Msengapavi
JF-Expert Member
- Oct 23, 2008
- 8,919
- 7,772
Okay nadhani hili linatupeleka kujadili conflicting rightsMkuu,
Suala la haki ni nini ni pana sana na mara zote huwa tunatumia approximation, crude versions, agreements, etc.
Yani ni hivi, ukitaka kufuatilia haki pasu pasu always kuna room kwamba uchaguzi haukufuata haki.
In fact kifalsafa haki is a Selassian illusion, to be pursued, but never attained.
Yani unaweza kuhoji mpaka kwa nini baba yako kakuzaa wewe na wewe hujamzaa yeye, hiyo si haki.
Unaweza kusema kwamba kwa miaka yote iliyotawala CCM hata wafanye nini, hata wajiondoe kumchagua mwenyekiti wa tume, hata walete katiba mpya ya kumpunguzia rais madaraka, hata wakiue chama na kuwaachia wapinzani tu uchaguzi, ukitaka kusema uchaguzi haukuwa wa haki kwa sababu ya utawala wa CCM unaweza kujenga case hiyo, kimantiki kabisa. Kwa sababu ya legacy ya CCM. Yani hata ukiwaondoa ma CCM wote wasishiriki uchaguzi hiyo nayo itakuwa si haki.
Point ya msingi hapa, ambayo watu wengi wana i miss, ni discussion ya individuals rights.
Kama watu wameamua kushiriki katika uchaguzi, bila kujali huo uchaguzi ni wa haki au si wa haki (this is not the discussion, the discussion is about if wanaharakati wana haki ya kuwalazimisha wengine wasipige kura).
Wanaharakati wana haki ya kuwaingilia wanaotaka kupiga kura katika haki yao hiyo ya kushiriki katika uchaguzi?
Kama wanayo hii haki, maana yake kundi moja linaweza kulazimisha kundi jingine lifanye tofauti na linavyotaka.
Hili lina maana gani kwa wanaharakati?
Hawaoni kuwa hili linafungua mlango kwa wanaharakati nao kulazimishwa wapige kura katika uchaguzi wasioutambua?
I am more interested in the abstract philosophical points than the concrete politics of Tanzanian elections which many people seem to focus on.
Hapana hujawazuia bali umezuia zoezi zima.Mfano.
Ukipiga mabomu kituo cha uchaguzi, kisiweze kutumika kupiga kura, ukisema utapiga mabomu watu watakaojitokeza kupiga kura, unaweza kuwa umewalazimisha watu wanaotaka kupiga kura wasipige kura.
Huelewi wapi hapo.
Haki ni neno pana sana, lenye mizizi katika nafsi na akili za watu. Kila mtu ana tafsiri yake ya haki, kulingana na alichopitia, alichonyimwa au alichotendewa. Ndiyo maana ni vigumu kuhukumu kwa urahisi ni nani yuko sahihi na nani amekosea, kwa sababu katika macho ya kila mmoja, haki yake ina sura ya kipekee.Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine wasipige kura?
Tuna siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025. Uchaguzi huu umegubikwa lindi la kukosa uhalali pengine kuliko uchaguzi mwingine wowote Tanzania.
Hata mgombea wa CCM ameshutumiwa na mpaka kufunguliwa kesi kuwa kajipitisha bila kufuata utaratibu.
CHADEMA imesusia uchaguzi. Mgombea wa ACT Wazalendo kazuiwa kushiriki, ingawa kuna wanaosema kafanya makosa mwenyewe. Wagombea wengi, hata ndani ya CCM wamekatwa bila sababu za kueleweka.
Kuna watu wengi wanalalamika kuwa uchaguzi hauna uhalali, tume ya uchaguzi inachaguliwa mwenyekiti na rais anayegombea urais pia katika uchaguzi, na matatizo mengine mengi ya kikatiba na kiuendeshaji.
Hivyo, wanaharakati wengi wanataka kuandamana siku ya uchaguzi tarehe 29 October. Hiyo ni haki yao ya kikatiba.
Lakini, wengine wanakwenda mbali zaidi, wanataka kufanya civil disobedience kuzuia wengine wasifanye uchaguzi. Hawa si tu wanataka kuandamana, bali pia wanataka kuzuia uchaguzi hata kwa kutumia fujo na nguvu.
Wanasema huu si uchaguzi, ni uchafuzi, ni maigizo, ni figisu tupu. Hivyo, wana haki ya kuuvuruga usifanyike.
Lakini, kuna watu wameamua kushiriki kwenye uchaguzi huu. Kwa kujua na kukubali huu si uchaguzi ni uchafuzi, au kwa kutokujua na hata kukataa habari hiyo inayopinga uhalali wa uchaguzi.
Na wao wanasema wana haki yao kushiriki uchaguzi huo, na wana haki ya kufanya uamuzi binafsi kwamba uchaguzi huu ni halali au si halali, waachwe waitumie haki yao. Demokrasia si kulazimishana, ni watu wote kupata uhuru wa kufanya maamuzi wanayoona ni sahihi.
Hili ni swali muhimu na gumu kifalsafa.
Kuna wanaharakati wanasema wana haki ya kuvuruga uchaguzi usio halali.
Kuna wapiga kura wanasema haki yao ya kuamua kupiga kura iheshimiwe.
Haki hizi mbili zinaonekana kugongana.
Tunapitaje hapa kwa usalama bila kuvunjia kundi moja la wanaharakati haki yao ya civil disobedience kuvuruga uchaguzi, lakini pia tusiwavunjie watu walioamua kupiga kura?
Na kama hatuwezi ku maintain haki zote, haki ipi inaipiku nyingine? Kwa sababu gani?
Naomba mazungumzo ya kidhahania zaidi, yajikite kwenye sababu za kifalsafa Zaidi, kimantiki, kuliko kuwa na mjadala wa kisasa wenye hisia zaidi.
Hizo points zote nazielewa na binafsi nazikubali.Kama hata hiyo katiba mbaya ingekuwa inazingatiwa kwa wagombea wa upinzani kutoenguliwa, watu kutopotezwa, msajili kutovuruga vyama vya upinzani na kukichukulia CCM kama vingine na kesi za ubunge na udiwani za wapinzani kuendeshwa kwa haki mahakamani tusingefika hapa. Tumefika hapa kwa sababu hata hiyo katiba mbovu yenyewe haizingatiwi katika ubovu wake.
It doesn't matter unavyoona wewe.Hiyo sauti ndogo wanayoitaka hao watu wa vyama shikizi ndio itatumika kama rungu la kuendelea kukwamisha demokrasia ya kweli na haki ya watu kuchagua kwa sababu kila mara itakapoibuliwa hoja ya demokrasia na uchaguzi huru itasemwa tayari kuna uchaguzi huru na demokrasia ndio maana hata Zitto na wingine wawili au watatu wa CHAUMMA wameshinda wametangazwa na wako bungeni. Hiyo ndio utakuwa turufu ya MaCCM ku gaslight watu ndani na nje ya nchi wanaotaka demokrasia na utawala bora.
Hii ni hoja kimbilio kwa watu wavivu na wajinga wasioweza kujadili hoja kifalsafa na kidhahania.
Okay nadhani hili linatupeleka kujadili conflicting rights
Kwasababu maandamano ni haki, na anayepiga kura anatekeleza haki, sasa haki hizi mbili zinazo kinzana zikitaka kukutana ni haki ipi ambayo itapaswa kupewa uzito zaidi?
Katika situation hii nadhani tuipime kwa kuangalia ni haki ipi ina uzito zaidi kwa maslahi ya wengi.
Nitumie mfano wa Corona, Katika janga hili la afya, haki ya mtu kutembea bila barakoa inaweza kuzuiwa kwa maslahi ya afya ya jamii.
Ikiwa uchaguzi unahatarisha mustakabali wa taifa, basi kuzuia uchaguzi huo kwa maandamano ya amani inaweza kuwa tendo la kulinda haki ya wengi.
Ni kweli nakubaliana na wewe kuwa wakati wa janga la Corona, baadhi ya hatua zilizochukuliwa zilionekana kuwa na msingi wa kisayansi, lakini baadaye zilitiliwa shaka.Suala la Corona halikuwa argumentative what is right and what was wrong. This was a matter of public health, science. The science was thought to be clear (even as we later found out it wasn't so clear).
In fact suala la Corona ni mfano m,uri wa kutufundisha kusikikiza sauti za watu ambao hatukubaliani nao. Kwa sababu wanasayansi wamekuja kuona kuwa kuna restrictions fulani zilizowekwa wakati ule hazikuwa na ulazima wala msingi wa kisayansi.
So, tunaona hata pale tunapofikiri mambo yapo clearcut, kisayansi, mambo hayako clearcut hivyo.
Suala hili la uchaguzi si sayansi, lipo argumentative. Wanaokataa kupiga kura wanasema wako right, wanaotaka kupiga kura wanasema wako right. Hili ni suala la demokrasia si sayansi, hivyo huwezi kusema kwa uhakika wa kisayansi.
Dhana ya "maslahi ya wengi", which is basically utilitarianism, hqpa inakwama, kwa sababu kuna suala la individual rights na demokrasia. Demokrasia inaangalia mpaka minority rights kwa hivyo uchache au wingi hausababishi mtu akose kabisa sauti katika demokrasia.
Ndiyo maana katika demikrasia kuna msemo wa "majority rulrle, minority rights".
Kwa hiyo ukiwanyima watu, hata kama ni wachache, haki yao ya kuoiga kura, ume violate minority rights.
Ukiambiwa leo uuawe kwa maslahi ya wengi, utakubali kuuawa? Kwa nini uuawe wewe?
Pia, dhana nzima kwamba kutopiga kura kunabeba maslahi ya wengi ni dhana yako wewe.
Yule anayetaka kupiga kura pengine naye anaona kupiga kura kunabeba maslahi ya wengi. So this is also argumentative, opinion based and unclear.
Hoja si maandamano. Maandamano tushakubali ni haki ya kikatiba na kibinadamu.
Mimi sioni mjadala kwenye maandamano.
Hoja ni wanaharakati kuzuia watu kupiga kura.
Ni sawa au si sawa?
Umeelewa tofauti?
Kama mfumo ni danganyifu, na watu wengi wa fungu A wameona hivyo, watu wengi hao hawahitaji kuwanyima watu wa kundi B wanaotaka kupiga kura haki yao ya kupiga kura ili kuondoa mfumo danganyifu.Ni kweli nakubaliana na wewe kuwa wakati wa janga la Corona, baadhi ya hatua zilizochukuliwa zilionekana kuwa na msingi wa kisayansi, lakini baadaye zilitiliwa shaka.
Lengo la mfano huo ilikuwa sio kuifanya sayansi ionekane ni kamilifu “clearcut”, bali kwamba katika mazingira ya hatari ya kiafya, jamii inaweza kukubaliana kwa pamoja kuweka mipaka kwa baadhi ya haki binafsi kwa ajili ya kulinda uhai wa wengi.
Hii ndio pointi ya msingi ambayo niliijenga nikibainisha kuwa katika mzingira uncertainty jamii huweza kuamua kwa ujumla kuweka uzito zaidi kwenye haki fulani (kama ya kuishi) kuliko nyingine nikimaanisha sio kila haki ina uzito sawa.
Binafsi naamini haki zinatofautiana uzito. Ndiyo maana katika historia, kuna mambo mengi yaliyowahi kuonekana kama haki, lakini leo hii tunayatambua kama dhuluma.
Naamini kila kilichoitwa haki back then kingesimamiwa hivyo hivyo kama kilivyo sidhani kama hata huu uhuru tulionao leo tungeupata. Huu uhuru umekuja baada ya watu kuanza ku question yale yaliyosemekana kuwa ni haki katika miaka hiyo.
Umesema ukweli kuwa demokrasia inalinda haki za wachache, huo ni ukweli. Lakini swali ni je haki ya mtu mmoja kupiga kura katika mfumo wa kidanganyifu inapaswa kulindwa zaidi kuliko haki ya wengi kudai mfumo wa haki?
Binafsi naamini haki ya mtu mmoja kupiga kura haipaswi kuwa kisingizio cha kuendeleza mfumo dhalimu. Kama mfumo mzima ni wa kitapeli, usio na usawa, unalenga kukibeba chama tawala wa kifisadi, au wa kidikteta, basi kushiriki humo ni sawa na kuidhinisha udhalimu kwa jina la haki.
Mkuu,..vipi kuhusu wanaotaka kutiki kuwazuia wasiotaka kutiki kuandamana?
Mkuu,Kifalsafa, haki ya kupinga ni muhimu kwa uadilifu wa jamii, lakini inapovuka mpaka na kuzuia wengine kutumia haki zao, inajinyima uhalali.
Uhuru wa kupinga hauwezi kuwa juu ya uhuru wa kuchagua ,maana demokrasia huishi tu pale panapokuwepo nafasi ya wote kufanya maamuzi yao binafsi bila kulazimishwa.
Ikiwa kama hoja unayojaribu kuijenga ni kuangalia haki na kutaka haki hiyo itendeke hata kama ni dhidi ya wachache, dhidi ya ukweli nk.Kama mfumo ni danganyifu, na watu wengi wa fungu A wameona hivyo, watu wengi hao hawahitaji kuwanyima watu wa kundi B wanaotaka kupiga kura haki yao ya kupiga kura ili kuondoa mfumo danganyifu.
Kwa sababu watu wengi wa kundi A hao wanaweza kuwaacha hao wanaotaka kupiga kura, hao wa kundi B, halafu hao wa kundi A wakaiondoa serikali isiyo na uhalali kwa maandamano.
Kama huutambui uchaguzi, kwa nini unawanyima watu kupiga kura? Unawanyima watu nafasi ya kupiga kura kwenye nini wakati huutambui uchaguzi?
Huoni kuwa ukishaanza kuwanyima watu kupiga kura tu, kwa namna fulani, umeutambua kuwa huu ni uchaguzi?
Waachie wapige kura, wewe jipange kivingine uiondoe serikali.
Wa Romania hawakukataza mtu kupiga kura.
Walifanya popular uprising wakamkamata Rais Ceausescu, wakampiga risasi December 25 1989.
Hawakumkataza mtu kupiga kura.
Waliwapiga risasi Nicolae Ceausescu na mkewe siku ya Christmas 1989.
Wakaondokana na utawala dhalimu.
Huhitaji kumvunjia mtu haki yake ya kupiga kura ili wewe utimize haki yako ya kuondokana na utawala dhalimu.
Hapana,Ikiwa kama hoja unayojaribu kuijenga ni kuangalia haki na kutaka haki hiyo itendeke hata kama ni dhidi ya wachache, dhidi ya ukweli nk.
Basi kama ndio hivyo tutapofikia tunaweza kusema pia kuwa endapo mgombea A akipata kura nyingi dhidi ya mgombea B, hapaswi kutangazwa mshindi kwasababu tutakuwa tumevuruga haki ya wapiga kura wachache waliomchagua mgombea B.
Ila kama tunaweza kupuuza hao wachache na kwenda na wengi kwa kupima uzito wa haki katika misingi ya demokrasia ya kweli, uwazi, sheria zenye kutoa fairness kwa kila mgombea basi utakubaliana na mimi kuwa sio kila inayoitwa haki lazima itekelezwe bali kupitia kanuni za kweli zinazo thibitisha uhalali wa hiyo haki.
Mimi nachokiona hapa niMkuu,
Umeiweka vizuri, kwa maneno rahisi na machache.
Mawazo yako yanashabihiana kabisa na yangu.
Najaribu kuwaelewa wasioukubali uchaguzi wanaotaka kuzuia wengine kupiga kura, kwa sababu naelewa dhana ya civil disobedience kifalsafa.
Lakini na mimi nimefikia hitimisho kama lako kwamba haki ya anayeukataa uchaguzi haitakiwi kuiminya haki ya anayeukubali uchaguzi.
Kwa sababu hata kupiga kura katika uchaguzi usio halali ni haki ya kidemokrasia. Demokrasia si haki ya kufanya maamuzi sahihi tu, ni haki ya kufanya maamuzi hata yasiyo sahihi.
Zaidi ya yote, suala la nani yupo sahihi na nani hayupo sahihi ni argumentative, kila mtu anamuona mwenzake hayupo sahihi, kidemokrasia kila mtu ana haki sawa.