Je, wanasiasa wa Kanda ya Ziwa wanahujumiwa?

Je, wanasiasa wa Kanda ya Ziwa wanahujumiwa?

Wangekuwa wananizidi wasingeenda kutetemekea ajira za kujipendekeza. Mbona Mimi kwangu Niko vizuri kiasi sioni haja ya kujipendekeza kwa yoyote?
Uzuri Jukwaa hill hata vilaza wenye account fake full kujitutumua! Wewe Kubali tu hao sio level zako!!
 
Uzuri Jukwaa hill hata vilaza wenye account fake full kujitutumua! Wewe Kubali tu hao sio level zako!!
Ni kweli sio level yangu, maana wao wanaweza kujipendekeza ili wapate maisha, lakini Mimi sitamani hata.
 
Unajua kuna watu wanaojiona first Class full kujitutumua!
Kwani kujiona First class na kujitutumua ni kosa kisheria?
Maisha hayana mbabe wake na kila jamii Inapambana kivyake!
Upo sahihi kila jamii ipambane kwa njia inazozijua.
Kuna mchungaji wao Kimaro alikuja Mwanza akaanza kusifia watu wa Mwanza mara anataja Wahaya wana akili sana mara Wakerewe wanamaprofesa na ndo maana Mwanza ni sehemu nzuri!
Hakudiriki kutaja wasukuma maana ndo threat yao kubwa
Kweli wewe ni mtu wa ajabu .. kichwa cha mada yako ni hiki !

Je, wanasiasa wa Kanda ya Ziwa wanahujumiwa?​

Hapa umeishia kuja na mada ndani ya mada kutaka kutuaminisha kuwa Kanda ya Ziwa ni ya wasukuma na wahaya au makabila nyingine si sehemu ya kanda ya ziwa.

Kama huyo mchungaji Kimaro Mchagga hajawasifia Wasukumu na kuwapa sifa Wahaya au Wakerewe huo ni uhuru wake na mtazamo wake.

Kimaro na wewe @sambungulu hamna tofauti kwa sababu kila mmoja anatoa maoni na mtazamo wake na hakuna kabila lililowatuma mkawasemee, hata wewe hapo hakuna Msukuma aliyekutuma kuja kuwasemee hapa JF.
Mda wao Ulishaisha na bila kuwa na?mzizi kanda ya Ziwa chama Chao Watasubiri sana!
Kama huo muda wewe Msukuma ulianzisha na kuamini kuwa bila kanda ya ziwa hakuna kitakachoenda basi sawa.
 
Kwanini wanasiasa kutoka kanda ya ziwa wanashambuliwa sana kwenye mitandao ya kijamii. Je, kuna chuki dhidi yao au kuna agenda maalumu asitokee mwanasiasa mwenye nguvu kutawala siasa kanda ya ziwa kama wanavyofanya Zitto Kabwe kule Kigoma, Freeman Mbowe kanda ya kaskazini au alivyokuwa marehemu Maalim Seif alivyokuwa anatawala siasa za Zanzibar?

Au kuna agenda maalum ya baadhi ya wanasiasa kuitumia kanda ya ziwa kwa manufaa yao ya kisiasa kwa kuwaathiri wanasiasa wanaotokea kanda ya ziwa?

Kwasababu tumeona alivyoteuliwa Dotto Biteko kuwa naibu waziri mkuu na waziri wa Nishati na Paulo Makonda kuwa mwenezi wa CCM kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na nyuzi mbalimbali za kuwashambulia na wanaofanya kazi hiyo ni wale wale waliotumika kushambulia utawala wa hayati Rais Magufuri kwa viongozi walioteuliwa kutoka kanda ya ziwa.

Ukiangalia mitandao ya kijamii kama X(tweeter) asilimia kubwa za nyuzi zinazofunguliwa ni vita dhidi ya wanasiasa wa kanda ya ziwa sio Makonda na Dotto pekee bali wanasiasa wote wanatokea kanda ya ziwa wanaoonekana wana nguvu fulani ya kisiasa.

Ndio maana nauliza kuna ajenda mahususi kwa ajili ya kuwadhoofisha wanasiasa wanaotokea kanda ya ziwa?

Kwanini wanasiasa wanatokea kanda ya ziwa ndio wanaonekana wabaya?
Na watu wanaotumika ni wale wale wanajificha kwenye kichaka cha kutetea demokrasia lakini ukifuatilia kwa makini nyuzi zao zitawahusu wanasiasa wa kanda ya ziwa kuwadhoofisha kisiasa wasipate nguvu.
Ni wivu tu unawasumbua pia lake zone inaonekana kuwa tushio kwenye medalii za kisiasa, kwa sasa
 
Halagu tofautusha Kanda ya Ziwa na Usukumani. Kanda ya Ziwa ni kubwa Sana. Itoe Mara na Kagera kwenye huyo ujinga wenu
 
Punguzeni chuki na ubinafsi dhidi ya jamii fulani hata humu watu walio comment negative wote ni wachaga, chuki hazitawasaidia.

Wewe na mleta mada mpunguze chuki. Baadala mseme Usukumani mnajumuisha Kanda ya zima yote kwenye ujinga wenu.
 
Halagu tofautusha Kanda ya Ziwa na Usukumani. Kanda ya Ziwa ni kubwa Sana. Itoe Mara na Kagera kwenye huyo ujinga wenu
Nyinyi mara na kagera mi manority! Kwa mpole! Na huku kanda ya ziwa wanaume ni wasukuma na Wakurya kisiasa na kiuchumi!
 
Ni wivu tu unawasumbua pia lake zone inaonekana kuwa tushio kwenye medalii za kisiasa, kwa sasa

Mmerudi na ukanda wa Ziwa. Mbona kwenye uchaguzi ilibidi muibe kura?. Kama Kanda ya Ziwa ndio tegemeo lenu?. Mnaongea vitu ambavyo sio halisia. Kwenye maukabila yenu iondoeni mara na Bukoba.
 
Wezi,wazulumati na vibaka wa taifa katika ubora wenu, Cha ajabu mna tukana kina ngosha huku mmejificha nyuma ya keyboard
Hao mnao watukana pengine wamewazidi Kila kitu katika maisha
Nyie ni vinara wa kutukana huku mmejificha
 
Mmerudi na ukanda wa Ziwa. Mbona kwenye uchaguzi ilibidi muibe kura?. Kama Kanda ya Ziwa ndio tegemeo lenu?. Mnaongea vitu ambavyo sio halisia. Kwenye maukabila yenu iondoeni mara na Bukoba.
Hivi wewe uko na ubongo kweli? Ukizungumza kanda ya ziwa unaongelea Wasukuma kwanza hao Kagera na Mara hawana ushawishi wa kubena kanda ya ziwa!
 
Nyinyi mara na kagera mi manority! Kwa mpole! Na huku kanda ya ziwa wanaume ni wasukuma na Wakurya kisiasa na kiuchumi!

Minority ndio ujinga gani?. Kama mna agenda ya ukabila pelekeni Usukumani huko. Na ni nani kasema Mara na Kagera ni minority?. Ondooeni ukabila wenu huko.
 
Hata wakipiga kelele ,kanda ya ziwa haizuiliki
Kanda ya ziwa ni sawasawa na maji. Usipoyaoga utayanywa tu na hata kuyanawa. Ni wengi mno na bila kupata kura zao huwezi kutoboa. Ndiyo maana mama anahangaika japo kwa Biteko sidhani kama itamsaidia maana jamaa hana bashasha (charisma) kabisa. Afadhali hata angempa Dr. Kalemani au Luhaga Mpina....

Nilikuwa Lamadi juzi Makonda alipopita. Kulikuwa na atmosphere sawa na ile ya enzi za Magufuli na watu wanaonekana kumkubali.

Hao wa mtandaoni we usiwajali maana siyo wapiga kura. Wapiga kura wapo huku vijijini....
 
Tanzania ni moja na watanzania ni ndugu.
Muasisi na mjenzi wa hali hii ni mtu wa kanda ya ziwa (Baba wa taifa).
Watanzania wote walimkubali na wanamkubali hadi leo kwa sababu ya hoja zake zilizotokana na fikra zenye mantiki za kuwaunganisha watanzania na waafrika kwa ujumla kwa ukombozi wao.
Mwalimu Nyerere alikuwa na uono mpana, zaidi ya kabila, kanda na taifa.
Changamoto ya wanasiasa wa leo ni kwamba fikra zao ni zile za kijima za ukabila na ukanda ambazo muasisi wa taifa alizivuka miaka hiyo. Fikra hizi ni hatari sana kwani zaweza kutumiwa na maadui wa nje kuturudisha kwenye utumwa na ukoloni (mamboleo).
Mijadala mingi sasa hivi ni mapambano ya jamii na viongozi kuhusu kukubali utumwa na ukoloni mamboleo.
Utaratibu wa wagawanye uwatawale unatumika indirectly na watu wa kanda ya ziwa ni muhimu kufanikisha Hilo.
 
Wezi,wazulumati na vibaka wa taifa katika ubora wenu, Cha ajabu mna tukana kina ngosha huku mmejificha nyuma ya keyboard
Hao mnao watukana pengine wamewazidi Kila kitu katika maisha
Nyie ni vinara wa kutukana huku mmejificha

Bora wewe umeenda moja kwa moja kwenye kabila. Sio hao wajinga wanajumuisha Kanda ya Ziwa yote kana kwamba wote ni wasukuma. Acheni hizo.
 
Mmerudi na ukanda wa Ziwa. Mbona kwenye uchaguzi ilibidi muibe kura?. Kama Kanda ya Ziwa ndio tegemeo lenu?. Mnaongea vitu ambavyo sio halisia. Kwenye maukabila yenu iondoeni mara na Bukoba.
Kuna kabila hapo umeona limetanjwa?
 
Hivi wewe uko na ubongo kweli? Ukizungumza kanda ya ziwa unaongelea Wasukuma kwanza hao Kagera na Mara hawana ushawishi wa kubena kanda ya ziwa!

Wewe ndio huna akili na punguani. Kwa hivyo kwa Sasa Kanda zinatambulika kwa makabila na sio mikoa. Eti mara na Kagera hatutambuliki. Zamani Kanda ya Ziwa ilikuwa Mwanza, Kagera na Mara. Baadae wakaleta shinyanga, Simiyu na Geita. Halagu wewe mkabila usiye na haya unadai mikoa ya Mara na Kagera haina Ushawishi?. Punguzeni dharau na haya mambo ya Kenya msiyalete huku Tanzania.
 
Hii mijamaa mijinga kweli. Inapenda kutaja Kanda ya Ziwa ikimanisha Usukumani, halafu kwa dharau wanadhani wataiburuza Mara na Kagera kwenye ujinga wao. Mtu anasema Mara na Kagera hamna ushawishi kwenye Kanda ya Ziwa make kimya. Very stupid.
 
Back
Top Bottom