Je, wajua nini hutokea katika Ulimwengu wa Roho wawili wanapoungana katika NDOA Takatifu?

Hakuna ndoa wanaishi tu na miaka nane imetimia na watoto wawili hawa walijazwa roho mtakatifu?
Huo ni UZINZI,

Katika Roho kufanya kitendo tu tayari mmeungana, ila muunganiko huo ni kinyume na mapenzi ya Mungu.

Kama mume ana mke zaidi ya mmoja, Inatakiwa aamue kubariki NDOA na mke mmoja kati ya hao, akusanye watoto wote wa mama wengine aliozaa nao na avunje mahusiano yote na wanawake wengine na atunze family ya mke mmoja na mume mmoja.

Amen
 
Joseph alikua ni mume Wa wake zaidí ya mmoja Kwa mujibu Wa historia ya vitabu Vya kale na masimulizi.
Hivyo Yesu alikua na ndugu upande Wa baba. Ila Kwa Mariam alikua peke yake .
Na hakuwahi kuingiliwa na mwanadamu MAISHA yake yote.
Ni mtakatifu sana . Wabadai mpaka vyakula alivyokua anakula vilikua vinaletwa na Malaika.
Joseph alikua ni mume mlezi tuu. Na alikua na wake wengine kama Mila Zao na Ilikua ni halali kuoa wake wengi
 
Maandiko Yako wazi, Mariam alizaa watoto wa kiume na WA kike na Yusuph. Na Yesu aliwachagua baadhi ya ndugu zake kuwa wanafunzi wake.

Vyakula special vya kuletwa na Malaika hayo ni maelezo Yako yasiyoandikwa kwenye BIBLIA.
 
Basi shetan kaupiga mwingi sana
Shetani hajui maana ya NDOA.

Yeye ni mpinzani wa SHERIA za Mungu siku zote.

Mungu akiagiza watu wake,

Shetani huja na compaign ya kataa NDOA.

Wa Mungu tutamtii na kumsikiza Mungu siku zote.

Amen
 
Mkuu 😅😅 nakuelewa sana na kwa bahati mbaya ulichosema sio msingi wa Dini unayoamini Ni msingi wa Mila za kiKatolick ambao unaenda mpaka kwenye Council of Ephesus mwaka 431 AD..

Ambao ndo walianzisha Dogma na mila inayoitwa "Theotokos" katika Kanisa...
Maana yake ni Kumsafisha maria na kuwa Mama wa Mungu ...
Maana hakuingiliwa mpaka anakufa....

Sasa huko tupaache nataka tutoke kwenye misingi ya kidini wala misingi yoyote ya ukweli uliopo wala y watoto..

Natka twende kwenge mantiki na logic..

Kuna mwanaume unayemjua ambaye atamlipia Mahari mwanamke Na atakaa naye miaka yote zaidi ya 20 bila kumuingilia (Na zingatia mwanamume ni Rijali)...

Unacholeta ni Wazo la kwenye aprokrifa moja inayoelezea kuhusu uchungu wa maria wakunga waliomzalisha na Jinsi alivyokuwa Bikra na alivyoendelea kuwa bikra baada ya kujifungu...

Narudia Tena Someni Sana ili mtoke gereza la akili
 
Hapana hawakuwa na undugu na Yesu wa namna hiyo Yohana na Yakobo walikuwa ni ndugu kwa kuwa walikuwa watoto wa Mamkubwa wake Yesu, Mama wa Yesu alikuwa mamdogo wao.Kama unaongelea wale wanafunzi ambao ni watoto wa Zebedayo(Marko 3:17) ila kama unaongelea Yakobo,Yuda, Simoni na Yose na mabinti kadhaa ambao majina hayajaandikwa hao ndo walikuwa ndugu wa Yesu kwa kuzaliwa(marko 6:3)
 

Attachments

  • 20231121_114813.jpg
    129.3 KB · Views: 3
  • 20231121_114849.jpg
    178.3 KB · Views: 1
Mbona hata kwenye biblia kuna siku Maria alikuja na nduguze kumuona yesu aliozaa na joseph
 
Huwa napenda nisirudie sana maelezo kma unaweza rudi post namba 103 (comments # 103)
Halafu leta hoja kulingana na comments hiyo
 
Ndyo hiyo naifahamu mkuu Tatizo watu hawaelewi wamefumbwa kwenye Theotokos
Afu wanataka lazimisha kuwa Joseph alikuwa mcha mungu kiasi cha kuishi na mwanamke bila kumla mtu alikuwa seremala wanasema kwa enzi hizo ni tajiri
Ibrahim baba wa imani alishindwa vumilia akagonga nje atakuwa joseph
 
Huwa napenda nisirudie sana maelezo kma unaweza rudi post namba 103 (comments # 103)
Halafu leta hoja kulingana na comments hiyo
Nimekupata vizuri na ahsante kwa kile ulichokisemea kwa kina.. mimi nilireply kutoka na post namba 59
 
Ila kwa leo kuhusu Kuhamasisha Ndoa Rabbon Hongera sana kaka..

Mhubiri 4:9-12
[9]Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja;
Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.
.
[10]Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!

[11]Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?

[12]Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.
 
Mmmh hapa umetupiga uongo. Mungu alisemaje? Ebu soma maelekezo yko vzr
 
Huo ndo UKWELI,

Ukipata mke sahihi mkaelewana, hatua zote kimaisha, kimaendeleo, kiimani huenda Kwa haraka sana.

Mbaya ni Kuoa mtu asiye sahihi, unaweza kudhani NDOA zote ni shida, kumbe wapi!!

Wengine wanaenjoy maisha ya NDOA,
 
Unamlisha maneno mwenyezi. Yeye alisema Tuijaze dunia. Habari za kuoa zililetwa na Paulo kwenye waraka wake wa kwanza kwa wakorintho.
 
Unamlisha maneno mwenyezi. Yeye alisema Tuijaze dunia. Habari za kuoa zililetwa na Paulo kwenye waraka wake wa kwanza kwa wakorintho.
Yesu ndo alipigilia msumari,

Petro usimsingizie.
 

Sasa unasema vipi lazima kuwepo mungu watu wawe wamemuuliza roho mtakatifu?
Wakati wapo watu kibao hawajaoana na wana miaka mingi kwenye mahusiano.
 
Sasa unasema vipi lazima kuwepo mungu watu wawe wamemuuliza roho mtakatifu?
Wakati wapo watu kibao hawajaoana na wana miaka mingi kwenye mahusiano.
Naongelea ambao hawajaoa Bado.

Waliopo kwenye NDOA wakabariki NDOA zao na maisha yaendelee,

Mbona hizo ni minor issues unaraise?
 
Naongelea ambao hawajaoa Bado.

Waliopo kwenye NDOA wakabariki NDOA zao na maisha yaendelee,

Mbona hizo ni minor issues unaraise?

Unakubaliana na mm mahusiano au ndoa si lazima umpachike huyo mungu ili yawe mazuri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…