Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

1.Wanaume tunasafiri sana ili kutafutia familia mahitaji yao hivyo ajali ikitokea,tunakufa wengi kuliko wamama au wadada.
2.Wanaume huwa tunatunza mambo mengi moyoni hivyo kupelekea kudhurika kwasababu ya hayo mambo kutuletea matatizo ya moyo n.k.
2.Wanaume wengi tunakua na maadui wengi hasa wanaopatikana katika harakati za utafutai,hivyo hao maadui hutuwinda kutuua hasa kama dhuluma ilifanyika.
3.Shughuli nyingi hasa zile hatarishi kwa maisha yetu sisi wanadamu,hufanywa na sisi wanaume,mfano uchimbaji madini,hivyo mgodi ukianguka,tunakufa... mbali na magonjwa yanayopatikana kutokana na hiyo shughuli.
4.n.k
Hapo kwenye namba 2 nakuunga mkono,mfano,sehemu ninayofanyia kazi wanawake wakifika ofisi either atamsimulia mwezake shida zake na mume wake au ataimwaga hadharani ili apate msaada,lakini kwa wanaume hili sijawahi kuliona kwahiyo ni kweli tunabeba maumivu mengi sana wenyewe,na hii inatokana na kuwa ni nature yetu kuwa wasiri wa shida zetu au unaona ni aibu watu wengine kujua kuwa unaelemewa na mwanamke...
 
Sababu zimetolewa nyingi na zina mashiko,japo sikusoma zote.

Kwanza kwa biology ya kawaida,hata mbegu zikitolewa na mwanaume,twaambiwa za kiume,japo zipo na juhudi,ila hazina uwezo wa kuishi mda mrefu zikishafika panapokusudiwa kusubiri yai tofauti na mbegu ya kike ambazo ni slow lakini zenye kuishi zaidi-matokeo chance ya kuzaliwa wanawake wengi zaidi.Hii ni dalili moja kuwa,wanaume kuchoka kimaisha ni haraka zaidi toka kuzaliwa (labda)

Pili,pilika nyingi za maisha na pia za hatari na hata tabia za matumizi mabovu ya mlo,sigara,pombe na kubeba mengi moyoni bila kuyaanika au kuyatoa,ni chanzo kingine.

Lakini,HASA anayekosea na kuchukua mke asiyekufaa (kwa kuvutiwa tu na maumbile,sura n.k.),na kumbe huyo mwanamke hakupata mapenzi mwafaka HASA ya baba yake(na mama pia) katika makuzi yake toka utotoni,hawi na uwezo wa kutoa kile ambacho hakupewa na baba yake,yaani upendo hata kama rohoni angependa kweli,labda kwa muujiza wa Mungu tu.Hatajua tu namna ya kuuonyesha au kuutenda upendo zaidi ya mambo ya chumbani tu.Baba anayelea binti kwa upendo,urafiki na uelewa,huwekeza kwenye akaunti ya moyo wa bintiye upendo ambao,atakayefaidi zaidi ni atakayemuoa huyo msichana.

Sasa ukiwa na mke wa namna hii (japo labda si mara zote),yafuatayo ni almost kuyakwepa si rahisi sana.Nayo ni;
michepuko(na hata kuuchepuka na mchepuko pia),
ulevi,
stress,
workholic (ili kukwepa kuwahi nyumbani),
nyumba ndogo na tunyumba tudogodogo,
sigara (kupunguza stress abda)
na mambo kama haya,ndio yanaharakisha kutumbukia kaburini.

Ukichanganya hayo yote na mengine labda nisiyoyajua,huleta haya masuala ya vifo vya mapema kwa wanaume.

Ila naamini,mwanaume mwenye mwanamke sahihi,ana nafasi kubwa sana kuyaishi maisha yake in full kwa mapenzi ya Mungu kwani mengi ambayo yanachangia uharaka wa umauti wake,yatayeyuka.Maoni na mtazamo tu.

Hivyo,mtazamo wangu,mwanamke sahihi kwa mtu ndio salama yake namba moja,mengine tunamwachia Mungu baada ya mhusika kujitunza na kujiheshimu.
 
Wanaume wengi hufa mapema kwa sababu ya stress ilo halipingiki,kwanza kabsa jamii ina matarajio makubwa sana na mtoto wa kiume kuliko wa kike.

Kuna umri mwanaume akiufikisha na hajatoka kimaisha stress zinakuwa nyingi ndio mana hata mateja wengi ni wanaume,jela wengi ni wanaume hii yote ni kwa sababu anapambana kikidhi matarajio ya jamii na anapofeli stress zinakuwa nyingi
 
Kuna nyakati huwa nakitamani kifo, sema ndio hivo tuna watoto tuwatunze kwanza
 
Kuna nyakati huwa nakitamani kifo, sema ndio hivo tuna watoto tuwatunze kwanza
Pole sana.Mungu alikuwa mwerevu kutupa watoto,labda pia alijua litatupa sense of purpose katika kuishi hasa kwa kuwatazama watoto wakati maisha yameshapoteza ladha au maana.
 
Pole sana.Mungu alikuwa mwerevu kutupa watoto,labda pia alijua litatupa sense of purpose katika kuishi hasa kwa kuwatazama watoto wakati maisha yameshapoteza ladha au maana.
Kuna muda napoteza furaha kabisa ya kuishi.
Uko sahihi familia, hasa watoto wanatupa sababu ya kuishi zaidi.
 
Wanaume tuandae mapema maisha yetu ya uzeeni.
Ujue hakuna wakujakumtegemea financial sio wanao wala ndugu. Wala mke usimtegemee uzeeni.


Andaa mapema ukiwa kijana.

Punguzeni kuoa uzeeni na kuzaa uzeeni.
 
Pia umesahau huwa kuna utamaduni wa kuoa mwanamke ambaye ni mdogo kwako ki umri kisheria mwenye Umri mkubwa ndiyo hutangulia kufa. Sasa unakuta mtu kapishana na Mkewe miaka 15-20 halafu mnataka kufa pamoja.
 
Hii mada ni ya siku nyingi zilizopita ila kutokana na uhalisia wake inaonekana kama imewekwa leo vile!
Ila wanawake hasa wa siku hizi Mungu anawaona !
 
Wanaume tuandae mapema maisha yetu ya uzeeni.
Ujue hakuna wakujakumtegemea financial sio wanao wala ndugu. Wala mke usimtegemee uzeeni.


Andaa mapema ukiwa kijana.

Punguzeni kuoa uzeeni na kuzaa uzeeni.
Maandalizi ya maisha ya uzeeni ni kwa wote,wanawake na wanaume na halina mahusiano ya utegemezi kwa yeyote kati yao,ila wakiwa pamoja,ndio maana ya kusaidiana na umaana wa kuwa pamoja.

Maisha kuoteza umaana au ladha,haimaanishi uzee.hayo huweza kutookea sababu ya changamoto kadhaa,hata kwa vijana.Ndio sababu wapo wazee wanaona maisha yana ladha nzuri sana hadi miisho kabisa ya maisha yao.

Mtoto unamleta duniani ili kutimiza amri ya Mungu ya kuijaza nchi (nadhani dini mbili zakubaliana na hili).Ila uzeeni,hata uwe na mabilioni pamoja na mali,msaada ya nguvu ya mtoto utahitajika,labda kama ulizaa majuha ama hukuzaa kabisa ama watoto ni washenzi kiasi ya kusahau kuna wazee waliowaleta hapa duniani.Na ni hapo hata ndugu watahusika (hasa kama nawe uliwajibika katika huuenzi undugu na hata urafiki kwa misaada n.k wakati una nguvu ujanani mwako).

Watoto wanazaliwa mda wowote ambao Mungu anamjalia mtu.Kwa usahihi,vema wakizaa mapema zaidi wakati mtu akiwa na nguvu NA UWEZO WA KULEA.Ila,si kila mtu Mungu humjalia uwezo huo mapema.Ktk dini,Ibrahimu alijaliwa mtoto uzeeni,na ndio akaleta uzao ulioenea sana leo huko waliko.

Kuzaa mapema bila maandalizi ndio kuleta viumbe duniani,wanateseka na kuishia kuja kuwa machokoraaa si ajabu na hata kuja kuwaona wazazi ama mzazi ni chanzo cha madhila yao.Huzai tu sababu una mbegu-sawa na huli tuu chakula sababu kipo.Hivyo,usahihi ni kujitahidi kuandaa mapema na kuzaa mapema,MUNGU akipenda na hali ikiruhusu kimalezi.

kila kitu chema chahitaji maandalizi makubwa na umakini sana,HASA KWANZA kuchagua mwenza (kabla hata ya huko kuzaa).Kuoa tu mapema (sijui unamaanisha ni mapema kiasi gani-nachukulia ukibalehe tu na kuwa na kashughuli LABDA).Kukurupuka na kukimbilia kuoa tu ndiko huku kuzalisha kuoa 'stress' ambazo zitapelekea labda hata malezi mabovu ya hao uliozaa 'mapema',maisha mafupi sababu ya tensions kwa muoaji na hata kuja kuharibu ndoa na watoto kuishi maisha ambayo hayakutazamiwa.

Haipaswi mtu kumpangia mda mtu mwingine kwani,binadamu hawafanani kamwe.Hili litamfaa huyu na lisimfae sana mwingine japo ni zuri.Akiga na kufuata mkumbo sababu tu nia ni njema ndio kuishia mahangaiko,majuto n.k.Kila mwenye akili ndogo tu ajua ni muhimu kutumia juhudi,maarifa na pamoja kudra za Mungu,kujiandaa mapema,kuoa mapema na kuzaa mapema ili kulea mapema wakati nguvu (na hata labda akili) zipo.Ila,si kila binadamu hupata hiyo baraka.Tupatapo hayo mapema,yabidi kushukuru Mungu na si kudhani 'kila mtu apaswa ayapate mda huo wa mapema na kila mtu anayapata ila ni kuzembea tu'.Ila,kwa mzembea kusudi kufanya hayo mapema,hilo ni tatizo lake mwenyewe na hasa ukizingatia risks za kuzaa uzeeni pia, hasa kibaiolojia,licha ya risks zingine.

Kuoa mapema na kuzaa mapema si sifa ama ujanja sana,na ndio chanzo cha kuvunjia ndoa kadhaa.Ila,kila mtu yapendeza akifanya hayo mapema HASA,kama alijiandaa mapema,na AKAFANIKIWA KUCHAGUA MTU SAHIHI 'mapema' na hatimae,kukubaliana WOTE WAWILI wazae mda upi na idadi gani ya watoto watakaowamudu.Kwani,sio ukishaoa tu ndio uzalishe ili watoto waje tu kiholela bila makubaliano na mipangilio ya wawili.Maoni yangu tu.Kila la heri
 
Mshiiri,
Huu ni mtazamo wangu ambao umetohoa maarifa ya kibiologia na kigizikia.
KINACHOTUMIKA KINACHOKA NA KUANGUKA MAPEMA IKILINGANISHWA NA KILE KINACHONUFAIKA. mtazamo huu unazingatia sana na kuheshimu dhana ya aina ya utumiaji, kiwango cha utumiaji na maintenance pia.

Wanawake wao wanapokea na wanavyopokea kutoka kwa wanaume vinawa sustain kuishi wakati wanaume wanatoa na kubaki wamechoka. Hii inaweza kuangaliwa pale mwanaume anapomaliza kufanya tendo la ndoa na kupiz anakuwa amechoka au yupo hoi ilihali mwanamke anakuwa amechangamka (endapo hakutakuwa na matumizi yasiyo ya asili: mfano condomu au dawa za kusisimua misuli)
Katika mazingira haya ni rahisi kwa mwanaume kuchoka mapema tofauti na mwanamke.

Hii inazingatia pia aina ya kazi wanazofanya wawili hawa,aina ya vyakula... hali ya kiafya (ya mwili na akili) genetic alleles, nk.
 
Mshiiri,
ME NILIACHANA NA MKE WANGU KIDOGO NIFE NA MAWAZO NA POMBE... NASHUKURU MCHEPUKO UKANIOKOA 🙁
 
Aiseh hii ndio sababu wanawake wataishi muda mrefu
 
Ukitaka kuepukana na janga hili,unapokuwa umejenga kibanda chako,na unaidadi ya watoto uliodhamiria,pamoja na mke wako,pengine na tugari twako tuwili,-achana na mkeo haraka sana kaa nae mbali na ishi kivyako isipokuwa lea watoto vyema remotely wasisumbuke kwa chochote ikiwezekana peleka boarding,wanawake wengi wakishazaa watoto kukishakuwa na nyumba,hutuona sisi wanaume ni wa kuuwa tu,mbaya wakikutana na magenge yao,huisi tunawabana kwa namna fulani,huanza kuingia katika majaribio la kutuuwa aidha kisaikolojia kwa mbinu zozote kutegrmeana na wenzake watakavyomshauri.By 75% wanaume wanakufa vifo vinavyosababishwa na wake zao.
 
Back
Top Bottom