Je, wajua nini hutokea katika Ulimwengu wa Roho wawili wanapoungana katika NDOA Takatifu?

Asili ya NDOA duniani ni Edeni.

Mungu hakukosea kumpa Adam mke mmoja.

Abraham alikuwa mpagani, na Mungu alipomchagua alimtumia hivyo hivyo.

Amen
 
Ndoa haifungwi kanisani na mchungaji hafungishi ndoa ule ni ushahidi tu, Ndoa nia agano la kiroho na inafungwa mara Moja tu basi kwenye maisha ya mwanamke nayo ni siku ile tu anayoitoa bikra yake.

Ndoa za sasa ni maigizo ya ndoa, mwanamke mchafu na mzinifu anaokotana na kijana wanaenda Kwa mchungaji (pengine ni mlevi, muongo, muasherati nk) anawaambia kuanzia Leo ninyi ni mke na mume na wenyewe ndio wanaota ndoa takatifu.

Ndoa ni agano, ukisikia mfalme Suleiman alioa wake zaidi ya mia Saba sio kama alikuwa anafungishwa ndoa kanisani ni wanawake aliowatoa usichana.

Hesabu 31: 17- 18 Mungu aliagiza hivi
'
Kwa hiyo basi, waueni watoto wote wa kiume na kila mwanamke aliyewahi kulala na mwanamume.'
 
Hao manabii na mitume waliokuwa wanaoa mke zaidi ya mmoja walikuwa wanaenda tofauti na MUNGU?
(Mathayo 19:3-9.)

Wanafunzi wa Yesu walimwuliza Yesu swali Hilo Hilo,

Na aliwajibu,

Musa ndiye aliwaruhusu kuacha mke na Kuoa wake wengi.

Akajibu kuwa warudi Edeni, Mungu aliumba mke mmoja, mume mmoja basi,

Zaidi ya hapo ni UASHERATI na UZINZI.
 
Licha ya Utamu unaohubiriwa siku zote ndani ya ndoa. Kwa baadhi imekua ni shubiri.

Wanandoa wameoana bila kua na Uelewa na ufahamu wa kutosha juu ya ndoa.
Wakazingatia zaidi vichocheo vya kimwili na fedha na sio upendo..

wako wanajutra sasa maeneo mbalimbali mtaani, wamekua ni wanaharakati sasa wa haki sawa kwenye ndoa...
Na wameshaanza na wanazibomoa kwelikweli..
 
Kuoa mke au Kuolewa na mume asiye ubavu wako ni kukumbatia miiba.

MKE hapatikani Kwa pesa, mke Si Kwa ajili ya tamaa ya macho pekee,

MKE au mume ni reflection ya familia ya Mungu duniani.

Watu wamuulize Mungu kabla ya Kuoa, atawapa mke au mume sahihi.

Amen
 
shukrani sana 💪👌
 
Ingekuwa kheri kwako kukubali kuwa u kipofu Ili ushikwe mkono kuelekezwa njia sahihi.

Amen
 
NDOA halali ni ya mke mmoja na mume mmoja,

AGANO la kale walifanya hivyo na Musa aliruhusu sababu ya ugumu wa mioyo Yao.

( Mathayo 19:3-9). Yesu kapigilia mstari kuwa, Kuoa wake wengi au kuacha mke ni UASHERATI na UZINZI!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…