lukubuzo Samsis
JF-Expert Member
- Nov 3, 2014
- 2,947
- 3,466
umesoma geography?population?Shalom wana jamvi!
Nimetafakari mwenyewe naona kama majibu hayakuji, au kuna maandiko pengine yanasema mwanaume atakufa mapema kuliko mwanamke? Kuna wengine nimepata kusikia wanasema eti mwanaume akipiga bao moja anapoteza dakika 3 za kuishi na wanasema hiyo ni kisayansi naamini humu wanasayansi wapo wengi watanitoa tongo tongo.
Ukitazama katika jamii wanawake waliofiwa na waume zao ni wengi kuliko wanaume waliofiwa na wake zao, hiyo imekuwa kama kawaida hivi hata wanawake katika kusisitiza waume zao kuwekeza katika assets huwa wanatumia msemo wa "Baba chanja kuna Leo na kesho usijetuacha tukawa tunateseka". Sasa hebu tuambiane ni kisayansi, kimaandiko au ni mazingira yanapelekea mwanaume anakufa mapema kuliko Mwanamke????
Karibuni kwa hoja
Sawa kumbe wanaume sio mashine tu wanaume kazi eeeeMajambazi wengi ni wanaume na wanakufa katika kazi yao,wafungwa wengi ni wanaume wanafia magerezani,wanaume wengi wanafanya kazi hatarishii
Hiyo sio sababu Jombaaa kuna wengine wameoa wanawake walio wazidi umri bado mwanaume anatanguliaSio kweli jinsia watu wanakufa ila kwa kua wanaume huoa wanawake wadogo hivyo tunatangulia kabla ya wake zetu. Zaidi ya 95% ya wanaume waliooa wamewazidi umri wake zao. Unakuta mtu kamzidi mke wake miaka 10 mpka 20 af akitangulia tuseme kawahi kufa sababu ni mwanaume?
Wewe unasemajee? Mambo wengine yanaonekana dhahiri kwenye jamii, kwa mfano mim Babu zangu sijawakuta ila Bibi zangu wote nimewakutainasemekana.....lakini hakuna tafiti ya kitaalamu iliyodhibitisha.....
Geography ndio inafafanua kwanini wanaume wanatangulia kufa kuliko wanawake?, hiyo population kipengele gani sasa population change, density, au distribution? Sijaona wapi panaeleza sababu za wanaume kutangulia kufa kuliko wanawake, labd wewe uliyesoma tusaidieumesoma geography?population?
Bado haija justify hoja yako kwamba ukioa mwanamke akiyekuzid umri itapelekea ufe mapemaHii ni kwa wanandoa wanaofariki wakiwa umri umeenda Mara nyingi kama mama ana 65-70yr jua Mme ana 80-90yr sasa hapo ujue miaka ikienda maradhi yanaongezeka hivyo Obviously tu mwaume atawahi kufa tu!!
Mkuu umeliongelea vizuri sana, mwanaume anaweza kuhangaika kutafuta mali lakini mwisho wa siku ni kwa ajili ya kumridhisha mkewe au mpenzi wake, na kuhangaikia familia yake na ndugu kwa ujumla. Wakati mwingine anatumia nguvu nyingi za mwili na akili kwa ajili hiyo. Ikitokea amesalitiwa na mpenzi wake kwa namna yoyote ile, hasa kwa hawa mabinti wa siku hizi waliokaa kimaslahi zaidi huwa inamuumiza sana na hii unaweza kuta inachangia kwa kiasi kikubwa katika matatizo ya maradhi ya moyo na vifo vya mapema vinavyowakuta. Cha muhimu ni kumwomba Mungu atuepusha na mambo kama hayoWanaume changamoto nying ni za ASILI! Na kwa hali hio hio ya ASILI tumekuwa watumwa wa Wake zetu tukidhani tunawaridhisha. Si ajabu mwanamke akiona hatari anakuita ukabiliane nayo na ukishoindwa dharau zinaanza. Hapa ndipo shida ilipo.
Wengi humu tunaweza kuwa tulishakutana na mdada amepata break down kwa mfano ya gari na kapaki pembeni hana hata wasiwasi na ukitokea unaanza mwenye "may I assist you?' Matokeo yake huwa tunatesa miili yetu na hata kuiingiza katika vihatarishi tukiwa katika kuwafurahisha na mwisho wa siku hata tulichofanyia kazi tusilipwe.
Tunafanya mengi ya kifamilia na ni nadra sana sisi kufaidika nayo wakati wao wakila raha. Kwa hili pengine ndio sababu hata wanaume wengi kuwa na hasira sana pale wake/wenza wao wanapowasaliti.
Mwanamke hazeeki!jiulize ni kwanin mwanamke anawahi kuzeeka kuliko mwanaume
False. kama mtihani umepata -100Ni kwa sababu mwanaume anachepuka sana, so anajitengenezea sumu bila kujijua
Iyo ndo sababu na pia ukizngatia kuwa na majukumuEti eee
Hilo la mchepuko si lazima.kuanzia pesa,kujenga familia,mapenzi na kazalika kila kitu ni wewe.nani mwanaume kwa nini usife mapema
alafu ukiongeza na mchepuko duuu
HaswaaRisk taker..
angalia kazi tuzifanyazo wanaume nyingi ni risk,kazi ngumu.. maisha yetu yanakuwa kwenye hatihati ktk pilika za utafutaji wa maisha tupo mstari wa mbele,pia ktk kukabiliana na hatari(mazingira ya hatari) sisi tunahusika sana.. pamoja na tabia wanaume huwa tuna tabia fulani za ubishi,utawala ikitokea umedharauliwa basi vurugu linaanza hivyo lolote laweza tokea.. baada ya kufanya kazi ngumu utapita bar kupiga mbili tatu,sigara kazaa(unaharibu mapafu),huku ukiwa umelewa utaendesha gari,pikipiki n.k ukiteleza kidogo kwaheri..
kiujumla wanaume ni watu tunaokuwa kwenye risk kubwa kushinda wanawake.
Kama zipi? Za kumfanya mwanamke kama bidhaa(njia) itumikayo kwa kuinadi bidhaa husika?Dhambi zinauwa!
Mwanamke ni mfalme kwenye uumbaji!
Mtu mweupe ameitambua hiyo ndiyo maana sheria zao zinalinda sana maslahi ya mwanamke,
Theory yako ni ya uwongo. Wanaume ni risk takers always. Wapo ambao hawakuwa na mchepuko lakin wamefariki mapema.Mkuu jaribu kutulia na kufikiri kidogo utakubaliana na mimi, 80% Wanaume wanakufa kwa ajili ya kuwa na wapenzi wengi