Je, wapinzani ni wakombozi?

Je, wapinzani ni wakombozi?

nadhani hawajui la kufanya au ni kutetea chochote kitu....wanaogopa wakileta za kuleta wanamwaga unga au wanakuwa wakolimba! Kwa hivyo hata wapinzani wakipewa nchi, mambo ya kulinda maslahi na kuogopa kushindwa yapabaki palepale. Kwa hiyo hakutakuwa na jipya sana. Cha muhimu ni kufight kubadilisha kwanza haya mambo, bila kuyabadilisha hawataweza kuchukua nchi. Kama wameweza kufichua ufisadi nadhani hata fight ya kubadili hizo institutions wanaiweza.

Mama:

Unachozungumza wewe ni EYES ON PRIZE. Lakini kuna upande mwingine hatujaungalia. Hivi wapinzani wakiweza kuwa na nusu ya viti vya bunge na kubaki kama wapinzani, ni vitu gani vitatendeka bungeni? Ninaamini check and balance itakuwepo.
 
Yes Ngabu,

this is what I am also talking about. Utasikia mtu akikubali kuwa ccm haifai kabisa kuongoza nchi na kisha baadaye tena anaishia kwenye kusema kuwa si vyema kuitoa ccm madarakani sasa hivi.

CCM has taken my patience for granted and now I'm through with them. They just need to go away. No discussion.
 
Mama,

wapinzani walishaanza kuchukua nchi hata vijijini - anzia Tarime - samahani watani zangu wakurya lakini huko kwenu bado ni kijijini.

Bila kuiondoa ccm kwenye uongozi wa nchi, hizo katiba wala roots zingine za vijijini nani atajenga kama ccm wanatumia whatever they can to stay in power?

Huku kwetu bado sana, na wananchi wanajua upinzani maana yake ni vita!

kumbuka hata majimbo yote ya tarime yakachukuliwa na upinzani, na yale ya kilimanjaro pia, na kigoma na wapi tena bado sio nguvu ya kutosha kuleta maendeleo. Lakini ndio itakuwa mwanzo mzuri wa kuleta challenge bungeni na sio kuchukua madaraka ya nchi nzima.
 
Huku kwetu bado sana, na wananchi wanajua upinzani maana yake ni vita!

kumbuka hata majimbo yote ya tarime yakachukuliwa na upinzani, na yale ya kilimanjaro pia, na kigoma na wapi tena bado sio nguvu ya kutosha kuleta maendeleo. Lakini sio itakuwa mwanzo mzuri wa kuleta challenge bungeni na sio kuchukua madaraka ya nchi nzima.

Mama ukisema kuwa wapinzani wasichukue madaraka nchi nzima unamaanisha kuwa ccm waendelee kuongoza si ndio?
 
Mama:

Unachozungumza wewe ni EYES ON PRIZE. Lakini kuna upande mwingine hatujaungalia. Hivi wapinzani wakiweza kuwa na nusu ya viti vya bunge na kubaki kama wapinzani, ni vitu gani vitatendeka bungeni? Ninaamini check and balance itakuwepo.

kama wataweza kuchukua nusu ya viti bungeni, kudos. Lakini wapinzani ,watawezaje kuchukua nusu ya viti bungeni?ukweli unabaki kuwa hawataweza kwa vile hawajajiandaa, leo hii ni May 2008! kuna mwaka tu kabla kampeni za uchaguzi hazijaanza.
 
Mama ukisema kuwa wapinzani wasichukue madaraka nchi nzima unamaanisha kuwa ccm waendelee kuongoza si ndio?

Kwa vile hamjajiandaa kuchukua kura yangu, sasa mie nifanye nini? hata kama wanaJF wote tukaamua kuwapa kura wapinzani its just a small fraction to win......5000 in ca 40m?
 
kama wataweza kuchukua nusu ya viti bunge, kudos. Lakini wapinzani ,watawezaje kuchukua nusu ya viti bungeni?ukweli unabaki kuwa hawataweza kwa vile hawajajiandaa, leo hii ni May 2008! kuna mwaka tu kabla kampeni za uchaguzi hazijaanza.

Muda mwingine huwa najiuliza kama hawa wapinzani ni kina nani. Hivi ni nani leo hii anajitolea kupoteza kila kitu kuwa mpinzani wa ccm Tanzania?

Taarifa zinaonyesha kuwa wale viongozi wa upinzani ni sehemu kidogo tu ya population ya Tanzania. Je waachiwe wao tu kuleta mabadiliko Tanzania.

Nani yuko responsible na kwenda kuhamasisha upinzani kiteto kama matokeo yatakuwa ni kukutana na full brass ya ccm kuanzia Msekwa hadi Komba hadi FFU na wengine ambao wana orders za kupiga yule anayeonekana kuhatarisha maslahi?

Kuna kazi hapa kama ccm ikiendelea kuachiwa dola hata hiyo ndoto ya wabunge 50 percent haitafikiwa.
 
Kwa vile hamjajiandaa kuchukua kura yangu, sasa mie nifanye nini? hata kama wanaJF wote tukaamua kuwapa kura wapinzani its just a small fraction to win......5000 in ca 40m?

Mama tatizo ni kuwa kinachofanyika sio kushinda tu, ni kubadili maisha ya watanzania. Nani anapenda kuwa mpinzani? Nani anataka maisha yake yote ayapoteze kwenye upinzani dhidi ya serikali za huko Afrika?

Mimi nakubali kuitwa mpinzani kwa vile napinga kila kinachofanywa na top brass ya ccm kwenye kuuza nchi na kuifilisi huku watoto na mama wajawazito wakifa kwa magonjwa yanayoweza kutibika kabisa kwa hivyo vijisenti vya wizi.
 
kama wataweza kuchukua nusu ya viti bungeni, kudos. Lakini wapinzani ,watawezaje kuchukua nusu ya viti bungeni?ukweli unabaki kuwa hawataweza kwa vile hawajajiandaa, leo hii ni May 2008! kuna mwaka tu kabla kampeni za uchaguzi hazijaanza.

Kwa matatizo yalivyopo Tanzania wapinzani wajiandae vipi?
 
Muda mwingine huwa najiuliza kama hawa wapinzani ni kina nani. Hivi ni nani leo hii anajitolea kupoteza kila kitu kuwa mpinzani wa ccm Tanzania?

Taarifa zinaonyesha kuwa wale viongozi wa upinzani ni sehemu kidogo tu ya population ya Tanzania. Je waachiwe wao tu kuleta mabadiliko Tanzania.

Nani yuko responsible na kwenda kuhamasisha upinzani kiteto kama matokeo yatakuwa ni kukutana na full brass ya ccm kuanzia Msekwa hadi Komba hadi FFU na wengine ambao wana orders za kupiga yule anayeonekana kuhatarisha maslahi?

Kuna kazi hapa kama ccm ikiendelea kuachiwa dola hata hiyo ndoto ya wabunge 50 percent haitafikiwa.

na CCM wanatumia uzoefu tu na mwisho wao upo kama hao wanaoitwa wapinzani watakuwa na upinzani wa kweli...wasisubiri wakati wa uchaguzi ndio tuwaone. Ubaya wa CCM ni kujikita katika ngazi zote za administration.

Kijijini hadi balozi wa nyumba 10 ni CCM na halipwi chochote.....lkn hayo mapenzi aliyonayo kwa CCM humwambii kitu. Miundombinu tangu inaribiwe na elnino ni miaka kumi sasa bado hakuna hata daraja moja lililojengwa lkn ukimchanja damu yake inatoka ni ya njano na kijani.

Mchawi wa maendeleo ni mwananchi, so ili Tanzania iendelee haihitaji chama chochote kuiendeleza bali ni moyo wa maendeleo wa kiongozi yeyote yule awaye....asiye na tamaa ya kujilimbikizia mali bali mwenye tamaa ya jina lake kukumbukwa na vizazi vyote pindi maisha yake yatakapofikia tamati kwa kuleta hayo maendeleo.
 
Mimi nadhani tusije kukosa kuelewana. Ngoja nisema msimamo wangu kwenye hili ili kusiwe na utata wowote ule.

a. CCM imeshindwa kuongoza nchi
b. CCM ndiyo chanzo cha matatizo yote ya kisiasa na kiuchumi.
c. CCM ndiyo mama ambaye amemzaa mtoto ufisadi.
d. CCM hawastahili hata dakika moja ya ziada ya kuendelea kutawala jinsi walivyo
e. CCM lazima iondolewe madarakani mapema iwezekanavyo.

That given:

a. Kwa wanaotaka kuiondoa CCM lazima wajue lengo lao la mwisho ni nini. Kuiondoa CCM siyo lengo la mwisho.

b. Lengo lao la mwisho lihalalishe nia yao ya kuiondoa CCM; hivyo kuiondoa CCM ni sehemu ya kufikia lengo hilo.

c. Lengo hilo lazima liwe wazi, linalowezekana, linalovutia na linaloweza kushawishi akili ya mtu yeyote yule. Kwa maneno mengine, lazima liwe lengo lenye kufanya watu waone matumaini, wajawe na shauku, na watambue sababu ya wao kulifikia lengo hilo.

d. Lengo hilo lazima lishawishi fikra za watu wengi zaidi na kati yao lazima wawepo wana CCM. Bila kushawishi idadi ya wana CCM (crossovers) kuiondoa CCM ni njozi isiyotimilika. Ndio maana wenzetu hapa hawategemei kura za watu wa chama chao tu bali wanategemea pia crossovers na independents. Ni lengo gani linaweza kuwashawishi wana CCM na watu wasio na vyama?

e. Wale wanaotaka kuiondoa CCM lazima waonekane kuwa ni bora kuliko siyo sawa au dhaifu kuliko. Hadi watu waone kuwa wale wanaotaka kuingia badala ya CCM ni BORA kwa kila hali hawataweza kuibadilisha CCM. Hivyo, haitoshi kuonesha ubovu wa CCM, bali pia UBORA wa wanaotaka kuingia madarakani.

f. Kwa upande wangu naamini njia ya msingi ya kuonesha ubora wa wanaotaka kuiondoa CCM ni kujenga fikra zenye mvuto na kushinda katika uwanja wa fikra unaothibitishwa na vitendo vya kuvutia.

g. CCM inaweza kuondolewa madarakani saa na siku yeyote pale tu lengo sahihi litakapowekwa wazi na litatimiza kifungu (c) na litakalohakikisha kuwa kifungu (e) nacho kinatimizwa. Nje ya hapo, CCM na ubovu wake itaendelea kuongoza.

h. Kila anayetaka kuona CCM inatoka madarakani lazima aanze kushiriki katika nafasi yake. Ndugu msomaji, wewe unashiriki vipi katika kuhakikisha CCM inaondoka madarakani mapema iwezekanavyo? Jibu la swali lako litakupa wazo ni mapema kiasi gani CCM itaondoka madarakani.

M. M.
 
Je thread hii imefikia conclusion? kama ndio bado hilo swali lako linahitaji thread mpya ili tusichanganye mambo!

Uliuliza swali kuwa upinzani haujajiandaa. Matatizo ya Tanzania ndio maandalizi ya mabadiliko ya serikali. Na kama mtu haoni matatizo ya kutaka mabadiliko then there are something wrong.

Wanasema: Mtu anakuita mpumbavu kwa ridhaa yako na watanzania ni ridhaa yetu kutawaliwa na vichwa maji.
 
Habari ndiyo hiyo. nasubiri maendeleo ya tanzania 2010 kutoka kwa serikali ya upinzani,
 
Uliuliza swali kuwa upinzani haujajiandaa. Matatizo ya Tanzania ndio maandalizi ya mabadiliko ya serikali. Na kama mtu haoni matatizo ya kutaka mabadiliko then there are something wrong.

Wanasema: Mtu anakuita mpumbavu kwa ridhaa yako na watanzania ni ridhaa yetu kutawaliwa na vichwa maji.

Sijauliza swali bali nilisema kwa maandishi kuwa wapinzani hawajajiandaa kuchukua madaraka ili kuleta hayo maendeleo.
 
Kwa vile hamjajiandaa kuchukua kura yangu, sasa mie nifanye nini? hata kama wanaJF wote tukaamua kuwapa kura wapinzani its just a small fraction to win......5000 in ca 40m?

Kwa hiyo ina maana CCM wamekushawishi uwape kura yako?
 
hawajanishawishi kama ambavyo wapinzani hawajanishawishi, lkn bibi yangu na babu na majirani zao kule kijijini wameniambia wanawapa kura zao sisiemu.
 
Mimi nadhani tusije kukosa kuelewana. Ngoja nisema msimamo wangu kwenye hili ili kusiwe na utata wowote ule.

a. CCM imeshindwa kuongoza nchi
b. CCM ndiyo chanzo cha matatizo yote ya kisiasa na kiuchumi.
c. CCM ndiyo mama ambaye amemzaa mtoto ufisadi.
d. CCM hawastahili hata dakika moja ya ziada ya kuendelea kutawala jinsi walivyo
e. CCM lazima iondolewe madarakani mapema iwezekanavyo.

That given:

a. Kwa wanaotaka kuiondoa CCM lazima wajue lengo lao la mwisho ni nini. Kuiondoa CCM siyo lengo la mwisho.

b. Lengo lao la mwisho lihalalishe nia yao ya kuiondoa CCM; hivyo kuiondoa CCM ni sehemu ya kufikia lengo hilo.

c. Lengo hilo lazima liwe wazi, linalowezekana, linalovutia na linaloweza kushawishi akili ya mtu yeyote yule. Kwa maneno mengine, lazima liwe lengo lenye kufanya watu waone matumaini, wajawe na shauku, na watambue sababu ya wao kulifikia lengo hilo.

d. Lengo hilo lazima lishawishi fikra za watu wengi zaidi na kati yao lazima wawepo wana CCM. Bila kushawishi idadi ya wana CCM (crossovers) kuiondoa CCM ni njozi isiyotimilika. Ndio maana wenzetu hapa hawategemei kura za watu wa chama chao tu bali wanategemea pia crossovers na independents. Ni lengo gani linaweza kuwashawishi wana CCM na watu wasio na vyama?

e. Wale wanaotaka kuiondoa CCM lazima waonekane kuwa ni bora kuliko siyo sawa au dhaifu kuliko. Hadi watu waone kuwa wale wanaotaka kuingia badala ya CCM ni BORA kwa kila hali hawataweza kuibadilisha CCM. Hivyo, haitoshi kuonesha ubovu wa CCM, bali pia UBORA wa wanaotaka kuingia madarakani.

f. Kwa upande wangu naamini njia ya msingi ya kuonesha ubora wa wanaotaka kuiondoa CCM ni kujenga fikra zenye mvuto na kushinda katika uwanja wa fikra unaothibitishwa na vitendo vya kuvutia.

g. CCM inaweza kuondolewa madarakani saa na siku yeyote pale tu lengo sahihi litakapowekwa wazi na litatimiza kifungu (c) na litakalohakikisha kuwa kifungu (e) nacho kinatimizwa. Nje ya hapo, CCM na ubovu wake itaendelea kuongoza.

h. Kila anayetaka kuona CCM inatoka madarakani lazima aanze kushiriki katika nafasi yake. Ndugu msomaji, wewe unashiriki vipi katika kuhakikisha CCM inaondoka madarakani mapema iwezekanavyo? Jibu la swali lako litakupa wazo ni mapema kiasi gani CCM itaondoka madarakani.

M. M.

Wewe ni mwanachama wa CCM? Jibu lako litatupa insights zaidi....
 
hawajanishawishi kama ambavyo wapinzani hawajanishawishi, lkn bibi yangu na babu na majirani zao kule kijijini wameniambia wanawapa kura zao sisiemu.

Kwa hiyo bibi yako na babu yako wameshawishika na hoja kabambe za CCM au wameuzika na pilau, soda, kanga, na kofia za bure?
 
Back
Top Bottom