“Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” — Mwanzo 1:1
- Mwanzo — Muda (Time)
- Mbingu — Nafasi (Space)
- Nchi — Maada (Matter)
Kwa maneno machache, mstari huu unaonyesha mwanzo wa vipengele vitatu vya msingi vya ulimwengu: muda, nafasi na maada. Vipengele hivi vinategemeana; maada haiwezi kuwepo bila nafasi, na matukio katika ulimwengu hayawezi kueleweka bila muda.
Kwa hiyo, Muumba wa muda, nafasi na maada hawezi kuwa amefungwa ndani ya vitu alivyoviumba. Ni lazima awe nje ya muda, asiyewekewa mipaka na nafasi, na asiyeumbwa kwa maada.
Hapo ndipo tunapomwona Mungu kama
Muumba wa vyote, lakini Yeye mwenyewe hakuumbwa (Uncreated creator, uncaused Causer etc).