jambo linalotofautiana na mafundisho ya injili ya upendo, msamaha, na kuvumilia mateso.
Aya hii inasisitiza kuwa haki haipaswi kupindishwa kwa upendeleo wa familia au maslahi binafsi.
Hata kama mnamchukia mtu, bado ni wajibu kutenda haki.
Aya hii hutajwa sana katika khutuba za Ijumaa, ikisisitiza kwamba uadilifu ni msingi wa amri za Mwenyezi Mungu.
Aya hizo ulizo zitaja hazija agiza tu watu wapigane vita bila sababu,bali vita vilipiganwa katika kuondoa dhuluma,kuweka uadilifu katika jamii,na kusimamisha hakiMuda wa porojo haupo ndugu, jikite kwenye hoja na mada
Sikutumia ISIS kama kipimo cha Uislamu mzima, bali nilisema wazi kuwa vitendo vyao vinaendana moja kwa moja na baadhi ya Aya na Hadith za Kiislamu. Wao hawatungi sheria, wanatekeleza zilizoandikwa. Mfano:
Qur’an 9:5
"Waue washirikina popote mnapowakuta..."
Qur’an 8:12
"Nitatie hofu katika nyoyo za waliokufuru, wapigeni juu ya shingo..."
Sahih Muslim 1:33
"Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka washuhudie kuwa hakuna mungu ila Allah..."
Sasa swali ni Je, ISIS walitunga aya hizi au wanazitekeleza?
Hata viongozi wa ISIS wamesema,
"Tunaleta Khilafa kwa kufuata Qur’an na Sunnah za Muhammad."
Hii haimaanishi kila Muislamu ni gaidi lakini inamaanisha maandiko yao yanaruhusu au hata kuamuru vitendo vya kimabavu dhidi ya wasioamini, na mtu yeyote anayetaka kuchukua maandiko hayo kwa usomaji wa moja kwa moja (literal interpretation) ataishia kama ISIS.
Hata wewe ukiyatumia maandiko vizuri ya Quran na hadithi lazima uwe GAIDI
Ok nitakujibu kadri nilivyojaaliwa ,Aya hizo ulizo zitaja hazija agiza tu watu wapigane vita bila sababu,bali vita vilipiganwa katika kuondoa dhuluma,kuweka uadilifu katika jamii,na kusimamisha haki
Uislamu upo kwa maslahi ya jamii nzima,pale panapokuwa na uonevu wa namna yoyote basi hatua zilihitajika kuweka mambo sawa
Waislamu walipigana na wale ambao walistahili kupigwa
Vile vile madhara waliyofanyiwa waislamu na wazushi wanatakiwa warudishe madhara yale yale kama waliyofanyiwa
Vile vile Mwenyezi Mungu hapendi wale wanao anzisha vita
Tusome aya zifuatazo:
Katika Qur’an, kuna aya zinazoruhusu Waislamu kujilinda dhidi ya dhulma, lakini pia zinasisitiza kujizuia, kusamehe, au kulipa kwa uadilifu. Hapa ni baadhi ya aya husika:
1. Surat Al-Baqarah (2:190)
“Piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaowapiga, lakini msianze uadui. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaoanzisha vita.”
2. Surat Al-Baqarah (2:194)
“... Basi anaye kudhuru, mdhuru sawa na alivyo kudhuru...”
3. Surat Ash-Shura (42:40)
“Na kisasi cha uovu ni uovu kama huo. Lakini anayesamehe na kusuluhisha, basi thawabu yake iko kwa Mwenyezi Mungu...”
4. Surat Al-Hajj (22:39)
“Wameruhusiwa kupigana wale wanaodhulumiwa, na hakika Mwenyezi Mungu anao uwezo wa kuwasaidia.”
Aya hizi zinaweka mizani ya uadilifu: Waislamu wanaruhusiwa kujilinda dhidi ya mashambulizi, lakini hawapaswi kuvuka mipaka, na kusamehe kunapendekezwa zaidi.
Sasa tuje tuangalie njia za kupigana vita, Vita ambazo waislamu walikuwa wanapigana zilikuwa kwa wale tu wenye kushika silaha,lakini haikuruhusiwa kuwapiga wazee,wanawake na watoto
Vile vile haikupaswa kuharibu mazao,majumba ya ibada
Lakini je ISIS wanafanya hivyo? Utakuta hao ni magaidi wanapigana kwa kivuli cha Uislamu lakini nyuma yake ni wahalifu kama wahalifu wengine
jipange expert wangu
Kesho inshaAllah tutaendelea na mjadala
Asante
Ndugu yangu unachanganya propaganda na ukweli uliopo, naimani na nitakuombea utoke kwenye uislamu umpokee Yesu kama Bwana na mwokozi wa MAISHA yako.Kuzaliwa katika uislamu sio hoja,kuna waislamu wengi wana majina ya kiislamu lkn hawajui uislamu wao
Mmoja wapo ni wewe,lau ungeujua Uislamu usingekuwa kafiri abadani kwakuwa unajua kabisa yeyote anayemshirikisha Allah ni motoni,kwahiyo huna unachokijua katika Uislamu
Uuslamu ni dini ya amani sana ila makafiri wametengeneza propaganda nyingi sana juu ya hoja hii matokeo yake wote nyie mmeingia kwenye mfumo na kuimba wimbo ule ule
Mtume Muhammad swalla aallahu alaih wasallamu,kabla ya kupigana vita yoyote ile kwanza alifanya mazungumzo mengi sana juu ya kutafuta suluhu na kuepuka vita
Ukichukulia kwanza wengi ambao walikuwa ni washirikina walikuwa ndugu na wale ambao wameukubali Uislamu,kwahiyo zilifanyika juhudi nyingi sana,pale zilipo shindikana ndio vita vikachukua nafasi
Mfano mzuri ni mkataba wa Udaibiyah,hawa Mtume na wafuasi wake walikuwa wanaenda kuhiji Makka pasina silaha zozote zile,walienda kwa amani,sasa washirikina wa Makka waliposikia Muhammad anaongozana na msafara mkubwa kwenda Makka,basi wakataka kuwazuia wasiingie Makka au walitaka vita
Lakini Muhammad swalla aallahu alaih wasallamu alisema wanaenda kwa amani,ndio mkataba ukafungwa,lkn mkataba huu haukuwa na maslahi yoyote na waislamu
Moja wapo ya vipengele ni kwamba,mshirikina akienda Madina basi arudishwe Makka kwa watu wake,lakini muislamu akienda Makka asirudishwe
Kufupisha story kuna vipengele vingi sana viliwapa favor washirikina na kuwabana waislamu
Ikafikia kipindi masahaba wakataka kupigana vita,lakni Mtume akakubali akakubali mkataba wa upande mmoja lengo ni kuepusha vita
Kuna masahaba wa Mtume walienda kwenye kabila moja kwa amani kabisa kuutangaza uislamu,lkn wale masahaba 70 wote waliuwawa,je kwa hali hiyo ungetegemea waislamu wachukue hatua gani kama sio kulipiza kisasi
Vita nyingine hazikuwa vita hasa bali ni mbinu za kivita kuwazunguka maadui,kuna makabila ambayo yalileta uasi kwenye dola ya kiislamu,waislamu walichofanya ni kwenye kuwazingira kwa masiku kadhaa mpaka wakaomba poo
Kwahiyo hizo zinazo itwa vita kwa asilimia kubwa zilikuwa ni kuzuia au kuweka mambo sawa baada ya waasi kutaka kupima nguvu ya waislamu
Na kwa taarifa yako,kihistoria waarabu walikuwa wako proud sana na historia yao ya vita hata kabla ya Uislamu kuenea kwa wingi,mtu anaweza kuhadithia ushindi wa vita flani ambazo babu zake walishinda miaka kadhaa huko nyuma,kwahiyo matokeo historia ya bara arabu imejaa visa vingi vya mambo ya vita na watu kwa bahati mbaya wakahusisha vita hizo na Uislamu
Waislamu walieneza dini yao kwa amani ikiwemo kupewa hoja ambazo ziliwaingia kwenye nyoyo zao na wenyewe kwa hiari yao wakaingia katika Uislamu
Mfano mzuri baada ya waislamu kuiteka Hagia Sofia,watu waliachwa huru kuabudu dini zao wakiwemo wakristo,ikafikia kipindi watu waliwapenda zaidi waislamu kuliko hata Waroma,kwakuwa katika Uislamu kuna haki
Uislamu unatufundisha kutenda haki hata ikiwa dhidi ya ndugu yako mwenyewe
Angalia aya zifuatazo:
Katika Uislamu, kutenda haki ni jambo kuu sana. Qur’an inaagiza waislamu watende haki hata kama ni dhidi yao wenyewe au ndugu zao. Hizi ni aya muhimu kuhusu haki (uadilifu):
---
1. Surat An-Nisa (4:135):
"Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi wa haki, mkitoa ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapokuwa ni kinyume na nafsi zenu au wazazi wawili au jamaa wa karibu..."
---
2. Surat Al-Ma’idah (5:8):
"Enyi mlioamini! Kuweni wasimamizi wa Mwenyezi Mungu kwa ushuhuda wa haki. Wala chuki ya watu isiwakupelekeeni kutokutenda haki. Tendeni haki; hiyo ndiyo karibu na uchamungu..."
---
3. Surat An-Nahl (16:90):
"Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu, ihsani, na kuwapa jamaa..."
---
Hitimisho:
Katika Uislamu, uadilifu ni msingi wa imani. Muislamu anatakiwa kuwa na mizani ya haki daima, bila upendeleo wala uonevu – iwe kwa ndugu, marafiki au maadui.
Je,ukristo unasemaje kuhusu Upanga:
1. Mathayo 10:34
"Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la, sikukuja kuleta amani, bali upanga."
2. Luka 22:36
"Basi akawaambia, lakini sasa, yeye aliye na mfuko, na auchukue, na vivyo hivyo mkoba; na yeye asiye na upanga, na auze joho lake, akanunue upanga."
Jipange expert wangu!
Huwa unapenda sana kutilia mkazo wa kufuata historia na maandiko ya huko zamani,waandishi wengi ni makafir kama wewe,ambao waliandika kwa lengo la kuuchafua Uislamu na waislamu,na ambao rejea zao ndio zinawapotosha wengi sana ukiwemo na wewe,halafu unakuja hapa kifua mbele kana kwamba unayosema ni sahihiNitaendelea kukujibu kadri ninavyoweza ,maana ni wazi waislamu hamtaki kutoka nje ya box ,hamtaki Kuhoji Imani yenu kuona kwanini imekuwa hivi na sio vile ,
Jitahidi kusoma historia ,AKIOLOJIA na maandiko kabla ya kuja uislamu,uzuri hata Quran imewaambia msome kwa wale waliopewa kitabu kabla yenu
Kaka, kusema kuwa kukubali uumbaji wa Mungu ni sawa na kuwa Muislamu si hoja inayojitosheleza. Maana kila mwanadamu anayekubali kuwa kuna Muumba hajawa Muislamu moja kwa moja. Wakristo, Wayahudi, na hata dini za jadi pia wanakubali kuwa Mungu yupo na ndiye Muumba, lakini hawaitwi Waislamu.
Kuwa Muislamu ni zaidi ya kukubali uumbaji ni kukubali mafundisho ya Muhammad na Qur’an kuwa ndiyo njia sahihi ya kumfikia Mungu, jambo ambalo si kila mtu anakubaliana nalo.
Kuhusu Iblis kukataa kumsujudia Adam kwa sababu ya kiburi, hiyo hadithi imo ndani ya Qur’an na inafanana na simulizi za kale za Kiyahudi (Midrash). Lakini hata hivyo, inaibua maswali mengi fikirishi ,
Kama kusujudu ni kwa Allah peke yake, kwa nini Allah mwenyewe aagize viumbe wamsujudie kiumbe mwingine, hata kama ni kwa “heshima”?
Hii inazua mkanganyiko kuhusu maadili ya kiungu kwani Mungu angeagiza jambo linalochanganya ibada na heshima?
Na kama Iblis alihukumiwa kwa sababu ya kukataa agizo hilo, je, adhabu hiyo ni kwa sababu ya uasi au kwa sababu alitumia akili kufikiri tofauti? Hii inafanya mtu ajiulize je, imani ya kweli inahitaji kufuata kila agizo bila kuuliza, au inahitaji kuelewa kiini cha agizo hilo?
Kwa hiyo, hoja ya kwamba kujisalimisha kwa uumbaji ni sawa na kuwa Muislamu, au kwamba Iblis alikosea kwa kukataa “sujudu ya heshima,” si hoja yenye nguvu ya kiakili wala ya kiroho. Ukweli unapatikana si kwa kufuata simulizi, bali kwa kumjua Mungu aliye Hai, ambaye alijifunua kwa ulimwengu kupitia Yesu Kristo.
Ndugu yangu, kabla ya kujenga hoja kwa jazba na kejeli, ni muhimu kukubali ukweli wa kihistoria, Uislamu ni dini mpya ukilinganisha na dini ya Uyahudi na Ukristo. Uislamu ulianza karne ya 7 (baada ya Kristo), wakati tayari Biblia ilikuwa imekamilika, Wayahudi walikuwa na Torati na Wakristo walikuwa wameenea sehemu kubwa ya dunia.Huwa unapenda sana kutilia mkazo wa kufuata historia na maandiko ya huko zamani,waandishi wengi ni makafir kama wewe,ambao waliandika kwa lengo la kuuchafua Uislamu na waislamu,na ambao rejea zao ndio zinawapotosha wengi sana ukiwemo na wewe,halafu unakuja hapa kifua mbele kana kwamba unayosema ni sahihi
Sisi tunazijua hizo propaganda zao na hatuwezi kuzichukua kama rejea za kupata maarifa,hizo ni kwa ajili yenu
Huwa nafurajishwa sana mkristo anapojifanya anatumia hoja za akili wakati yeye mwenyewe ameshindwa kutumia hoja ya akili katika dini yake
Mfano,kuamini kwamba Mungu alijibadilisha katika umbo la kibina damu ili aje ateswe na kuwakomboa wanadamu katika dhambi, huu ni upuuzi wa hali ya juu sana,kama umeshindwa kutumia akili hapa,je utaweza kutumia akili sehemu nyingine?
Kama unaamini Mungu kazaliwa na mwanamke na akakaa tumboni miezi tisa,akaja kuwa fundi selemala na baadae kuwaambia watu kuwa yeye ni Mungu,mtu anayeamini haya ana uwezo gani wa kutumia akili yake?
Anyway twende kazi, nakufundisha ujue tofauti ya jambo la kiibada na jamba ambalo sio kiibada
Ibada ni matendo au maneno mazuri ambayo anayapenda Mwenyezi Mungu,na haya yana malipo kutoka kwake
Kwahiyo Kusujudu kama ibada ni kwa ajili ya Allah tu
Wakati Allah anataka kumuumba mwanaadamu aliwaambia Malaika kwamba nataka kumuumba hiki kiumbe,wao Malaika wakasema "unataka kumuumba kiumbe kingine ambacho kitakuja kumwaga damu na ufisadi"
Allah akasema "mimi nayajua msiyoyajua nyinyi"
Baada ya uumbwaji wa adamu, Allah subhaanahu wa Taala akawauliza malaika wataje majina ya vitu vyote,wao wakashinda
Alipoulizwa Adamu akataja majina ya vitu vyote,ndio hapo Allah akaagiza Malaika na Iblis wamsujidie Adam sijida ya heshima
Sasa Iblis alikaidi amri ya Mola wake,ndio akahukumiwa motoni kwasababu ya kuonyesha kiburi mbele ya Allah
Na hata pale Iblis alipo wahadaa Adam na Hawa kule bustanini, Adam aliomba msamaha kwa Mola wake na akasamehewa lakini Iblis hakuomba msamaha,hii inaonyesha ni tabia yake ya kiburi
Na Allah ndio mwenye kujua yote,alijua hiki kiumbe ni kikaidi na hakitobadilika
Unasema ulikuwa Muislamu,unajivua nguo mwenyewe,lau ungekuwa usingeuliza swala hili
Na hii sijida ya heshima hata wazazi wake nabii Yusuphu waliifanya kwa Yusuphu pale walipo mkuta Yusuphu akiwa na mamlaka nchini Misri
jipange expert wangu
Hauwezi kuwa serious wewe,yaani uwe na uhakika na imani ambayo inajicontradict severeNdugu yangu, kabla ya kujenga hoja kwa jazba na kejeli, ni muhimu kukubali ukweli wa kihistoria, Uislamu ni dini mpya ukilinganisha na dini ya Uyahudi na Ukristo. Uislamu ulianza karne ya 7 (baada ya Kristo), wakati tayari Biblia ilikuwa imekamilika, Wayahudi walikuwa na Torati na Wakristo walikuwa wameenea sehemu kubwa ya dunia.
Hii ina maana kwamba Uislamu uliingia katika dunia ambayo tayari ilikuwa na historia ndefu ya dini, maandiko, na mitazamo kuhusu Mungu., Uislamu umekuja umekuta Kuna vitabu vingi vya historia ,hata hiyo Quran yako imekopi visa vingi sana kutoka vitabu vya apokrifa,ukitaka ushahidi nitakupa utashangaa sana ,
Huwezi kuja baadae halafu ukatae kila kitu kilichokutangulia kana kwamba hakina msingi, halafu ujiite peke yako mwenye “ukweli wa mwisho”., ndugu Uislamu ni dini mpya
Sasa waliandikaje historia ya kuchafua uislamu wakati haukuwepo ,Nina vitabu vya historia Hadi vya 95AD ,kuja Hadi 500AD hapo hakuna kitu kinaitwa UISLAMU,
Zaidi ya hapo, hata wanazuoni wa Kiislamu wenyewe hawapingi kila kitu kilichoandikwa kabla ya Uislamu.
Kwa mfano, wanahistoria wa Kiislamu kama Ibn Ishaq, Ibn Hisham, Al-Tabari, na Ibn Kathir wameandika wazi kabisa kuhusu maisha ya Muhammad na pia wamekiri uwepo wa maandiko ya kale kama Taurati na Injili.
Wengine kama Al-Bukhari na Muslim walikusanya Hadith ambazo zinaonyesha uhusiano wa karibu wa Uislamu na dini zilizokuwepo kabla, hasa Uyahudi na Ukristo. Kwa hiyo si sahihi kusema kila aliyeandika historia ya dini ni kafiri mwenye nia ya kuchafua Uislamu, hasa mnapotegemea hao hao wanazuoni kwenye maelezo ya historia ya dini yenu.
Umekuja na hoja ya kudharau Ukristo eti kwa sababu Mungu alikuja kwa mfano wa mwanadamu, ni vyema tukubaliane kwamba hoja hiyo haipingwi kwa akili bali kwa mtazamo wa kidini wa Kiislamu.,dini ambayo ni mpya kabisa ,
Kama kweli Mungu ni mwenye uwezo wote, basi hawezi kushindwa kuchukua umbile la mwanadamu kwa lengo la kuwaokoa viumbe wake. Huo ni wema na upendo, si udhaifu. Na kama unakubali kuwa Malaika walisujudu Adamu kwa amri ya Allah, na wazazi wa Yusufu walimsujudia Yusufu kwa heshima, basi huwezi kuwalaumu wanaomsujudia Yesu aliyezaliwa kwa muujiza, akaponya, akafufua wafu, na akafufuka mwenyewe kutoka kwa wafu. Hilo ni tukio ambalo halijawahi kutokea kwa mwingine yeyote katika historia.
Kwa kweli, hoja zako si mpya. Zimeshaelezwa na kupingwa na Wakristo kwa karne nyingi sasa. Ni vizuri kujifunza na kuchunguza kwa undani kabla ya kupinga kwa matusi au dhihaka. Dini yoyote inayokwepa maswali, inayokataa historia, na inayoogopa hoja huwa ina udhaifu ndani yake.
Mimi nina uhakika wa imani yangu kwa sababu nimechunguza kila upande, nimepima kwa historia, akili na maandiko. Naomba na wewe ufanye hivyo kwa moyo wa kutafuta kweli, si kwa jazba.
Maandiko ambayo ni ya Injili ya Yesu ni yale ambayo yana mafundisho sahihi,ambayo yanaendana na vitabu vya Mwenyezi Mungu toka kwenye Zaburi,Torati,Injili na Qur'anNaona unarudi kule kule ,kwanza
Niambie ni maandiko yapi ya biblia unayaamini na yapi huyaamini ,halafu nijuze huyaamini kwasababu hayaendani na Quran au kwasababu hayakusaidii kujenga hoja zako?
Kisha tuendelee
Nimeona unapotosha Yesu alifundisha uislamu,kijana acha huu ujinga humu wenzako walishaachana nazo hizo hoja dhaifu
Yesu alimuita Mungu baba ,je Uislamu unakubali Mungu kuitwa baba ?
Je Unajua Yesu na ISSA ni watu wawili tofauti wenye Sifa tofauti kabisa ?
wewe ni moja kwa moja 'fi nnaar jahannam', usitafute wa kufuatana naoMi nimemuuliza jamaa hapo juu amesema Allah anaenda jehanamu. Sasa kama na mimi naenda sio mbaya kama Mungu anataka niende huko.....ila Muhammad ni uhakika ana moto wake wa pekee kwa kuharibu ulimwenguni
Siri moja kubwa ya mtu ambaye hajiamini au anatapatapa ni kutafuta sababu zisizo na msingi na kuzifanya za msingiNilikwambia usitumie CHATGPT nilikuwa namaanisha kubwa ,sababu kwanza inakulemaza ,pili inakupa majibu ambayo ni yale yale ya UPOTOSHAJI wa kila siku ,nilikuwa na maana kubwa tu,
Unachofanya hapo wenzio walishafanya , yaani ni kituko
Una compare Biblia na Quran ,una compare manabii wa kiyahudi na uongo wa Muhammad,kwanza unazalisha maswali mengi sana
Unatakiwa ujue na ni wazi ipo hivo kabla ya Muhammad hakukuwahi kuwepo uislamu au dini ya Uislamu,
Mitume na manabii wote wa kiyahudi historia zao zipo, walikuwa dini ya kiyahudi ,mbali kabisa na uislamu
Ni wazi huna elimu na dini yako ,ndio maana ninapokuhoji unaenda unapachika kwa CHATGPT inakujibu kwa kadiri ya propaganda za Uislamu
Kwanza huoni unajikoroga?
Biblia huiamini, hapo hapo unataka kuitumia justify uislamu,
Hii ni mbinu ishapitwa na wakati ,utakapokuja na akili yako njoo tujadili ,
Ni kweli, kuna tofauti kati ya Uislamu na nguzo za Uislamu, na ni kweli pia kwamba Mitume wote waliwafundisha watu kumtii Mungu Mmoja na kuacha maovu. Lakini hoja ya msingi hapa si kama watu wa kale walimtii Mungu bali ni kama walifuata "Uislamu" kama dini au la.,hiyo ndio hoja yangu , Uislamu kama dini kuwepo kabla ya Muhammad,sio kuungaunga kwa kuokoteza Aya za biblia ambayo dakika moja mbele nikikubana unasema imetiwa mikono ili Hali biblia halisi huna .
Huwezi kusema kwamba Musa, Daudi au Yesu walikuwa Waislamu kwa sababu hawakutamka shahada ya Muhammad, wala hawakufundisha watu kuswali rakaa tano, kufunga Ramadhani, au kwenda Hajj Makka hizo ni sheria mpya, si mwendelezo tu.
Kama dini ya kweli ni ile iliyokuwepo tangu zamani, basi Uislamu ulioletwa na Muhammad si wa asili bali wa marekebisho ya baadaye na Biblia haimtaji Muhammad popote kama nabii ajaye. Hivyo, kudai kwamba Uislamu wa sasa ni mwendelezo wa dini ya Mitume wote si sahihi kihistoria wala ki maandiko.,huu ni UPOTOSHAJI mkubwa , Huwa napenda kusema Uislamu ni dini mpya,maana imekuja tayari Kuna dini imezikuta,imekuta Kuna historia, vitabu,teknolojia,n.k
Jitahidi kujadili kama unamfundisha au kumlingania mtu ambaye anatakiwa aingie kwenye uislamu bila propaganda au Taqya ,
Nina maswali matano kwako maana hoja zako ulizojibu kwa CHATGPT zimezalisha maswali mengi sana ambayo mtu anayekusikiliza zaidi unazidi kumfanya atilie mashaka uislamu
Kama Mitume wote walikuwa Waislamu, mbona hawakufundisha watu kusema
"Ash-hadu alla ilaha illa Allah, wa ash-hadu anna Muhammad rasulullah"?
kama Musa au Yesu walikuwa Waislamu, mbona hawakwenda Hajj Makka, hawakufunga Ramadhani, wala kuswali rakaa tano?
Kama Uislamu ni dini ya kale kabisa, mbona jina "Uislamu" na "Waislamu" havijatajwa hata mara moja katika Biblia nzima au vitabu vya kale?
Kama sheria tu ndio tofauti ila msingi ni uleule, kwanini Qur'an inasema
"dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa"? Mbona haikusema “dini yoyote inayomwabudu Mungu mmoja ni sawa”?
Mbona Yesu hakusema popote kwamba baada yake atakuja Muhammad? Badala yake alisema “Mimi ndimi njia, kweli, na uzima, mtu haendi kwa Baba ila kwa njia ya mimi” (Yohana 14:6)
Najua utaenda kuuliza kwa CHATGPT,litakupa majibu kulingana na propaganda za Uislamu ila utazalisha maswali zaidi, jitahidi kujibu kama unamfundisha au kumlingania mtu anayetakiwa kuingia kwenye dini isiyo na shaka kama uislamu unavyosemwa