Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Haya mambo hayatokei bahati mbaya na pengine mnadhani yanasababishwa na masababu makuuubwa kama vile; baba kutumbua mali na michepuko au kumpiga/kumfoka mke wake kipindi akiwa na nguvu la hasha! Sababu ya haya pengine ni ndogo ndogo sana zinazokuja kumpa “uthamani” mama wakati wa uzee dhidi ya baba.

Nimesema sababu ya haya ni ndogo ndogo sana kwakuwa si kila baba aliwahi kumtreat vibaya mkewe kipindi wakiwa na nguvu na si kila baba alikuwa anatumia mali zake nje balada ya kwenye familia, wababa wengine huishi na wake zao vizuri tu na bado uzeeni hupokea treatment isiyofair kutoka kwa watoto. Kinachowafelisha wababa wengi ni kutokuwa na uwezo wa kutengeneza bond na watoto wao isiyovunjwa/vunjika kwa urahisi na bond hiyo yapaswa aitengeneze mwenyewe baba na si kusubiri kupigiwa chapuo na mama. Kwenye hili linatufavour wanawake sababu ya vitu vidogo vidogo tunavyofanya kila siku kwa watoto wetu, mfano: wakiwa wadogo kuwapikia, kuwalisha, kuwabembeleza, kulala nao, kucheza nao muda mwingi, kuwaogesha, kuwapeleka hosptal, kuwapeleka shopping etc, na wakiwa wakubwa kuwa nao karibu na kuact kama daraja kati yao na baba yao, mfano: mtoto ana shida anamueleza mama, mama anaichukua anaipeleka kwa baba inatafutiwa suluhisho, then suluhisho hilo analibeba mama kulipeleka kwa mtoto as if amelitatua peke yake wakati kiukweli wamelitatua kushirikia na baba, au baba amelitatua nyuma ya pazia, mbele ya pazia amemrudisha mama kupeleka feedback, hapo mama anajizolea credits zote kwa mtoto.

Lazima tufahamu hivyo vitu vidogo vidogo wanavyovifanya wamama (care taking) automatically huwafutia hatia kwa watoto wao na kusababisha kupokea huruma ya moja kwa moja kutoka kwa watoto zao kuliko wababa, sijasema wanaume muanze kuwapikia, kuwalisha sijui kucheza na watoto huu ni uamuzi wa mtu binafsi kufanya au kutokufanya lakuzingatia wacheni kujitia ubusy uliopitiliza kwa madai ya kuwatafutia ada sijui kuwajengea nyumba jifunzeni kubalance mambo sababu inaonesha nature haiwapi favor katika hili. Nafahamu kubalance mambo ni ngumu sana, lakini lazima mkubali kuwa kuwa mwanaume unayejielewa inahitaji XXL efforts, na msidhani kuwa mama bora ni rahisi kiivyo mtu yakupasa ujitoe ufahamu kweli kweli, kila mtu ana ugumu wake.

Ukitaka kuamini ninayosema, chunguza mtoto aliyelelewa na single father uone kama kuna siku za maisha yake atamchagua mtu mwingine yeyote dhidi ya babayake.
 
unakuta baba ambae kakojolea kishimo cha mama na kuendelea na mishe zake, anakuandikia ujumbe kama huu kisa umemwambia hela sina

"Tambueni kuwa, kama unao uwezo, na mzazi wako akahisi kwamba unao huo uwezo halafu ukaacha kumwondolea machungu au shida zinayomsibu unaweza ukajikuta unakumbana na matukio yafuatayo:-
* unaweza ukajikuta fedha nyingi pamoja na vitu vingine muhimu vinapotea kwa wakati moja bila kutatajia
* Matukio makubwa kama maradhi ya mara kwa mara yatakayokugharimu fedha nyingi yakajitokeza.
* Ukajikuta mtafaruku unaibuka ghafla kati yako na mwenzako (mkeo) hata kwa jambo dogo na kupelekea kukimbilia mahali pa kuondoa maudhi kwenye unywaji wa pombe, wanawake au vyote kwa pamoja.
* Ukajikuta umejiingiza kwenye urafiki na makundi ya vijana waovu au kamari na kujikuta unafuja fedha njingi bila kujitambua.
* Ukajikuta jeuri au uwezo wa kifedha unakuwa wa kujionyesha zaidi ili utukuzwe au kujipatia sifa kutoka kwa watu hao wakati wazazi wako wako tayari kuridhika kwa kiasi kidogo sana na kukuacha ujishughulishe zaidi na mambo yako mwenyewe. Wekeni kumbukumbu hizi kwa ajili ya kuwapa mafundisho watoto wenu watakapokuwa wakubwa.

Ni mimi Baba yenu."

hayo maneno nimeambiwa na baba yangu mzazi ambae hakujihusisha na mimi kwa lolote lile maishani mwangu. na hela za mafao alizopewa na mfuko alienda kuongeza mwanamke mwingine na kumuacha mke wake wa ndoa.

Leo hii anaandika ujumbe kama huo analialia nimtumie hela ila azitumie na huyo mwanamke wake.

huo upuuzi sifanyi na lolote halinipati maana hata Mungu ameona.
Hakuna laana duniani hiyo imani iue

Unachopaswa kujua zile ni fedha za baba yako si za mama yako wala zako
Inawezekana baba yako alimuoa mama yako akiwa na kazi hivyo matunda ya kazi yake yamekulea na kumtunza mama yako

Mafao yake ni yake acha aamue cha kufanya kazi yenu ni kumsaidia ushauri wa namna ya kuzitumia ila ushauri wenu si amri

Msaidie baba yako kama tendo jema kwa kila mtu pia tambua kumtunza ni kudhihirisha heshima kwake ambayo ni amri ya Mungu
Heshima>>>>>>integrity

Mama hasiwe borakuliko baba yako

Unajua mateso ya baba yako?
Unajua kwa nn ameoa kibinti?
Uliwahi kuwa kati au ulichukua upande ulipofikiri maisha ya wazazi wako?

Unajua litakalokupata wewe?

Life only one who lives in can define it!

Waheshimu wazazi wako upate rehema na neema duniani

Ukishindwa ni jukumu la Mungu si wazazi na Mungu hatoi hukumu leo isipokuwa lessons na hukumu ni mwisho
 
Ramark,
Mkuu sisi wote ni wanaume ila unatetea upuuzi, kama mafao yake ni yake hata akiyatumia kuhonga, kwa nini awe mlalamishi kwa watoto ambao hakuwathamini kipindi akiwa na mali?
 
Mkuu sisi wote ni wanaume ila unatetea upuuzi, kama mafao yake ni yake hata akiyatumia kuhonga, kwa nini awe mlalamishi kwa watoto ambao hakuwathamini kipindi akiwa na mali?
Mlalamishi!!!? Nawakati anakukumbusha takwa la kimungu la kumheshimu
Kuheshimu inamaana kubwa ndiyo maana nilitumia 'integrity' kuonyesha uwote katika kuheshimu yaani kuanzia mawazo hadi mwili na wewe shauri basi
Ukiamua nawe timiza wajibu wako wa kumsaidia kwani nani aliwaambia wazazi wanalipiziwa kisasa?
Ukitengeneza kisasi kati ya wewe na wazazi wako wakati wanao wanashuhudia unafundisha nini? Na kanisani au msikitini unaenda!!
Na si kwamba nawe umeacha kuhonga!! Au kutumia 80% ya mshahara au fao lolote peke yako!
Vijana wa kiume tunasumbuliwa na tamaa ya kisasi kuliko mabinti ambao wao wanajua baba anapaswa apate hela ya gongo.kidogo au tumbaku lkn wewe unataka hata ukimpa hela lazima anunue sukari nawakati sukari mwili wake ni chache

Eleweni mantiki ya kuishi na familia

Ukiwa mkubwa tambua huwezi badili kwa haraka tabia mbaya ya mzazi wako, take time tena kwa wema

But your first priority must be your legitimate familiy before wazazi
 
Hata mchepuko ni sehemu ya majukumu

Hakuna mwanaume mwenye ndoa hasiye na mchepuko tangu dunia ianze
Wewe endelea kusema hoja isiyo na uhalisia

Lazima mwanaume achepuke ili aorganize mawazo na ndiyo maana mchepuko ukiwa na kelele kinapigwa chini
Mke analea na kutunza familia hana muda wa kumfariji mwanaume as friends hivyo mwanaume kwa asili bila faraja hawezi kusurvive na akisurvive hapigi hatua na ndiyo maana wabeba mizigo jioni wanahonga na kula mzigo ili kesho wafanye kazi kwa furaha
Basi na ikifika jioni pambana na michepuko sio kuleta mizigo nyumba kubwa komaa huko huko, ndiyo maana wengi hula mpaka mabanzi kwa wake zao[emoji3][emoji3][emoji3], kama ni faraja kinacho warudisha huwa nini!
 
Yes baba unatakiwa uwe hardcore, mama ananguvu ya ushawishi na ni mzazi ambaye kiasili hupendwa na watoto sana kuliko baba.

Halafu ukitegemea kupata faraja kutoka kwa watu wengine utapata depression zisizo na misingi. Kipindi ambacho unanguvu na unamshiko ndio kipindi sahihi cha kuamua maisha yako ya uzeeni yaweje.

Sasa kama ulikua mtu wa tungi daily viwanja na hukuwekeza sehemu yeyote ili kipindi kama hiki unufaike utawalaumu watoto na mama yao?
Oyaaa ngapi uko
 
Hakuna laana duniani hiyo imani iue

Unachopaswa kujua zile ni fedha za baba yako si za mama yako wala zako
Inawezekana baba yako alimuoa mama yako akiwa na kazi hivyo matunda ya kazi yake yamekulea na kumtunza mama yako

Mafao yake ni yake acha aamue cha kufanya kazi yenu ni kumsaidia ushauri wa namna ya kuzitumia ila ushauri wenu si amri

Msaidie baba yako kama tendo jema kwa kila mtu pia tambua kumtunza ni kudhihirisha heshima kwake ambayo ni amri ya Mungu
Heshima>>>>>>integrity

Mama hasiwe borakuliko baba yako

Unajua mateso ya baba yako?
Unajua kwa nn ameoa kibinti?
Uliwahi kuwa kati au ulichukua upande ulipofikiri maisha ya wazazi wako?

Unajua litakalokupata wewe?

Life only one who lives in can define it!

Waheshimu wazazi wako upate rehema na neema duniani

Ukishindwa ni jukumu la Mungu si wazazi na Mungu hatoi hukumu leo isipokuwa lessons na hukumu ni mwisho
Chief, kwanza kabisa mzee alipita tu kwa mama, alikua na mke wake wa ndoa, mama hakujua.

pili, nilijitahidi sana kurudisha majeshi kwa mzee. nikampanga aje bar flani tuongee jambo moja zito sana, baada ya bia kutuchangamsha akaanza kulia shida zake nikamwambia mzee hela yako ipo usjali tunywe bia, baada ya mda kidogo nikamwambia mzee tuagize chakula tule, akadai hio hela ya chakula iongezee kwenye hela uliyonipromise kunipa, kiukweli moyoni nilimshangaa sana huyu mzee. ni kwamba yupo kimaslahi sana hata kula chakula cha pamoja na mimi anaona kama natumia hela zangu vibaya ni kheri nimpe yeye akale na mwanamke wake mwingine.

akaanzisha tabia kila wiki ananiomba hela. nikaona kwamba mimi nimemfata kiupendo tujenge chemistry na ukaribu, yeye ananiona kama kitega uchumi kipya kimeleta kwenye maisha yake.

alipoharibu kabisa ni baada ya kuomba hela jumamosi ya kuamkia Pasaka nikamwambia sina, ndo akatuma mmeseji mreeefu wa kulaani watoto wake ambao hawamtunzi.

kiukweli tangu siku hio nilimwona hana maana. ni mtu ambae hataki kuelewa wewe mfuko wako upoje, yeye anataka shida zake zitimizwe kabla ya za kwako.

sina mazoea nae tena.
 
Honour and sense of duty
Basi na ikifika jioni pambana na michepuko sio kuleta mizigo nyumba kubwa komaa huko huko, ndiyo maana wengi hula mpaka mabanzi kwa wake zao[emoji3][emoji3][emoji3], kama ni faraja kinacho warudisha huwa nini!
 
Chief, kwanza kabisa mzee alipita tu kwa mama, alikua na mke wake wa ndoa, mama hakujua.

pili, nilijitahidi sana kurudisha majeshi kwa mzee. nikampanga aje bar flani tuongee jambo moja zito sana, baada ya bia kutuchangamsha akaanza kulia shida zake nikamwambia mzee hela yako ipo usjali tunywe bia, baada ya mda kidogo nikamwambia mzee tuagize chakula tule, akadai hio hela ya chakula iongezee kwenye hela uliyonipromise kunipa, kiukweli moyoni nilimshangaa sana huyu mzee. ni kwamba yupo kimaslahi sana hata kula chakula cha pamoja na mimi anaona kama natumia hela zangu vibaya ni kheri nimpe yeye akale na mwanamke wake mwingine.

akaanzisha tabia kila wiki ananiomba hela. nikaona kwamba mimi nimemfata kiupendo tujenge chemistry na ukaribu, yeye ananiona kama kitega uchumi kipya kimeleta kwenye maisha yake.

alipoharibu kabisa ni baada ya kuomba hela jumamosi ya kuamkia Pasaka nikamwambia sina, ndo akatuma mmeseji mreeefu wa kulaani watoto wake ambao hawamtunzi.

kiukweli tangu siku hio nilimwona hana maana. ni mtu ambae hataki kuelewa wewe mfuko wako upoje, yeye anataka shida zake zitimizwe kabla ya za kwako.

sina mazoea nae tena.
Mwambie ukweli huo hapo juu ukisum up uzi huu

Laana haina mizizi dunia ache ajiliwaze na laana

Mwambie pesa yangu si yako be cold pliz
Mwambie nakusaidia na si lazima upate kila unapotaka na ajue kabla ya yeye kuna familia, wewe, mama yako, na wadogo zako

Kuomba hela kila mara kwa ajili ya matumizi ni upuuz now kama unaweza mpangie bajeti ya kila mwezi kiasi fulani kama huwezi mwekee miez miwili, mkatie bima ya afya kama ofisi inakuruhusu au ya mwaka reneuwable kisha muache

Usimuhukumu kwa matumiz yake kwani jukumu lako ni kutoa si kusimamia matumizi( mke wake huyo hakuhusu na wala hasidisturb uamuzi wako kwa baba yako)

Dunia hii na wazazi hawa wenye mitindo yao si lazima wabadirike unachopaswa ni kukubali ndiye baba, muaminishe mke na watoto, mama, ndugu zako na rafiki then maisha yatakuwa rahisi yaani kubali uhalisia uhalisia kisha ishi katika Honour, justice and sense of duty
 
wilson kaiser senior,
Pamoja na kwamba mambo ya kijamii yanachangia kufa mapema zaidi kwa mwanaume ukilinganisha na mwanamke, ukweli ni kwamba katika Demography kuna kitu kinachoitwa 'sexual dimorphism' ambayo kwayo mortality rate kwa wanaume ni kubwa zaidi kuliko ya wanawake kwa binadamu wote ulimwenguni.

This is by nature. Sex-ratio at birth ulimwenguni kote huwa takriban 105. Maana ya sex-ratio ya 105 ni kwamba kwa kila wasichana 100 wanaozaliwa, wanazaliwa wavulana 105. Takwimu za Tanzania, kwa ujumla, kwa mwaka wo wote ule zitathibitisha hilo. Angalizo: takwimu za kliniki moja moja ndogo ndogo zinaweza kuwa tofauti kwa kuwa idadi inayohusika ni ndogo.

Kwa kuwa mortality rate ya wanaume ni kubwa zaidi, wavulana hupungua kwa kasi zaidi kuliko wasichana, na mpaka kufikia miaka ya 60 wanawake ambao bado wanaishi huwa wengi zaidi ya wanaume. Hivyo basi, ulimwenguni kote huwa kuna wajane wa kike (widows) wengi zaidi kuliko wa kiume (widowers). Sex-ratio kwa umri wa miaka 60 na kuendelea huwa kwenye 90 hivi na huzidi kushuka kadiri umri unavyopanda mpaka kufikia hata 85.

Maana ya sex-ratio ya 85 ni kwamba katika kila wanawake 100 waishio, wapo wanaume 85 tu. Kipindi pekee ambacho mortality rate ya wanawake huwa kubwa zaidi ya ile ya wanaume ni wakati wa reproductive period (umri wa miaka 15-49) kukiwa na high maternal mortality (vifo vinavyoandamana na uzazi). Kwa nchi ambazo zimethibiti maternal mortality kiasi kwamba wanawake wachache tu ndiyo hufa kutokana na uzazi, mortality rate ya wanaume huwa juu zaidi ya ile ya wanawake for the entire lifespan. Haya ndiyo malimwengu.
Technical answer
 
Baba inabidi ujiandae na haya yote kwa kuwekeza katika ujana wako. Hata uzeeni watoto wakijitenga huwezi kufa njaa, vitega uchumi vyako vinakulea.
Kumbuka ma Baba hutumia mpaka senti yao ya mwisho hata ikibidi kukopa watoto wao wapate elimu,mahitaji na malezi Bora kwa mstakabali wa maisha yao lakini wakishalishwa sumu na mama zao ndio matokeo yake sasa hapo ni muda gani atajiwekea hakiba?
 
  • kuna kile kipindi cha kuanzia miaka 0 hadi 7 ya mtoto, kabla hajaanza primary unaweza kujijenga.
  • pia kuna kipindi cha primary na sekondary mtoto akisoma public school ada ni bure unaweza ukajimudu kujijenga.
  • pia kuna kipindi kile cha chuo mtoto akipata BOOM unaweza kujijenga.
  • pia kuna SACCOS na mabenki unaweza kukopa ukajijenga.
baba anaesema hela zake zote zinaishia kusomesha ni mvivu wa kufikiri.
 
Niliwahi kuongea na mwenzangu mmoja japo alikataa lakini huo ndo ukweli

Tuchukulie incidences kama kulinda lindo usiku,dereva wa gari akifa,wanaovua samaki,wanaoingia migodini.n.k,katika haya matukio zaidi ya 90% ni waume na inapotokea vifo namba kubwa ya vifo ni wanaume na hapo tayari tunaongeza wajane kama alivyo mama yangu naye ni mjane tayari...Mungu awalinde wanaume
Aisee wanaume tunapitia ktk majukumu mazito sana ktk kutafuta ridhiki mfano mie kazi nikuyo kuwa nayo before ilinibdi niwe naendesha gari.

Ktika pilika hizo ndani ya miaka mi 4.....
1.Nimepinduka na gari mara moja
2.Gari gari imekata tyroid hand mara moja nikaingia porini hii steering inakuwa out of control gari inakupeleka inakotaka
3.Nikabadlishiwa gari kilichofuata nikishaingia nayo porini out of control mara 2 unakuata mguu unachoma tyre ya mbele inachomoka...... so inakupeleka direction yake...
4.Nyingine usk nimesinzia baada ya kazi nzito.....kuendesha gari nikasikia ngu...ngoma igonga karavata inayoyoma mtaloni.....!
So kazi,zetu ili kupata kipato cha kukidhi familia kama kula,kusomesha na kuwa na maisha mazuri.

Wanaume tunachotaka kwenu kina mama ni mapenzi,na amani hatupendi kelele na ukosefu wa amani na maneno mengi hapo ndio tunaenda nje kujiliwaza na pombe na sigara na vimada.

So tunakuwa na misongo ya kazi,ndoa,na kendesha familia,kuingia ktk vimada ila nako yunakutana vimeo mwisho wa siku nako kunaleta shida na kuongeza invoice...

Kifupi maisha ya mwanaume ni taabu tupu na hapo ndio unagundua Baba zwtu wamepitia ktk shida japo tunajifanya hakuna kama mama.
Wababa mnanielewe changamoto tulizonazo,
Tunashindwa kula kazini ili mradi unachopata wale watoto na mama kazi ngumu mlo mmoja wenzio mke na watoto wanapiga lakaa 3......

Mwisho wa siku uzeeni baada ya kustaafu mwili ndio unajibu mapigo,mke anakuona you are nothing,watoto wanaona mama ndio kila kitu so unabaki mpweke tu.

wamama wanajitunza,wanavaa,wanjipodoa,wanakula vizuri,kazi zao sio hatarishi,wanakuwa krb sana na watoto wao maana muda mwingi wako nao we uko mzigoni upendo wao na watoto ni mkubwa mnoooo...

Tujitahidi kuwekeza ili akiba itufaaa maisha ya uzeeni,tuanzishe vibiashara vitusaidie uzee,tule vzr na tujitunze...tuishi maisha yenye furaha.....! amani na upendo,maisha ni sasa mbeleni taabu tuache visununu...!

Tusisahau kuishi na wenzetu/ke kwa akili...imeandikwa
 
Apo
sijafanya utafiti wowote siriaz..lakini najaribu kuangalia mazingira nitokayo pale kijijini..idadi ya wajane wanaotuzunguka akiwemo mama yangu mzazi..inatisha!!wamebaki kina mama/bibi peke yao kule nyumbani........tumaini lao lipo kwa watoto wao na kama mungu amewajaalia vijukuu mapema basi ikiwapendeza wamuache pale nyumbani akae na bibi/mama...

hivi wenzangu huko mtokako mmeshaliona hilo?...wanaume wamekuwa wakiripotiwa either kufa mapema zaidi au kufa mapema tu kwa sababu kadha wa kadha..........wanaume mnalizungumziaje hili suala...tumejiandaaje..au tunajiwekea mazingira gani ya kupunguza idadi ya wajane n ayatima hasa ukizingatia wanaume ndio vichwa vya familia...................eeh Mungu tunusuru!!

ebu tujaribu kuliangali ahili.............
Apo kwenye kichwa Cha familia tu ni kifo tosha
 
Mimi Sina utafiti wowote ila natazama mazingira tu
Chukulia kijana anafanya kazi ya bodaboda zaidi ya miaka kumi alafu mkewe yupo tu nyumbani na makopo yake ya mkaa,jamaa anaendesha basi dar to bukoba alafu wife wake ana mradi wa saloon...mwanaume wa kipemba ni mvuvi usiku kucha yupo baharini huku mkewe anajipara na kula vzr...usisahau Kuna makamanda wapo migodini huko lazima tufe mapema
 
Baba anapokuwa bado ana nguvu, yuko kazini huwa anakua na nguvu na ushawishi mkubwa sana kwenye familia yake, familia humsikiliza, huzingatia uwepo wake.

Tatizo huanza pale baba anapozeeka, nguvu za uzalishaji mali zimekwisha, amestaafu! Na pale watoto wanapokua wamekua watu wazima wameanza maisha yao! Hapo ndipo mambo kwa baba humgeuka.

Mkewe huanza kumchukulia poa! Ile heshima aliyokuwa akipewa huanza kupungua taratiib.. baba hasikilizwi tena Kama zamani, isitoshe anakua hahusishwi sana tena kwenye mambo ya mkewe sababu hata akiambiwa atasaidia nini na pesa hana? Badala yake mkewe huanza kuwafanya watoto kuwa washirika wake zaidi na kumuweka kando mumewe. Baba anaachwa pembeni.

Mama huanza safari kwenda kwa watoto, huko hukaa sana, baba kaachwa nyumbani peke yake! Watoto wanagombea mama aende kwao, lkn baba hakuna anayemtaka.

Wakiwa nyumbani na mkewe, simu toka kwa watoto 80% anapigiwa mama, baada ya maongez mareefu, ndo baba anapewa simu anasalimiwa dk 2 imeisha hiyo! Baba simu anayo, ila haoni simu za watoto wakimpigia, na wakimpigia ni kwa sababu maalumu tena maongez huwa mafupi! Hawana muda nae.

Baba anajikuta anakuwa mpweke sana, anakuwa mgeni kwa familia yake mwenyewe! Wale ambao alizimalizia nguvu zake za ujana kuwatafutia hawana muda nae.

Pale baba anapokuwa anaihitaji sana faraja ya familia yake sababu ameshazeeka... Familia humpa kisogo! Upweke unamsonga! Sababu ya upweke mawazo humsonga, hili hupelekea kinga ya mwili kushuka na kufanya iwe rahisi kushambuliwa na magonjwa na haichukui muda anafariki.

Familia wataliaa, watachapisha matisheti, watatoa mapesa kumnunulia sanduku la gharama na kumjengea kaburi la gharama, mitandaoni watampost sana! Lakini alipokuwa hai... No one cares.

Tuwajali baba zetu, walijitoa na kujinyima sana kufanya tufike tuliko! Ni dhambi mbele za Mungu tena ni laana mbaya kuwapuuza baba zetu.
[emoji30][emoji30][emoji30] imenigusa san tena mnoooh,
 
Aisee wanaume tunapitia ktk majukumu mazito sana ktk kutafuta ridhiki mfano mie kazi nikuyo kuwa nayo before ilinibdi niwe naendesha gari.

Ktika pilika hizo ndani ya miaka mi 4.....
1.Nimepinduka na gari mara moja
2.Gari gari imekata tyroid hand mara moja nikaingia porini hii steering inakuwa out of control gari inakupeleka inakotaka
3.Nikabadlishiwa gari kilichofuata nikishaingia nayo porini out of control mara 2 unakuata mguu unachoma tyre ya mbele inachomoka...... so inakupeleka direction yake...
4.Nyingine usk nimesinzia baada ya kazi nzito.....kuendesha gari nikasikia ngu...ngoma igonga karavata inayoyoma mtaloni.....!
So kazi,zetu ili kupata kipato cha kukidhi familia kama kula,kusomesha na kuwa na maisha mazuri.

Wanaume tunachotaka kwenu kina mama ni mapenzi,na amani hatupendi kelele na ukosefu wa amani na maneno mengi hapo ndio tunaenda nje kujiliwaza na pombe na sigara na vimada.

So tunakuwa na misongo ya kazi,ndoa,na kendesha familia,kuingia ktk vimada ila nako yunakutana vimeo mwisho wa siku nako kunaleta shida na kuongeza invoice...

Kifupi maisha ya mwanaume ni taabu tupu na hapo ndio unagundua Baba zwtu wamepitia ktk shida japo tunajifanya hakuna kama mama.
Wababa mnanielewe changamoto tulizonazo,
Tunashindwa kula kazini ili mradi unachopata wale watoto na mama kazi ngumu mlo mmoja wenzio mke na watoto wanapiga lakaa 3......

Mwisho wa siku uzeeni baada ya kustaafu mwili ndio unajibu mapigo,mke anakuona you are nothing,watoto wanaona mama ndio kila kitu so unabaki mpweke tu.

wamama wanajitunza,wanavaa,wanjipodoa,wanakula vizuri,kazi zao sio hatarishi,wanakuwa krb sana na watoto wao maana muda mwingi wako nao we uko mzigoni upendo wao na watoto ni mkubwa mnoooo...

Tujitahidi kuwekeza ili akiba itufaaa maisha ya uzeeni,tuanzishe vibiashara vitusaidie uzee,tule vzr na tujitunze...tuishi maisha yenye furaha.....! amani na upendo,maisha ni sasa mbeleni taabu tuache visununu...!

Tusisahau kuishi na wenzetu/ke kwa akili...imeandikwa
🙏🙏🙏🙏🙏 Umenikosha mkuu na wanaume tuzingatie point yako ya mwisho tujiwekezee wake zetu tukishafika miaka 60 ndio wanatumaliza kiulaini Sana wakishirikiana na wayoto
 
Back
Top Bottom