Ndio maana sisi wanaume tunaaswa sana kujenga bond imara kwa watoto wetu.
Mama zetu waliwazidi kete baba zetu, sababu wababa wetu walikuwa busy sana na kazi,kiasi cha kutohangaika na watoto kabisaa,mtu anashinda kazini akirudi misele, kwa washkaji vijiweni.akirudi ni usiku mkali anakoromea mama na watoto wanapigwa hovyo.
But siku hizi mjitahidi jaman, nenda katumikie beberu, ila ukirudi hakikisha hata mnashindana kucheza game la nyoka kwenye simu na mtoto, mnabadilishana story mbili tatu mnacheka na masomo nk.
Halafu hakuna upuuzi mwingine wababa mnafanya kama kufokea, kupiga mama au kumtamkia maneno ya dharau mbele ya wanaye. Hiyo ni mbaya sana. Watoto wanakuwa na rangi nyeusi kuhusu baba yao, na hata wakifanikiwa kutoka, wanamuwaza mama yao kwamba anateseka tu huko aliko, maana wanakufahama baba yao[emoji181]