Je, wajua nini hutokea katika Ulimwengu wa Roho wawili wanapoungana katika NDOA Takatifu?

Kwanini zote zitumike na unadai agano jipya ndio halisi na la kale ni kivuli?

Kwanini waendelee kutumia vitu viwili wakati kimoja ndio halisi kwa madai yako?
Neno la Mungu halibadiliki toka mwanzo mpaka sasa na Kristo ni yule yule toka mwanzo mpaka sasa.

Neno la Mungu halijawahi kupitwa na wakati toka mwanzo mpaka sasa.


Tunaposema agano la kale ni kivuli cha agano jipya hatumaanishi la kale limekufa na halifai kutumika tena.

Hebu angalia mtume Paulo anavyosema.

Soma waebrania 8:1-13 yote Ila nasisitiza mstari wa 13

Waebrania 8:13
"Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka."

Ukilisoma agano la kale kwa picha ya agano jipya utalielewa vizuri sana na Kristo utamuona vizuri humo.

Ndio maana Yesu alisema hakuja kuivunja torati Ila kuikamilisha.

Amri ya 6 ya torati inasema usizini Ila kwa agano jipya ni kwamba ukimtamani mwanamke toka moyoni umeshazini.

Amri ya 5 inasema usiue Ila kwa agano jipya yeyote anayemchukia ndugu yake ni muuaji.

zitto junior Mathanzua
 
Mkuu nimefurahi kwakuwa Umenotice kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake/Kaka zake...

Sasa nifatilie..
Kwanza kabisa utambulisho wa Ndugu hao Unaanza kwenye Mathayo 13:55-56
Nitakuandikia kiyunani (Greek) as the original language....

"
Οὐχ οὗτός ἐστιν ὁ τοῦ τέκτονος υἱός; οὐχ ἡ μήτηρ αὐτοῦ λέγεται Μαρία καὶ οἱ ἀδελφοὶ αὐτοῦ Ἰάκωβος καὶ Ἰωσὴφ καὶ Σίμων καὶ Ἰούδας; καὶ αἱ ἀδελφαὶ αὐτοῦ οὐχὶ πᾶσαι πρὸς ἡμᾶς εἰσιν; πόθεν οὖν τούτῳ ταῦτα πάντα;

Na hivi ndivyo hutamkwa...

Ouch houtos estin ho tou tektonos huios? ouch he meter autou legetai Maria kai hoi adelphoi autou Iakobos kai Ioseph kai Simon kai Ioudas? kai hai adelphai autou ouchi pasai pros hēmas eisin? pothen oun touto panta?

Kwa mama Samia tungeandika hivi..

Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?
Na dada zake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote?


neno lililotumika kama Ndugu(Kaka ) ni ἀδελφοὶ" (adelphoi) na Mara zote hutumiwa kwa Ndugu wa Damu yaani wale wa Tumbo moja...
kwa case yako kuwa Huenda lilitumika kama Ndugu wa Dada ake Mama yake..
neno ambalo lingetumika nafikiri lingekuwa ανηψιός (anepsiós)

Sasa kama utaweza bado swali liko pale pale walikuwa watoto wa nani!
 

Kristo ndio muhimu kumfahamu mkuu maana yeye ndiye aliyetuletea injili na wokovu, hao ndugu wengine ni 'minor characters' tu.
 
Yesu ndio wa muhimu mkuu na in

Kristo ndio muhimu kumfahamu mkuu maana yeye ndiye aliyetuletea injili, hao ndugu wengine ni 'minor characters' tu.
Naelewa vizuri sana mkuu na ndo maana kila siku huwa nasema hili swala..
Tusome sana Biblia tulizonazo..
Na kama wewe ni Mu-islam soma sana Quran..
Na muhindu soma sana ulichonacho...
Na sio tu Kusoma Jikite kusoma kwa Textual Critiq (Textual analysis) ili ujue muktadha wa Maandiko Usifate sana Tafsiri maana kuna vitu wanaficha sana...

Kwa mfano watu Uliowataja Hao wanaoitwa Mariam..
Ukisoma Vibaya utakuta kuna Mariam zaidi ya 7...
Mariam cleopa,Mariam magda,Mariam mamaye ,Mariamu salome etc..lakini kuna siri kati ya hao..

Eniwei ni vyema kudeal na Injili kama ulivyosema
 
Neno la mungu halibadiliki? Sawa.

Waamuzi 1:19​

Mwenyezi-Mungu alikuwa pamoja na watu wa kabila la Yuda, nao wakaiteka nchi ya milima. Lakini hawakuweza kuwashinda wenyeji wa nchi tambarare kwa sababu magari yao ya vita yalikuwa ya Chuma.

Mathayo 19:26​

Yesu akawatazama, akasema, “Kwa binadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote huwezekana.”

Tuendelee kuonyesha contradiction zilizopo kwenye hekaya za kiyahudi?
 
Mkuu ziko nyingi sana ninao uwezo wa kuonyesha 100
 
Jidanganye. Ukishamjua? Si bora uhangaike kujua ukoo wako. Yeye kumjua itakusaidia nini labda? Hivi,ni nani kwanza? Ulijuaje aliwahi kuwepo?
 
Mkuu ziko nyingi sana ninao uwezo wa kuonyesha 100

Yaani huwa nashangaa omnipotent, omniscient na omnipresent anashindwa vipi kwa madai ya kwamba wenyeji walikuwa na magari ya chuma.

Hivi mkuu huwa inasababishwa na nn mtu anaona kabisa contradiction lakini anagoma anaamua kuufyata na kujitoa akili. Ukihoji unaambiwa unafanya blasphemy.
 
Ni tatizo la brainwashed tu mkuu na mt7 kujazwa kuamini kila kitu japo moyoni anajua kabisa hapa ni uongo ila anajikaza tu...

Kwa mfano story ya kazaliwa kwa yesu (inawezekana kweli alizaliwa) ila stiry yake imajaa vitu visivyp halisia na ukoo usio wa ukweli majina ya babu na bibi yasiyo kuwepo
 
Unaweza kuwa sahihi kusema Mungu ni WA wote, walevi wazinzi nk nk.

Wote ni wake sababu aliwaumba na kuwapa Pumzi Bure.

Ikiwa tayari mmeoana na hamjaokoka, au mmoja ana TABIA zisofaa, maombi yanaweza kumbadikisha akawa MWEMA mkavumiliana na maisha yakasonga.

Ninachoongelea ktk mada, ni NDOA Takatifu sawasawa na maandiko.

Kwamba NDOA ni takatifu, ya mme na mke mmoja, vijana watunze Bikra zao na waepuke zinaa kabla ya Kuoa,

Wamuulize Mungu kupitia Maombi, awape mtu sahihi Kutoka Kwa MUNGU.

Ubarikiwe, Amen.
 
Ninachouliza hawa watu wenye miaka nane na hakuna ndoa na watoto wawili walimuuliza mungu?
 

Mimi naonaga ni matatizo ya akili mkuu,
Yaani mtu unaaminishwa kiasi cha kuvaa mpaka mabomu na kujitoa uhai.

Kuna dada jirani akisikia unamsema t.b joshua lazima mgombane na anakuambia anafufua watu na huna kitu utamwambia akakuelewa😃
 
KATIBA kuu kuliko Katiba zote ni Neno la Mungu.

Inasema NDOA ni ya mke na mume mmoja.

Ikiwa hutaki Kuoa, ussizini Wala kununua MAKAHABA, Wala usijichue.

Amen
 
Mimi naonaga ni matatizo ya akili mkuu,
Yaani mtu unaaminishwa kiasi cha kuvaa mpaka mabomu na kujitoa uhai.

Kuna dada jirani akisikia unamsema t.b joshua lazima mgombane na anakuambia anafufua watu na huna kitu utamwambia akakuelewa😃
😅😅😅🤣🤣
Gwajima mwenyewe anafufua ila alipofariki mama yake alilia mpaka kuzmia Ila hakumfufua...
🤣🤣
 
KATIBA kuu kuliko Katiba zote ni Neno la Mungu.

Inasema NDOA ni ya mke na mume mmoja.

Ikiwa hutaki Kuoa, ussizini Wala kununua MAKAHABA, Wala usijichue.

Amen
Katazo la kujichua limeandikwa wapi kwenye biblia?
 
Uongo na utapeli wa hizo dini.... Wanawake wanapaswa kuolewa wawili wawili na zaidi.

Hayo makanisa na vitabu vyake vya uongo khs ndoa wana ajenda zao khs ndoa na wanawake kw ujumla. Ndio maana wanapinga nakuaminisha watu mke n 1 tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…