Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

Je, Wanaume wengi hufa mapema kutokana na msongo wa mawazo (frustrations) unaosababishwa na wake zao?

sababu zipo nyingi sana nyongeza pia sisi wanaume sio wepesi kufunguka pale tunapokutana na changamoto mbalimbali kwenye maisha tunabaki na usiri wa hali ya juu kuliko wanawake, pili lifespan ya mwanamke ni kubwa kuliko mwanaume, mwanamke kamzidi mwanaume 5yrs, tatu wanawake wanauwezo mzuri sana wa kucontrol stress zao na mwisho wanaume tuna take risk kwa mambo mengi sana kuliko hawa dada zetu.
 
Kubwa kuliko yote wanawake wanaishi muda mrefu kwasababu wao hawana "wake" wa kuwaendesha na kuwapa stress
 
Japo takwimu utofautiana toka taifa na taifa au sehemu na sehemu ndani ya taifa ,kwa wastani wanawake uishi maisha marefu kwa zaidi ya miaka 5 ukilinganisha na wanaume.
Wataalamu hulielezea hili kutokana na sababu za kibiolojia, kijamii ,kitamaduni na kiuchumi.

Inasemekana wanawake wana hormone(oestrogen) inayoimalisha mfumo wa Kinga na kupunguza risk ya magonjwa ya moyo tofauti na wanaume ambao hormone ya testesterone hufanya kinyume cha hapo juu.

Hata hivyo, baadhi ya tafiti zinaonyesha hata kwa watoto na vijana wadogo iyo gap ya gender motarity huendelea kuwepo Jambo linalopelekea kuamini zaidi kuwa sababu zingine za kijamii , kitamaduni na kiuchumi zinaweza kuwa ndo mzizi wa hali hii.

Sababu nyingine zinazotajwa kuwa ni chanzo cha wanaume kufa mapema ni pamoja na:

Tabia ya uvutaji wa sigara na vilevi vingine
Unywaji wa pombe kupitiliza
Kushiriki katika matukio Kama wizi na ujambazi
Kushiriki katika kazi hatarishi Kama migodini na viwandani
Kupenda ufusika na hivyo kuishia kupata magonjwa Kama ukimwi na hepatitis

Sababu nyingine ya msingi inayotajwa ni tabia ya kuwahi kutafuta huduma za afya ( health seeking behavior). Inasemekana wanawake wako likely kwenda Hospitali kupata matibabu mapema zaidi kuliko wanaume. Ili limewafanya wanaume kufika kwa kuchekewa katika maeneo ya tiba na hivyo kuathiri afya zao zaidi.

Nini mtazamo wako juu ya hili na usiache kutoa sababu unayoinua wewe.
 
Ni nini haswa huwaaminisha wanawake kuwa wanaume ndio hutangulia kufa?

Kwa mfano kwenye familia mwanaume akasema "tuuzeni hili shamba lote ili tufungue biashara" utasikia mwanamke akijibu "unataka siku ukifa niishije na watoto? Wakati unajua hilo shamba ndio kimbilio langu"

Kwanini wanakuwa na mawazo haya? Je, kuna ukweli wowote kuwa wanaume ndio hutangulia kufa kabla ya wake zao?
 
Kwa sababu huo ndiyo ukweli, Wanawake huishi muda mrefu kuliko Wanaume na hiyo ni Dunia nzima, sasa kuhusu Mke wako kutaka ufe mapema hilo ni swala lako binafsi na ningekuwa wewe ningehoji na Ndoa yenyewe kama hata ina upendo ukweli, kwa kawaida Mwanamke aliyekupenda na Mke wako angependa hata mfe siku moja ili asibakie peke yake, ...
 
Stress za Maisha , na madhila mengine mengi , wanaume hukumbana navyo Zaidi kuliko wanawake, hata kwenye matukio kama ajali wahanga wengi ni wanaume . Hii yote ni katika kutafuta ili kukidhi matakwa ya familia. Pia wanaume tutabeba mambo mengi vifuani mwetu hatufunguki kama wanawake ambao shida zake za ndani anaelezea kwenye kila saluni atakayokwenda. Matokeo ya wanaume kubeba mambo mengi vifuani yanawazalishia magonjwa ambayo hatimaye huwaletea vifo. Rejea wimbo wa Msondo kuna kibwagizo kinasema ……. wanaume tumeumbwa mateeso oh mateso kuhangaikaaa...
 
Hii yaweza kua sababu nzur mkuu [emoji106][emoji122]

wanawake wanatuzd akil ndo maana... wanawake wengi ndo hutaft dawa ajil ya waume zao na c wanaume kutafta dawa.... pia wanaume tunaandamwa na uadui mkubwa kuliko wanawake hilo pia huashiria ufup wa maixh ye2
 
Tuanze na ajali ya moto Morogoro takwimu zinasema wanaume ni wengi kuliko wanawake.

1. Mwanaume unaoa mwanamke umempita miaka 10!! kwa hali ya kawaida unategema nani atawai kufa?

2. Makundi hatarishi, mfano wanaume wengi ndio wanaoathirika na uvutaji bangi madawa ya kulevya pombe sigara kali na mambo mengine kama hayo

3. Kutegemewa na familia wengi wanajikuta katika msongo wa mawazo hivyo kupelekea stroke, bp nk

4. Kufanya kazi ngumu na hatarishi katika ujenzi wa aina zote, viwandani n.k hii hufanya mwili kuthoofu mapema hivyo kumfanya mwanaume kufa mapema

5. Mwanamke yupo sensitive kwenye health care tofauti na mwanaume.
 
Lakini katika nyakati zingine wanawake pia hufa mapema kabla ya wanaume kutokana na sababu mbalimbali. Hususani wale wenye roho nzuri ndo hutangulia kufa
 
Kwa sababu huo ndiyo ukweli, Wanawake huishi muda mrefu kuliko Wanaume na hiyo ni Dunia nzima, sasa kuhusu Mke wako kutaka ufe mapema hilo ni swala lako binafsi na ningekuwa wewe ningehoji na Ndoa yenyewe kama hata ina upendo ukweli, kwa kawaida Mwanamke aliyekupenda na Mke wako angependa hata mfe siku moja ili asibakie peke yake, ...
Hapo umeongea point sana.
Mara nyingi mwanamke anayeongea maneno hayo ujue hajakupenda kutoka moyoni bali ni umaskini wake au njaa yake ndio imemleta ili apate kusurvive tu na kuchuma mali na pesa.
 
1.Wanaume tunasafiri sana ili kutafutia familia mahitaji yao hivyo ajali ikitokea,tunakufa wengi kuliko wamama au wadada.
2.Wanaume huwa tunatunza mambo mengi moyoni hivyo kupelekea kudhurika kwasababu ya hayo mambo kutuletea matatizo ya moyo n.k.
2.Wanaume wengi tunakua na maadui wengi hasa wanaopatikana katika harakati za utafutai,hivyo hao maadui hutuwinda kutuua hasa kama dhuluma ilifanyika.
3.Shughuli nyingi hasa zile hatarishi kwa maisha yetu sisi wanadamu,hufanywa na sisi wanaume,mfano uchimbaji madini,hivyo mgodi ukianguka,tunakufa... mbali na magonjwa yanayopatikana kutokana na hiyo shughuli.
4.n.k
 
Ni nini haswa huwaaminisha wanawake kuwa wanaume ndio hutangulia kufa?

Kwa mfano kwenye familia mwanaume akasema "tuuzeni hili shamba lote ili tufungue biashara" utasikia mwanamke akijibu "unataka siku ukifa niishije na watoto? Wakati unajua hilo shamba ndio kimbilio langu"

Kwanini wanakuwa na mawazo haya? Je, kuna ukweli wowote kuwa wanaume ndio hutangulia kufa kabla ya wake zao?
Utafiti katika hii kanda ya mapenzi/mahusiano/ndoa imegundua kuwa wanaume wengi hufa kabla ya wake zao hata kama wamezaliwa mwaka mmoja na kubaini kuwa tabia za wake zao huwafadhaisha na kuwafanya waishi maisha magumu sana na kupata yale maradhi ya kufisha kama HYPERTENSION, SAIKOSISI, STROKE N.K
Madhanio wakati wa utafiti ni kuwa je wanaume wasio katika ndoa pia wanashambuliwa sana na magonjwa haya ya kufisha kama cohort wao walio katika ndoa? Hatimaye ilibainika kuwa wasio katika ndoa ni wachache sana karibu na hamna, ila walio kwenye ndoa ni wote kama sio aina moja ni nyingine. Hitimisho likawa wanawake huchangia vifo vya mapema vya wanaume katika ndoa.
 
Back
Top Bottom