Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 32,639
- 42,908
Neno la Mungu halibadiliki toka mwanzo mpaka sasa na Kristo ni yule yule toka mwanzo mpaka sasa.Kwanini zote zitumike na unadai agano jipya ndio halisi na la kale ni kivuli?
Kwanini waendelee kutumia vitu viwili wakati kimoja ndio halisi kwa madai yako?
Neno la Mungu halijawahi kupitwa na wakati toka mwanzo mpaka sasa.
Tunaposema agano la kale ni kivuli cha agano jipya hatumaanishi la kale limekufa na halifai kutumika tena.
Hebu angalia mtume Paulo anavyosema.
Soma waebrania 8:1-13 yote Ila nasisitiza mstari wa 13
Waebrania 8:13
"Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka."
Ukilisoma agano la kale kwa picha ya agano jipya utalielewa vizuri sana na Kristo utamuona vizuri humo.
Ndio maana Yesu alisema hakuja kuivunja torati Ila kuikamilisha.
Amri ya 6 ya torati inasema usizini Ila kwa agano jipya ni kwamba ukimtamani mwanamke toka moyoni umeshazini.
Amri ya 5 inasema usiue Ila kwa agano jipya yeyote anayemchukia ndugu yake ni muuaji.
zitto junior Mathanzua