Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Kwani wewe unajua roho ni nini?
Jenga utaratibu wa kusoma kwanza kabla hujaandika chochote mahali popote....
Swali lako nimeshalijibu kwenye mada hii hii .....!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani wewe unajua roho ni nini?
Jenga utaratibu wa kusoma kwanza kabla hujaandika chochote mahali popote....
Swali lako nimeshalijibu kwenye mada hii hii .....!!
Basi wanyama wana roho ndio maana wao na wanadamu wako kwenye kundi la viumbe hai. Yesu aluwaambia wanafunzi wakw siku alipowatokea baada ya kufufuka(tomaso alikuwepo) kwamba; ".....roho ndiyo itiayo uzima(uhai); mwili haufai kitu.
Sawa?
Uko sawa lakini sio kwa 100% kwasababu namna uhai ulivyopatikana kwa binadamu na viumbe wengine ni tofauti
Lakini uhai sio lazima usababishwe na roho ...
Kinachonifanya niseme hivyo ni chanzo cha uhaio wa wanyama na binadau kuwa tofauti,uhai wa binadamu ni roho kwasababu hiyo ndio ambayo Mungu aliiweka kwenye mwili na kwasababu Mungu ni roho basi kinachomfanya binadamu afanane na Mungu ni hiyo roho
Kwa upande mwingine wanyama na mimea haikuwa hivyo,Mungu alitamka navyo vikawa na hakuna mahali ambapo Mungu aliviopa roho ambayo ndio chanzo cha uhai,lakini kwakuwa navyo ni hai au vina uhai inawezekana uhai wao na wetu ni tofauti na ndio maana hata chanzo chetu ni tofauti
Kudai tu navyo vina roho kwasababu vina uhai wakati huo huo chanzo cha huo uhai ni tofauti na Mungu ambae ni Roho sidhani kama utakuwa sahihi!
Hapa hoja sio namna za roho bali ni kama wanyama nao wana roho au hawana, au sio? Tukirudi kwenye utofauti kati ya binadamu na mnyama ni ndogo sana, wote wanakula na kulala, wanasihisi njaa kama binadamu, wana hisia za kujaamiana ndio maana wanazaliana kama binadamu, wanazaa na kunyonyesha kama binadamu wafanyavyo, wanafurahi na kuhuzunika kama binadamu walivyo.
Hayo yote tukisingizia ni akili basi hata kichaa naye anahisi njaa na kutafuta kipoozeo, vile vile anahitaji kuwa huru na kufurahi hata kama ni kwa namna ya pekee kama kuokota makopo; kutukana watu nk. na mambo hayo yote kwa binadamu na mnyama yanaweza kutendeka wakati wakiwa hai tu(wakiwa na roho), wanapokufa moyo unasimamisha mapigo yake bila kujali huyu ni binadamu au mnyama, na wote wanakuwa hawajitambui, sasa nini kinakuwa kimepungua hadi hali hiyo itokee?
Mkuu unajichanganya mwenyewe tu, hoja yangu ni pumzi ya uhai yaani roho.Mti unasikia njaa?
Mti unasikia usingizi
Hivi unajua kama kuna wanyama hawajamiiani?
Unajua kama kuna wanyama ambao huyo huyo ni dume na huyo huyo ni jike?
Pamoja na hayo yote sijaona haya yanahusianaje na uwepo wa roho ....
Hata hivyo,unaweza kuniambia ni wapi ambapo umesoma au kupata ushahidi kuwa wanyamana miti nao wana roho?
Samahani mkuu Eiyer, kuna jambo linanitatiza kila siku. Halihusiani sana na maada iliyopo mezani ila naomba ufafanuzi wako tafadhali.
Napenda kujua endapo kazi ya uumbaji inaendelea au laa! Je Mungu bado anafanya uumbaji hadi leo hii? Je nami aliniumba kama alivyofanya kwa Adamu? Yaani alinifanyanga kwa udongo halafu akanipulizia pumzi ya uhai kama Adamu?
mkuu, vitabu vinatuambia uumbaji ulifanyika kwa siku sita halafu siku ya saba Mungu akapumzika ila hatuambiwi kama baada ya hiyo siku ya saba aliendelea na uumbaji au vipi. Hisia zangu zinaniambia huenda baada ya kuwaumba Adamu na Eva, Mungu aliweka tu system yaani kama aliseti tu mitambo hivyo utaratibu wa kuumba watu hautahusisha yeye kufinyanga udongo na kupulizia pumzi kama alivyofanya kwa Adamu. Napenda ujua kama uumbaji unaendelea au vipi.
natanguliza shukrani
Mkuu unajichanganya mwenyewe tu, hoja yangu ni pumzi ya uhai yaani roho.
Nafsi hai inakamilika hivi....
PUMZI YA UHAI + MAVUMBI YA ARDHI= NAFSI HAI ambayo ni mtu kamili anayeweza kufanya jambo au kitu kama wewe na mimi tunavyoweza kuandika na kuelewana.
Labda kwa kupata usahihi unaodhani watu hatuujui ungeeleza jambo linalowatofautisha binadamu na wanyama ni ipi? roho ina kazi gani kwa banadamu?
Nataka unioneshe kinachokufanya uone mimi siko sahihi!
Si nimekwambia kwa lugha tu hauko sahihi. Nafsi/ego sio spirit
Kubali ulitoa tafsiri sio. Nafsi maana ya ni ego na wala si spirit. Think of spirit as energy rather labda it will start to make senseDuh!
Kazi ipo ...
Eliza,unasema nafsi sio spirit kwasababu ipi na kwa misingi ipi na kwa ushahidi upi?
Sijui kama unalielewa hilo swali!
Dawa yenu,
Mungu hadi leo anaumba lakini sio direct bali anaumba indirect
Utaratibu ni ule ule ambao ulifanyika kwa adam lakini leo ni kwa njia tifauti kidogo ambayo ni kwa kujamiiana
Binadamu wanapojamiiana hutoka manii ambayo ni matokeo ya vyakula tulivyokula na vyakula ni matokeo ya udongo
Kwahiyo unaweza kuona jambo ni lile lile ila ni kwa namna nyingine tu!
Kubali ulitoa tafsiri sio. Nafsi maana ya ni ego na wala si spirit. Think of spirit as energy rather labda it will start to make sense
Mungu haumbi tena, bali kanuni alizoziweka awali ndizo zinaendeleza uzazi na mambo yote. Ukisema siku hizi watu wanaumbwa kwa kujaamiana vipi kwa miti na wawe? nayo yanajaamiana ili kuendeleza uzazi wao au wewe ukisikia uumbaji moja kwa moja unajifikiria wewe kwanza?
Uzazi wa kujaamiana ni matokeo ya kanuni za asili, kwamba mbegu za uzazi za jinsia mbili tofauti zinapokutana zinazalisha kiumbe kipya bila kujali wahusika walipanga au hawakupanga, hii ndio kanuni inayoendeleza uzazi; ndio maana kwa kanuni hii mtu anaweza kuzaa na ndugu yake wa damu ilhali mungu amezuia hilo.
Sidhani kama najichanganya bali naona hunielewi ...
Nimesema kwa kirefu vile ambavyo chanzo cha uhai wa binadamu na na wanyama ni tofauti
Nimekuambia kuwa uko sawa uhai unasababishwa na roho
Lakini nikakuambia kuwa sio lazima kwasababu wanyama wana uhai basi wana roho kwasababu inawezekana uhai wao chanzo chao kingine
Sababu iliyonifanya niseme hivi ni sababu ya chanzo cha uhai wao ambacho ni tofauti na sisi,sisi chanzo cha uhai wetu ni roho ambayo ni mfanano wetu na Mungu kwasababu Mungu ni roho,kwa upande mwingine wanyama wao uhai wao chanzo chake sio roho kwasababu hawakupewa roho kama binadamu ambayo ndio mfanano wa Mungu kwa binadamu
Kwa maana hiyo sasa,uhai wa wanyama chanzo chake naweza kusema sio roho lakini uhai wa binadamu chanzo chake ni roho!
Si nimekwambia kwa lugha tu hauko sahihi. Nafsi/ego sio spirit
Kukubali kwangu sio tatizo .....
Tatizo ni kwamba nikubali kwasababu gani?
Au nikubali tu kwasababu wewe umesema?
Kwanza niseme tu kuwa chanzo cha uhai ni mungu mwenyewe, pili hakuna tofauti kati ya roho na uhai, kama sivyo je inawezekana mtu akawa hai bila roho au kuwa na roho lakini hana uhai?(Rejea ulichosema wakati wa ufafanuzi hapo juu).
Nini maana ya uhai na nini maana ya roho?
Na soul ni nini?