Je, wajua? - Special Thread

Je, wajua? - Special Thread

Nchini korea kuna aina ya kifungo kinaitwa "THREE GENERATION " Yaani kifungo cha vizazi vitatu.
.
.
Vizazi vitatu ni kuanzia wewe hadi wajukuu zako.
.
Kwahyo Mtu aliyefanya kosa hupelekwa jela na familia yake na hukaa huko hadi kizazi cha 3 ndo wanaachiwa huru.
.
.
Chanzo cha habari hii hakijaeleza aina ya makosa yenye adhabu hiyo.

Source: BlowingFacts.org

NAWASILISHAView attachment 1544194

Sent using Jamii Forums mobile app
Korea ipi??

North or South?
 
KUMBUKUMBU MUHIMU SIKU KAMA YA LEO KWA MECHI DUME YA SIMBA SPORTS CLUB

Simba Sports Club kama Club kongwe nchini na barani Africa yenye kusheheni mambo mengi sana ni lazima kuwepo na vitu muhimu kama kumbukumbu ambayo haiwezi kuondoka kwenye Wanachama, mashabiki na Wapenzi wa Club ya Simba.

Miongoni mwa mambo mengi ila leo nitakuletea Kumbukumbu moja muhimu sana ya mechi iliyochezwa kipindi hiki ambayo ni historia nzuri sana.

KUMBUKUMBU HIYO

Kombe la CAF wakati huo ilikuwa linachezwa kwa mara ya 3 chini ya ufadhili au udhamini wa aliekuwa mfanyabiashara maarufu nchini Nigeria kipindi hicho aliitwa Moshood Abiola, Tanzania ikawakilishwa na Simba kwa mara ya kwanza.

Ilikuwa ni 18 September 1993 Miaka 17 iliyopita Simba Sports Club iliweza kutinga Nusu Fainal ya Kombe ya CAF baada ya kucheza mechi ya Robo Fainal siku hii na kufungwa 2 kwa bila na USM EL HARRACH mechi ilichezwa jijini Algiers nchini Algeria, hii ikiwa ni mechi ya marudiano huku ya kwanza ikiwa Dsm 05 September 1993 Uwanja wa Uhuru Simba ilishinda Goli 3 kwa 0 magoli ya Simba yakifungwa na Abdul Machine, Edward Chumila na Malota Soma.
Ikumbukwe kuwa kabla ya mechi hii ya Robo Fainal Simba Sports Club iliweka kambi nje ya bara la Africa Jijini NICE - FRANCE.

MECHI DUME YA NUSU FAINAL KIDOGO

Hii ndio ilikuwa moja ya mechi Dume ya Simba Sports Club maana timu iliyokutana nayo ilikuwa ni kifaa hatari sana na ilikuwa kwenye moto wa hatari sana.
ATLETICO SPORTS AVIACAO ya Angola ilikuwa ndio mpinzani wa Simba hawa Walikuwa wanaume wa ukweli.
Mechi ya Kwanza ilichezwa Dsm 17 October 1993 na hapa Simba ndio waliendeleza historia ya NYUMBANI HATOKI MTU kwa kumpiga kama amesimama 3 kwa mtungi hawa Atletico Sports Aviacao baada ya mechi walisema hawaamini matokeo haya kabisa kwani Simba imewashangaza sana hatakaa kusahau hawajawahi muda mrefu kufungwa popote TATU MZUKA KAVU na cha kuvutia zaidi Goli zote 3 kapiga Mwanaume mmoja EDWARD CHUMILA akaondoka na mpira wake.

Mechi ya marudiano ilifanyika Mjini Luanda Angola 31 October 1993 na timu zote kutoka 0 kwa 0 na kuipa Simba nafasi ya kwenda Fainal ya Kombe la CAF ni bonge ya historia ambayo haijakutwa wa kufikiwa mpaka sasa hivyo ni mwiko kufutika kwenye vichwa vya wana Simba.

KIKOSI CHA KAZI ZOTE HIZI 1993 KILIUNDWA NA HAWA

Kocha ni Abdala King Kibaden akisaidiwa na Ettene Eshente huyu alikuwa ni MuEthiopia.
Magolikipa walikuwa Mohamed Mwameja, Mackenzie Ramadhan na Often Martin alietokea timu ya Ushirika ya Moshi.

Wachezaji wa Ndani walikuwa Twaha Hamidu, Fikiri Magoso, Suleiman Pembe, Kasongo Athumani, Godwin Aswile, George Masatu na Deo Mkuki akitokea timu ya Pamba ya Mwanza.

Wengine walikuwa George Lucas, Ramadhan Lenny, Iddy Selemani, Hussein Marsha, Abuu Omari, Joachim Masumbuko na Dua bin Said Akitokea Small Simba ya Zanzibar.

Inaendelea kwa Damian Kimti, Nico Kiondo, Michael Paul, Thomas Kipese, Abdul Ramadhan Machine na hawa David Mihambo na Mbuyi Nyondani wakitokea Reli ya Morogoro.

Kikosi kilimalizika kwa hawa Malota Soma, Edward Chumila, Rashid Abdallah Magongo, Bakari Iddy, Razak Yusuph Careca toka Coastal Union, Feruzi Telu toka Milambo ya Tabora.

MTORI ULIANZA KULIWA TOKA ZAMANI KILICHOBADILIKA NI STYLE TOFAUTI TOFAUTI ZA MAPISHI
 
ATLETICO SPORTS AVIACAO ya Angola ilikuwa ndio mpinzani wa Simba hawa Walikuwa wanaume wa ukweli.
Mechi ya Kwanza ilichezwa Dsm 17 October 1993 na hapa Simba ndio waliendeleza historia ya NYUMBANI HATOKI MTU kwa kumpiga kama amesimama 3 kwa mtungi hawa Atletico Sports Aviacao baada ya mechi walisema hawaamini matokeo haya kabisa kwani Simba imewashangaza sana hatakaa kusahau hawajawahi muda mrefu kufungwa popote TATU MZUKA KAVU na cha kuvutia zaidi Goli zote 3 kapiga Mwanaume mmoja EDWARD CHUMILA akaondoka na mpira wake.
Hii timu ilijiita kwa kifupi ASA, ilikuwa hatari sana, na ilitoka kuwatoa Canon Yaounde ya Cameroon kisha Gor Mahia ya Kenya kabla haijakutana na Simba, na kote huko hadi inaingia nusu fainali ilikuwa haijaruhusu goli hata moja ndani ya dakika 90, hivyo waliduwaa sana kuona wanafungwa matatu hapa (ila nikusahihishe kidogo, first leg ilikuwa 3-1 na sio 3-0). Timu ilikuwa na golikipa mahiri kabisa wa viwango kama vya Mwameja, aliitwa Kanka Vemba, alikuwa hafungiki kirahisi. Wachezaji wengine ni winga hatari kabisa mzaliwa wa DRC, Libengue ambaye alipambana vilivyo na Kasongo Athumani mwenye bangi zake kichwani. Wengine ni Arlindo, Abilio, Kuleka, Nando na wengine nimewasahau
 
#UNAAMBIWA: Binadamu aina ya Mwanaume huwageukia Wanawake 10 kwa siku na kutamani muonekano wao, kwa wastani anatumia DK 43 kwa siku kuwakodolea macho Wanawake, hii ni sawa na kusema kwa wastani katika maisha ya Mwanaume anatumia mwaka mzima kuwageukia Wanawake tofauti.

Hii ni kwa mujibu wa Mark Ireland ambaye pia anasisitiza kuwa sio Wanaume pekee wanaomiza shingo zao kwani Wanawake huwageukia Wanaume 6 kwa kutumia dakika 20 kwa siku ambayo ni wastani wa miezi 6 ya maisha yake yote.

Kwa uzoefu wako kibongobongo Mwanaume anageuzia shingo Wanawake wangapi kwa siku? wastani wa muda gani kwa maisha yake yote ? 😀🤔
 
JUA HILI
Idadi ya raia wa China ni 1,437,268,056 na idadi ya bara lote la Afrika ni 1,340,598,140
Kwahyo utofauti wake na China inazidi bara lote la Afrika watu takribani 96,668,961
Hii inamanisha watu wote wa Afrika wanaweza ishi China na Watu wa China wakiishi wote Africa watakuwa wengi zaidi.
 
JUA HILI
Idadi ya raia wa China ni 1,437,268,056 na idadi ya bara lote la Afrika ni 1,340,598,140
Kwahyo utofauti wake na China inazidi bara lote la Afrika watu takribani 96,668,961
Hii inamanisha watu wote wa Afrika wanaweza ishi China na Watu wa China wakiishi wote Africa watakua wengi zaidi.
Hii ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka gani mku??
 
Back
Top Bottom