Hivi nyie watu,hilo mmeliona la ajabu sana.Ulishawahi fuatilia upuuzi unaofanywa nchi za wenzetu.
Nashangaa sana mtanzania ambaye huwa anakashfu vitu vizuri vinavyofanyika kuhusu nchi,hii ni sawa na kujikataa wewe mwenyewe na kusifia vya mwenzako,ili hali uwezo unao wa kurekebisha chako kikafanana au hata kuzidi cha mwenzako.
Shida yetu kubwa ni watu wamekosa uzalendo wa kutetea au kupigania nchi yao.Watu wapo tayari na kujisikia fahari kusifia vya nchi zingine kama vile huko kwingine ni peponi na pana kuhusu.
Mleta mada nilichomuelewa anasifia uwezo wa jeshi letu na anajisikia fahari kwa nchi yake kuwa na jeshi lenye uwezo,hata kama anajua au hajui kwa undani utajiri wa jeshi letu, lakini ndiyo jeshi lake,lazima ajivunie.
Sipendi kuamini nyie mnaembeza mleta mada na kudharau uwezo wa jeshi letu kuwa nyie ni wenzetu,inawezekana mkawa ni wa mataifa mengine,maana humu JF kuna wachangiaji na waleta mada toka nchi mbalmbali.
Nitoe Rai kwa watanzania kwamba tuipende nchi yetu,Maana hata hizo nchi zinazosifiwa maendeleo hayakushushwa na mungu kama zawadi bali ni watu wenye nchi husika ambao waliongozwa na roho za uzalendo.Ahsante mungu kwa kuniumba kuwa MTANZANIA.