GE2025 Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine wasipige kura?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine kupiga kura?

  • Wana haki kuzuia wengine kupiga kura

  • Hawana haki kuzuia wengine kupiga kura

  • Sijui

  • Sijali


Results are only viewable after voting.
Mfano wako ni logical non sequitur fallacy kwa sababu suala la collaborators South Africa halikuwa na utata mkubwa.

Ilikuwa vigumu sana kwa mweusi kusema ana support ubaguzi wa rangi kufalsafa tu, yeye si collaborator.

Suala hilo Tanzania lina utata mkubwa.

Mtu anaweza kusema yeye ana support CCM kifalsafa tu, si collaborator. Anaamini CCM inapitia a rough patch itajirekebisha na kwenye wapinzani hakuna uongozi bora kama inaoweza kuoat8kana CCM.

Huo ni msimamo w akifalsafa, ana haki ya kuwa na msimamo huo.

Mtu anaweza kusema ha support CCM yeye ana support chama cha upinzani na anaona upinzani unahitaji viti hata vichache bungeni kuichemsha CCM.

Huyo si collaborator wa CCM. Hiyo ni mpinzani.

Sasa mtu anayetaka upinzani uwepo bungeni kuichemsha CCM utamuitaje collaborator wa CCM?

Mfano wako ni logical non sequitur fallacy.

Unalinganisha vitu visivyolinganishika.

Kwa nini unajiona wewe ndiye mwenye monopoly ya ukweli na wengine wote wakiwa tofauti na wewe hawana haki?

Kwa nini inakuwa vigumu kukubali kuwa demokrasia inakutaka ujenge ushawishi, ukishindwa kujenga ushawishi watu wengine wana haki ya kuamua wanavyotaka bila kujali maamuzi yao ni sahihi au si sahihi?

After all, demokrasia si ni pa.oja na uhuru wa kufanya maamuzi yasiyo sahihi?

Au demokrasia ni lazima mtu afanye maamuzi sahihi, akikosea inakuwa si demokrasia?

Je, demokrasia inatoa haki ya watu kukosea?
 
"Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine wasipige kura?". This is a moot question and you can't make it hypothetical or abstract because we already have empirical evidence that there's not a significant number of the so called "wanaharakati" who are actively preventing other Tanzanians from voting on October 29th. The very premise of the question is essentially false; and, therefore, the post is not worth a serious discussion.
 
Bunge la chama kimoja bongo haliwezi kuwajibika kwa raia hivyo halina maana yoyote zaidi ya kufuja tu pesa za walipa kodi hata akiwepo huyo mbunge wa mmoja Zitto wa maonyesho haibadilishi chochote kwa sababu halipatikani kwa ridhaa halisi ya raia walio wengi hivyo halitawajibika kwao kwa vyovyote vile na hii ni sababu mojawapo muhimu sana ya kupinga huu uchaguzi wa kiini macho wa maonyesho.
 
Kwanza sio sahihi kusema wanaharakati, kanisa katoliki na wengine wanaoipinga uchaguzi wanataka upinzani bungeni au urais, wanachotaka ni uchaguzi huru na wa haki unaosimamiwa na tume huru, kama CCM itashinda katika mazingira hayo yanayofuta mchakato wa haki na uwazi kwao ni sawa tu hata CCM ikishinda kwa 100%
 
Wewe unaonaje kikatiba ni sahihi , huu ni uchaguzi? Kujua au kutokujia ni hali ya MTU BINAFSI kwani taifa Lina katiba na vyama pia je wewe unaona katiba HIZO zimezingatiwa? Kama lah ! MANAKE wanaopiga WAKO sahihi hatakama wapo wasiopinga YAANI wanakubaliana na uchaguzi ambao katiba yao haikufatwa kivipi ILI iweje?
 
Sawa.

Lakini wewe ndiye unayeona hivyo, wengine wanaona ni bora kuwa na sauti hata ndogo kuliko kukosa sauti kabisa.

Sasa wewe ni nani mpaka uwaamulie wasipate hiyo sauti ndogo wanayoitaka wao wasipige kura kabisa?

Wewe usiyetaka kupiga kura wakikulazimisha upige kura kwa sababu wao wanataka mbunge angalau mmoja utafurahi?
 
You are missing the point.

Call them what you want.

Swali ni.

Je, ni sahihi kwa kundi moja, kundi A, kulikataza kundi lingine, kundi B, kuliambia lisipige kura, kulinyima nafasi ya kupiga kura, kwa sababu kundi A libaona ucjaguzi hauna haki, ikiwa kundi hilo B linataka kupiga kura?
 
Wewe unazunguma kama vile watu wanaopinga uchaguzi hawataki uchaguzi jambo ambalo sio kweli, wata wanapinga "uchaguzi huu" ila wako tayari kushiriki uchaguzi mwingine utakaoandaliwa katika misingi sahihi iliyo huru na haki, kwa hiyo hao wanaopiga kura watapiga kura tu, labda kwa kuchelewa kidogo kwa miezi kadhaa au mwake mmoja ila ndani ya muda mfupi wataipata hiyo haki yao unayoitetea hapa. Kwa upande mwingine wanaopinga wakiruhusu uchaguzi huu ufanyike au ukifanyika ina maana wana miaka mitano tena au zaidi ya kusubiri kama angalau wataweza kupata bahati tena ya kupata uchaguzi huru.
 
libaona ucjaguzi hauna haki, ikiwa kundi hilo B linataka kupiga kura
Sio linaona ni sahihi unaposema linaona MANAKE ni mtazamo TU.


Ila kiuhalisia sio mtazamo kundi linalotaka kupiga kura ni la wajinga au wapumbavu najua unaelewa tafsiri ya hayo mawiki je utakubali mwanafamilia mwenzio alete shida nyumbani KISA ujinga wake wakati UNAWEZA kuzuia. Na jambo linaloweza kukuathiri wewe pia.
 
Ku invoke katiba ni ku invoke an argument from authority logical fallacy.

Kwa sababu uchaguzi unaweza kuwa sahihi kikatiba halafu katiba yenyewe ikawa haina haki.

Kwa hiyo hoja nzima ya "kikatiba ni sahihi?" ni hoja mufilisi, imejengwa katika appeal to authority logical fallacy.

Makaburu wa Afrika Kusini walitawala kwa sheria na katiba, lakini sheria zao na katiba zilikuwa dhalimu.

Kwa hivyo, ondoa hoja ya "kikatiba ni sahihi" kwa sababu ni hoja isiyo na mashiko.

Katiba yenyewe watu wengi wanaisema ni mbaya, inampa mamlaka makubwa rais, ina matatizo mengi, sasa kwa nini unataka kuifanya kigezo?
 
Mzee wetu sasa uwekewe uangalizi maana unakoelekea siko kabisa.

Umevamia Uzi kuja Kubariki katiba mnayoidharau Hadi ikifika siku za uchaguzi.

Ok, jadili Mada Kama ilivyo mezani huko kudanganywa hakuhusiki hapa.
 
W Watoto ni wenye umri usiofika miaka 18, hao hawahusiki na siasa sasa wazazi wawakanye kwa lipi ilihali hata siasa hawafanyi
 
Subiri muda ukifika tutajua.
 
Ikiwa wanasema ni mbaya wabadili kabla yakuendelea na uchaguzi ni nchi gani isiyoongozwa na katiba na wewe usipinge katiba wakati hujabadili katiba hatuongozwi Kwa hisia na uhuru tunaongozwa na katiba iliyopo AMBAYO ILI isifanye kazi ni lazima ibadilishwe na kwakuwa haijabadilishwa ina ina haki ya kufuatwa unazungumza democracy wakati unazuia haki ya katiba kufanya maamuzi? Kwa kusema haina mashiko kwahiyo WATU wavunje Sheria ?, ukivunja Sheria KUNA WATU unawaumiza hiyo ni democracy? Nambie huu uchaguzi uko sahihi ?

Unapenda complicate mambo RAHISI we mwanafalsafa mtanzania kazi unayo.
 
Subiri muda ukifika tutajua.
Hili si suala la kujulikana kwa kusubiri muda tu.

Kwa sababu unaweza kusubiri mpaka ukafa na kusitokee lolote la kukujuza.

Hili ni suala la kifalsafa na kidhahania la kuchunguzwa na kujadiliwa.

Matokeo ya uchaguzi njia moja au nyingine hayajibu swali hili.

Hakuna guarantee yoyote kwamba kusubiri tutapata jibu la swali hiki.

Unajuaje tukisubiri tutajua?
 

Wenye imani majibu yapo.
 
Kama hata hiyo katiba mbaya ingekuwa inazingatiwa kwa wagombea wa upinzani kutoenguliwa, watu kutopotezwa, msajili kutovuruga vyama vya upinzani na kukichukulia CCM kama vingine na kesi za ubunge na udiwani za wapinzani kuendeshwa kwa haki mahakamani tusingefika hapa. Tumefika hapa kwa sababu hata hiyo katiba mbovu yenyewe haizingatiwi katika ubovu wake.
 
Hiyo sauti ndogo wanayoitaka hao watu wa vyama shikizi ndio itatumika kama rungu la kuendelea kukwamisha demokrasia ya kweli na haki ya watu kuchagua kwa sababu kila mara itakapoibuliwa hoja ya demokrasia na uchaguzi huru itasemwa tayari kuna uchaguzi huru na demokrasia ndio maana hata Zitto na wingine wawili au watatu wa CHAUMMA wameshinda wametangazwa na wako bungeni. Hiyo ndio utakuwa turufu ya MaCCM ku gaslight watu ndani na nje ya nchi wanaotaka demokrasia na utawala bora.
 
,
KAULI za watu kama heche kwa muda tofauti tofauti kuhusu kutofanyika kwa uchaguzi na kuzuia uchaguzi ni kauli za hatari sana na kwa muda huu walitakiwa wawe wameshatiwa nguvuni na kuwekwa jela kwa kuwa wanachochea vurugu na uvunjifu wa katiba...
Nyie katiba hamjavunja? Kuteka na kuua watu katiba inaruhusu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…