Mkuu nimefurahi kwakuwa Umenotice kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake/Kaka zake...
Sasa nifatilie..
Kwanza kabisa utambulisho wa Ndugu hao Unaanza kwenye Mathayo 13:55-56
Nitakuandikia kiyunani (Greek) as the original language....
"
Οὐχ οὗτός ἐστιν ὁ τοῦ τέκτονος υἱός; οὐχ ἡ μήτηρ αὐτοῦ λέγεται Μαρία καὶ οἱ ἀδελφοὶ αὐτοῦ Ἰάκωβος καὶ Ἰωσὴφ καὶ Σίμων καὶ Ἰούδας; καὶ αἱ ἀδελφαὶ αὐτοῦ οὐχὶ πᾶσαι πρὸς ἡμᾶς εἰσιν; πόθεν οὖν τούτῳ ταῦτα πάντα;
Na hivi ndivyo hutamkwa...
Ouch houtos estin ho tou tektonos huios? ouch he meter autou legetai Maria kai hoi adelphoi autou Iakobos kai Ioseph kai Simon kai Ioudas? kai hai adelphai autou ouchi pasai pros hēmas eisin? pothen oun touto panta?
Kwa mama Samia tungeandika hivi..
Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?
Na dada zake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote?
neno lililotumika kama Ndugu(Kaka ) ni ἀδελφοὶ" (adelphoi) na Mara zote hutumiwa kwa Ndugu wa Damu yaani wale wa Tumbo moja...
kwa case yako kuwa Huenda lilitumika kama Ndugu wa Dada ake Mama yake..
neno ambalo lingetumika nafikiri lingekuwa ανηψιός (anepsiós)
Sasa kama utaweza bado swali liko pale pale walikuwa watoto wa nani!