Na wababa wahivyo ni wasumbufu hakuna mfano, na wengi wanalalamikia watoto wao,
ukirudi nyumba waliwaterekeza watoto sasa ili wasitengwe wanakuja na hilo lakutengwa
Sent from my SM-T800 using
JamiiForums mobile app
unakuta baba ambae kakojolea kishimo cha mama na kuendelea na mishe zake, anakuandikia ujumbe kama huu kisa umemwambia hela sina
"Tambueni kuwa, kama unao uwezo, na mzazi wako akahisi kwamba unao huo uwezo halafu ukaacha kumwondolea machungu au shida zinayomsibu unaweza ukajikuta unakumbana na matukio yafuatayo:-
* unaweza ukajikuta fedha nyingi pamoja na vitu vingine muhimu vinapotea kwa wakati moja bila kutatajia
* Matukio makubwa kama maradhi ya mara kwa mara yatakayokugharimu fedha nyingi yakajitokeza.
* Ukajikuta mtafaruku unaibuka ghafla kati yako na mwenzako (mkeo) hata kwa jambo dogo na kupelekea kukimbilia mahali pa kuondoa maudhi kwenye unywaji wa pombe, wanawake au vyote kwa pamoja.
* Ukajikuta umejiingiza kwenye urafiki na makundi ya vijana waovu au kamari na kujikuta unafuja fedha njingi bila kujitambua.
* Ukajikuta jeuri au uwezo wa kifedha unakuwa wa kujionyesha zaidi ili utukuzwe au kujipatia sifa kutoka kwa watu hao wakati wazazi wako wako tayari kuridhika kwa kiasi kidogo sana na kukuacha ujishughulishe zaidi na mambo yako mwenyewe. Wekeni kumbukumbu hizi kwa ajili ya kuwapa mafundisho watoto wenu watakapokuwa wakubwa.
Ni mimi Baba yenu."
hayo maneno nimeambiwa na baba yangu mzazi ambae hakujihusisha na mimi kwa lolote lile maishani mwangu. na hela za mafao alizopewa na mfuko alienda kuongeza mwanamke mwingine na kumuacha mke wake wa ndoa.
Leo hii anaandika ujumbe kama huo analialia nimtumie hela ila azitumie na huyo mwanamke wake.
huo upuuzi sifanyi na lolote halinipati maana hata Mungu ameona.