Baba anapokuwa bado ana nguvu, yuko kazini huwa anakua na nguvu na ushawishi mkubwa sana kwenye familia yake, familia humsikiliza, huzingatia uwepo wake!
Tatizo huanza pale baba anapozeeka, nguvu za uzalishaji mali zimekwisha, amestaafu! Na pale watoto wanapokua wamekua watu wazima wameanza maisha yao! Hapo ndipo mambo kwa baba humgeuka!
Mkewe huanza kumchukulia poa! Ile heshima aliyokuwa akipewa huanza kupungua taratiib.. baba hasikilizwi tena Kama zamani, isitoshe anakua hahusishwi sana tena kwenye mambo ya mkewe sababu hata akiambiwa atasaidia nini na pesa hana? Badala yake mkewe huanza kuwafanya watoto kuwa washirika wake zaidi na kumuweka kando mumewe... Baba anaachwa pembeni!
Mama huanza safari kwenda kwa watoto, huko hukaa sana, baba kaachwa nyumbani peke yake! Watoto wanagombea mama aende kwao, lkn baba hakuna anayemtaka!
Wakiwa nyumbani na mkewe, simu toka kwa watoto 80% anapigiwa mama, baada ya maongez mareefu, ndo baba anapewa simu anasalimiwa dk 2 imeisha hiyo! Baba simu anayo, ila haoni simu za watoto wakimpigia, na wakimpigia ni kwa sababu maalumu tena maongez huwa mafupi! Hawana muda nae!
Baba anajikuta anakuwa mpweke sana, anakua mgeni kwa familia yake mwenyewe! Wale ambao alizimalizia nguvu zake za ujana kuwatafutia hawana muda nae!
Pale baba anapokuwa anaihitaji sana faraja ya familia yake sababu ameshazeeka... Familia humpa kisogo! Upweke unamsonga! Sababu ya upweke mawazo humsonga, hili hupelekea kinga ya mwili kushuka na kufanya iwe rahisi kushambuliwa na magonjwa na haichukui muda anafariki!
Familia wataliaa, watachapisha matisheti, watatoa mapesa kumnunulia sanduku la gharama na kumjengea kaburi la gharama, mitandaoni watampost sana! Lakini alipokuwa hai... No one cares!
Tuwajali baba zetu, walijitoa na kujinyima sana kufanya tufike tuliko! Ni dhambi mbele za Mungu tena ni laana mbaya kuwapuuza baba zetu!
Sent using Jamii Forums mobile app
Una unri gani mkuu?! Maana si kwa pumba hizi aisee,mm nina mifano hai ya watu waliokuwa responsible mno na familia zao na wala sio walevi wala wazinzi lkn baada ya uzee kuingia na Mambo kuwaendea kombo wametengwa na familia zaoSiku zote Utakachokipanda ujanani utavuna uzeeni. Ukiona baba wa hivyo ujue wakati wa ujana alihangaika na michepuko na marafiki. Ukiiipenda familia yako na mkeo hawatakaa wakutenge hata iweje. Watoto wako watasimama na wewe wakituma tickets ya ndege watatuma 2 .
Ni mzee hao unaowaona kwa nje kwa undani huwajui angakia aliishi vipi na mke wake walikuwa marafiki au ndio ule urafiki wa kitandani tu alikuwa na mahusiano gani na watoto wake kuprovide na ku care kwa familia ni vitu viwili tofauti. Wewe toa pesa zako halafu hata watoto wako huongei nao unategemea nini? Ukizeeka wanakuona stranger tu maana hata hawajui hobbies zako. Mimi baba yangu ni mzee sana kwa sasa lakini kwa kweli anapendwa na sisi na watoto tu na mke na wajukuu pia ukikuta yuko kwa simu na wajukuu zake utafurahi. The same kwa mme wangu yeye mpk watoto wa kaka zake wako very close na yeye kuliko baba zao yaani anajua siri zao hata baba zao hawajui yote hayo ni kwanini kwa sababu always alikuwa anatenga muda wa kukaa nao walikuwa wanacheza karata mara football sasa wewe unafikiri kulisha watu tu ndio kuwa baba.Una unri gani mkuu?! Maana si kwa pumba hizi aisee,mm nina mifano hai ya watu waliokuwa responsible mno na familia zao na wala sio walevi wala wazinzi lkn baada ya uzee kuingia na Mambo kuwaendea kombo wametengwa na familia zao
Sent using Jamii Forums mobile app
Baba inabidi ujiandae na haya yote kwa kuwekeza katika ujana wako. Hata uzeeni watoto wakijitenga huwezi kufa njaa, vitega uchumi vyako vinakulea.Ngoja niuchukulie kuwa huu ni mtazamo wako wewe unavyoishi na wazazi wako!!
Mwanaume anayesimama vyema kwenye misingi na misimamo ya kiuanaume anabaki kuwa mume bora kwa mkewe siku zote za maisha yao na anabaki kuwa baba bora kwa watoto wao siku za maisha yao!
Kufa au kuishi ni mipango na kudra za Mungu, Na hata ukifa mke na wanao wataheshimu kaburi lako kama shujaa aliyevimaliza vita!
Sawa mawazo hayapigwi runguNgoja niuchukulie kuwa huu ni mtazamo wako wewe unavyoishi na wazazi wako!!
Mwanaume anayesimama vyema kwenye misingi na misimamo ya kiuanaume anabaki kuwa mume bora kwa mkewe siku zote za maisha yao na anabaki kuwa baba bora kwa watoto wao siku za maisha yao!
Kufa au kuishi ni mipango na kudra za Mungu, Na hata ukifa mke na wanao wataheshimu kaburi lako kama shujaa aliyevimaliza vita!
Mwanaume ambae anasimama imara kwenye misingi ya uanaume anajua na kutambua majukumu na wajibu wake kwa familia yake na daima anapigania kesho njema kwa familia yake!baba inabidi ujiandae na haya yote kwa kuwekeza katika ujana wako. hata uzeeni watoto wakijitenga huwezi kufa njaa, vitega uchumi vyako vinakulea.
Hivi unadhani Mali ni kitu?Si jukumu la mtoto kumtunza mzazi wake
Si jukumu lao hata kidogo
Shida ya wazazi wetu hasa wakulima na wavuvi hawana maarifa ya akiba hivyo mwisho kuhitaji huduma ya lazima kwa watoto
Watoto kuwasaidia wazazi wao ni option na si lazima
Suala la mama kujaliwa baba akipoteza ushawishi ni upuuzi pia wa baba wakati wa ushawishi na mali hakujitunzia hivyo alitumia mali na ushawishi wake kwa asilimia kubwa nje ya familia
Lkn mwanaume usikubali kupoteza ushawishi na mali yako hata ukistaafu kazi maana wanaume wengi nyakati hizo ndiyo huwapa fursa wake zao kuwa na ushawishi mfano mama salma kikwete, mke wa baba yangu nk
Na utakufa haraka ukipoteza ushawishi lazima uhakikishe mpaka unakufa uwe na marafiki zako, connections, akiba na maamuzi hata hao watoto watakupigia kwani uzoefu wa mipango ya maisha wanategemea kwako hata mikopo midogo
Husiishi kuwahangaisha wanao baadaye
Jenga nyumba yako yako, tunza mali zako zako na si za watoto mpe fursa mkeo aishi kwa uhuru kuanzia sasa, naye atimize ndoto zake akiwa nawe kijana ili mkizeeka mzeeke wote nguvu zenu zisidiane tangu mwanzo, watoto wakiona hivyo hata wewe hautakuwa na thamani
Hili ndio jibu.baba inabidi ujiandae na haya yote kwa kuwekeza katika ujana wako. hata uzeeni watoto wakijitenga huwezi kufa njaa, vitega uchumi vyako vinakulea.
Pamoja na yote hayo wengi wanakufa kwa sababu ya njaa,yaani kukosa Mali.Mali alizitumia ujanani kusomesha watoto ambao ni waume na wake za watu wengine.Hivi unadhani Mali ni kitu?
Hata uwe na mali nusu ya dunia , usidhani ndio furaha yako imekamilika.
Fikiria unakosa mtoto wa kukujulia hali. Mtoto wa kukutembelea.
Mke wako anakuacha nyumbani anahamia kwa watoto. Je hizo mali zako zaidi ya kukupa chakula zinakupa kipi kingine?
Wazee wanahitaji upendo kuliko Mali. Mzee usipompa hela lakini ukimjulia hali hilo kwake ni muhimu sana. Lakini akiwa na hela na hapati upendo huo ni upweke. Hata wewe usingetamani uwe kwenye hiyo nafasi.