Je, wajua? - Special Thread

Kweli aisee na population Africa ipo kwa nchi 6
Nigeria 179M
Ethiopia 108 M
Egypt 99M
DRC. 80 M
Tanzania 58M
South Africa 51 M

Kwingine mapori tuu
 
India unaiacha wapi ambayo inaipiku china muda si mrefu,
 
Humo wachina diaspora wapo?
 

Mende ni mdudu asiyeweza kuamla akilalia mgongo

Paka ni mnyama asiyeweza kuangukia mgongo

Sijui sisi binadamu tuna nini cha kushangaza ... labda siasa chafu!!! 😂 🤣
 
Je wajua kuwa ndege jamii ya Cuckoo hutaga mayai yao kwenye viota vya ndege wengine?

Ndege jamii ya Cuckoo hutaga mayai yao kwenye viota vya ndege wengine (hasa jamii ya dunnocks, meadow pipits & reed warbles) na kuacha mayai yao yaanguliwe na ndege wengine na vifaranga kulishwa na ndege wamiliki wa viota.
 
Aisee!
 
Je wajua mnyama aina ya Kenge mvua ikinyesha akiwa nchi kavu haraka huikimbia mvua na kukimbilia majini kama maji yako karibu kama hayako karibu anajificha mvua isimpate? kwanini?
Sababu alivyoumbwa maji ya mvua yanabadilisha haraka sana mfumo wake wa pressure ya mwili osmotic pressure kwasababu maji ya mvua hayana madini yeyote hivyo anakimbilia haraka majini maana angalau majini kuna madini yanayoweza kuweka mfumo wake wa osmotic pressure sawa au angalau akijificha hiyo shida haijitokezi.
Sio kwamba watu wanadhani ni ujinga wake kukimbia maji ya mvua na kukimbilia kwenye dimbwi kuna sayansi ndani yake.
 
Je wajua vifo vingi Mahospitalini vinasababishwa na uzembe wa Madaktari
 
Jewajua..

→✏ Nyanya ndo tunda Maarufu zaidi Duniani. Ndizi sio tunda ni mtishamba{Herbs}.
→✏ Kila Bara linaishia na Herufi iliyoanza nayo mwanzo, mfano: Africa, Europe, Asia.. [Kwa Kingereza lakini]
→✏ Maji huwa hayaexpire, expire date ni ya Chupa.
→✏ Asali ndo Chakula Pekee Kisichoharibika.
→✏ Unaweza kupunguza Uchachu wa embe kwa Kuliloweka dakika 10 kwenye Maji ya Uvuguvugu.
→✏ 96% ya Mishumaa hununuliwa na Wanawake.
→✏ Uking’oa kucha zote za vidole vya mkono, itakuchukua miezi 6 Mpaka ziote na Zikomae tena.
→✏ Kuna Radi takribani 2,000 kwa kila dakika Duniani.
→✏ Gesi haina Harufu, bali harufu huwekwa ili Kutaarifu kama Gesi ikivuja.
→✏ Katika Alfabeti zote, herufi ‘e’ ndo hutumika Zaidi.
→✏ Mabegi ya kuburuta Matairi yalianza Kutumika tangu 1971.
→✏ Watoto wadogo chini ya miezi 3, hawawezi kutetemeka kwa baridi.
→✏ Duniani kuna wastani wa Watu 6 ambao Unafanana nao kila Kitu kasoro Jina tu, na una 9% ya Kukutana nao!
→✏ Mahusiano mengi Duniani huzaliwa siku ya Jumatano.
→✏ 97%ya watu wakipewa Kalamu Mpya, basi wataijaribu ubora wake kwa kuandika Majina yao ama kuweka alama ya Sahihi.
→✏ Ukiwa unaandika namba zako za Siri, ukahisi Umekosea hata moja huwa Unafuta Zote na kuanza Upya.
→✏ 3% ya watu wote Duniani ni Mapacha. *Mapacha wanaweza Kuwa na Baba tofauti.
→✏ Watoto 255 huzaliwa kila dakika, taarifa: UNICEF.
→✏ Kama Umezaliwa 1999, Basi jua Umeishi ndani ya Miongo 3, Karne 2 na Millennium 2.
→✏ Kujinyonga India, kumeua Watu wengi Kuliko Ukijumulisha ajari na magonjwa kwa Pamoja
→✏ Pweza ana Bongo 9, Mioyo 3 na damu ya bluu. Maziwa ya Kiboko ni ya Pink.
→✏ Huwezi kupiga Chafya bila kufumba Macho.
→✏ Ukidownload file “PDF” inayoishia na ‘exe’ ifute io ni Virus.
→✏ 74% ya Watumiaji wa facebook huiangalia Kila siku, Mtu mmoja hutumia angalau dk 35 kwa Siku.
→✏ Video Billion 8 Hutazamwa fb kila Siku. Marekani ina idadi kubwa ya watumiaji fb. fb profile feki Duniani zinakadiliwa Kufika Million 270.
→✏ Account Million 391 za twitter hazina follower. Watu million 500 hutembelea Twitter kila mwezi bila kulog in.
→✏ Kombe la Dunia lilianzishwa rasmi 1930,Uruguay akiwa Mdhamini, na ndo aliyechukua Kombe kwa Mara ya kwanza.
→✏ Sehemu nyeupe ya Kucha yako inaitwa ‘lunula’.
→✏ Kama jicho lingekua Camera lingekua na MegaPixel [576MP].
→✏ Mende ana Uwezo wa Kuishi kwa Wiki kadhaa akiwa hana Kichwa.
→✏ Ukihesabu kwa Maneno ya kingereza 1-1,000 hutopata herufi ‘a’. Mpaka ufike 0ne thous‘a’nd ndo utaipata.
→✏ Kwa Siku, ni Bora Ukulala Mara mbili kwa Masaa 4, kuliko Kulala Masaa 8 kwa Pamoja.🙏

Wako Emmanuel Kasomi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…