KAMPUNI 7 KUBWA DUNIANI AMBAZO ZINA MAJINA HALISI YA WAANZILISHI WAKE.
1JBL.-ni kampuni ya kimarekani inayojihusisha na utengenezaji wa audio speakers na loud speakers.Kampuni hii ilianzishwa mnamo miaka ya 1946 miaka 76 iliyopita chini ya muanzilishi bwana "James Bullough Lansing huko Los Angeles USA.
2.Mercedes-Benz -jina Mercedes Benz lilitokea mnamo mwaka 1926 kutoka kwa Daimler Benz.Mercedes Benz ni gari la kwanza la petroli lililotengenezwa na Karl Benz benz patent motorwagen, kutokana na ufadhili wa berths benz na kupewa hatimilikiJanuari 1886. Gari hili liliuzwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1901 na kampuni ya Daimler.Makao makuu ya kampuni yanapatikana stuttgart Baden wurttemberg German.
3.Ford -wengi tunaifahamu kampuni hii kwa umahili wa utengenezaji magari kama aina ya ford ranger, na mengineyo sasa huyu hapa mwanzilishi ni-:Henry Fordalizaliwa julai 30,1863.Alikuwa muhandisi na mfanyabiashara nchini marekani Alianza kutengeneza magari mwaka 1896 akaunda kampuni ya Ford motor Company mjini Detroit.Gari la kwanza lililotengenezwa kwa idadi kubwa ilikuwa modeli ya Ford T akajenga milioni 15 Ford T.
4.Lamborghini-hii nadhani wengi wetu tunaijua Automobile Lamborghini ni kiwanda cha italia ambacho ni watengenezaji wa magari ya kifahari, magari ya michezo, na SUVs, kinachopatikana Sant'Agata Bolognese, Italia.Mwanzilishi na mmiliki wa hii kampuni anaitwa bwana Ferruccio Lamborghini alizaliwa munamo 28 April 1916.
5.Suzuki - hili jina pia najua si geni machoni na maskioni mwako.Mwanzilishi wa hii kampuni ni Michio Suzuki.ilianzishwa mnamo mwaka 1909 huko Hamamatsu, Shizuoka Japan kampuni hii pia ipo dunia nzima yani worldwide.
6.Siemens - hakuna asiejua kampuni hii kwa ubora na umahiri wake juu ya utengenezaji wake wa simu za mkoni kwanzia miaka hiyoo hadi sasa.ilianzishwa 1 October 1847 huko Munich na Berlin Germany.chini ya muasisi wake bwana:FounderWerner von Siemens kampuni hii ipo worldwide kila mahali.
7.Honda - kama hujawahi kuendesha magari yake basi naimani piki piki zake umeendesha ilianzishwa mwaka 1948 mwanzilishi chini ya muasisi wake mzee; Soichiro Honda.Alizaliwa 17 novemba 1902 huko Hamamatsu, Shizuoka, Japan.
Zipo nyingi zaidi sitoweza kuziolodhesha zote kama unazifahamu zaidi ongezea kwa faida ya wengi.