Je, wajua Tanzania inaongoza kwa nguvu za kijeshi Afrika Mashariki na kati?

Je, wajua Tanzania inaongoza kwa nguvu za kijeshi Afrika Mashariki na kati?

Kuna mtu mwenye bajeti ya ulinzi/ masuala ya kijeshi ya Tanzania?
 
Kwa taarifa yako hakuna nchi afrika inapokea vifaa na mafunzo ya mabilioni ya dola kwa wingi kutoka marekani kama Misri..hivyo sio ajabu.After all Nigeria imekuwa na uchumi wa kwanza afrika mwaka jana tu..soon wata take over kwasababu wana nguvu ya kiuchumi
asante kwa kuelewa uhusiano kati ya nchi kuongoza kiuchumi na nyingine ikaongoza kijeshi.
 
Mtoa mada haya uliyoyaeleza hapa ni SIRI za Taifa. Kabla hujapost kitu tafakari.
 
Mtoa mada haya uliyoyaeleza hapa ni SIRI za Taifa. Kabla hujapost kitu tafakari.
siri ipi mkuu? onesha kilicho siri, tukijadili. ndege ya kisasa ya pekee waliyoonyesha taifa mwaka jana na zingine na magari na vifaa vya kijeshi walivionyesha kwa kunguru au kwa binadamu? waonyeshe hadharani mbele ya Watanzania na mbele ya wageni na mabalozi, wewe bado unaita siri!, woga wa namna hii utadumaza hata namna yetu ya kufikiri. ilichosema jeshi au kukionyesha au kuruhusu kionyeshwe ni sawa kukijadili hasa kizalendo. mkuu na wengine mkoje? mbona hata wajeda wanapohitimu MONDULI, Media hualikwa?
 
Wewe ni mtu binafsi kuzungumzia maswala ya kijeshi ni budi uwe umepewa mamlaka au idhini ya kufanya hivyo.

Vifaa vile vilionyeshwa hadharani kwa idhini ya Amiri Jeshi mwenye mamlaka ya kufanya hivyo. Ukipewa ushauri ufanyie kazi.
 
kwa idhini hiyohiyo ya Amiri jeshi mkuu kuonyesha vifaa na zana hadharani automatically vinazungumzika hadi humu. kama ni kesi wapewe waliongeza hoja za kizushi au uchochezi ila mimi kwa uzi huu na michango yangu naeleza kitu cha kweli na ambacho sio siri tena. unasema nini juu ya MEDIA zikizoandika, kuzungumzia na kuonyesha vifaa hivyo? mbona watu waliingia taifa na simu na camera na jeshi halikukataza? jamani narudia tena tuache woga usio na tija. nadhani wasio wazalendo na nchi yetu wanatumia lugha ya kunitisha nisiipaishe nchi yangu pale inapoweza kufanya vzr.naomba kama kuna mtu wa SYSTEM u MI na anahisi nakosea basi awatumie MODS wa JF au njia nyingine nitakayowatambua ili nisimame ktk kutetea hoja zangu.asante mkuu
 
mkuu acha woga usio na tija. penda kusoma uzi vizuri na kufanya kautafiti kidogo juu ya kilichopo uzini. siri ipi imeanikwa kutoka ndani ya JWTZ? nimetaja vitu ambavyo jeshi lenyewe limesema au kuvionyesha. hivi ndugu yangu pale uwanja wa taifa kwa mfano ndege za kivita, vifaru na magari ya kijeshi na maelezo yanatolewa na watu wanasikia wanarekodi kwa audio na video na zimewekwa mitandaoni. hata mapigano ya jeshi la Kenya na Al-Shabaab watu wanaona zana zinazotumika. we bado unasema siri.
Sawa mkuu
 
asante kwa kuelewa uhusiano kati ya nchi kuongoza kiuchumi na nyingine ikaongoza kijeshi.
Fuatilia kuanzia miaka ya tisini mpaka juzi wakati wa vurugu,misri ilikuwa inaongoza kiuchumi,sioni kwanini wasiongoze kijeshi wakati miaka yote walikuwa wanaongoza kiuchumi,kuvurugika kiuchumi miaka miwili haina maana walikuwa vibaya.
 
labda kwa mfano huo inakuwia vigumu kuelewa. sasa nakualika ufuatilie orodha ya nchi zinazoongoza kiuchumi duniani uone kama orodha hiyo ndivyo ilivyo kwa nguvu za kijeshi. mkuu tambua hilo.
 
Inatusaidia nini Kwenye hii njaa!
faida za nguvu za kijeshi za nchi yetu:
1. wazawa na wawekezaji kuwa na uhakika kuwa taifa lina nguvu za kutosha kulinda maslahi yake na ya wananchi wote na hivyo kupata uwekezaji zaidi
2. nchi kupanga mipango yake kwa uhakika ikiwa na matumaini makubwa ya kuwa salama
3. uhakika wa kulinda watu na rasilimali zake
 
hapa umejibu hoja ipi ndugu, ili tuone eneo la kuongeza bidii. ni vema umnukuu mtu kisha utoe hoja zako.
Hii hapa na bidii kwa maana ya kujizatiti kikamilifu kuilinda ardhi yetu...
TANZANIA ikawa ngome ya jeshi la ardhi na hivyo ikaongoza kuwa na vifaa vingi vya ardhini mf. vifaru, magari mbalimbali ya kivita na mizinga.
 
tuko pamoja mkuu
 
Back
Top Bottom