Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Tunataka katiba ambayo wateuliwa katika nafasi nyeti watahojiwa na kamati za bunge, weledi wao kutathiminiwa na wathibitishwe na bunge. Kama hizo kamati za bunge zikiridhia hao wapwa na watoto wa rais kushika hizo nafasi baada ya kuteuliwa na baba yao sawa tu.
Mkuu unatakiwa utulie kwenye mada moja moja,kule kwa majaliwa umeondoka umekuja kuanzisha uzi huku anyway acha na hapa tuwe pamoja.
Naomba uniambie ni katiba ya nchi gani hairuhusu mtu kumchagua ndugu yake au mtu wake wa karibu kuwa katika nafasi husika pale endapo tu atakidhi vigezo husika ?
Hapo kwenye vigezo ndio point ya msingi.
Kwa sababu raisi hana uwezo wa kumchukua kaka yake ambaye yupo mtaani akamchagua akawa IGP lazima IGP awe askari wa cheo fulani.
Hiko kitendo cha kuwa askari wa cheo fulani ndio kigezo chenyewe.
Sasa kama amekidhi vigezo vya kuwa IGP yaani ni askari wa cheo fulani alafu ni ndugu yake naomba uniambie ni katiba ya Nchi gani hapa duniani inakataza jambo hilo ?
Lakini pili ukitaka katiba ambayo raisi hatoruhusiwa kumchagua ndugu yake ama mtu wake wa karibu katika nafasi fulani basi naomba UNIPE SABABU MBILI TU KWA NINI HII ISIWE KATIKA INAYOMBAGUA RAISI KATIKA KUTEUA ?
kwa nini isiwe katiba baguzi dhidi ya raisi ?