Mimi nadhani tusije kukosa kuelewana. Ngoja nisema msimamo wangu kwenye hili ili kusiwe na utata wowote ule.
a. CCM imeshindwa kuongoza nchi
b. CCM ndiyo chanzo cha matatizo yote ya kisiasa na kiuchumi.
c. CCM ndiyo mama ambaye amemzaa mtoto ufisadi.
d. CCM hawastahili hata dakika moja ya ziada ya kuendelea kutawala jinsi walivyo
e. CCM lazima iondolewe madarakani mapema iwezekanavyo.
That given:
a. Kwa wanaotaka kuiondoa CCM lazima wajue lengo lao la mwisho ni nini. Kuiondoa CCM siyo lengo la mwisho.
b. Lengo lao la mwisho lihalalishe nia yao ya kuiondoa CCM; hivyo kuiondoa CCM ni sehemu ya kufikia lengo hilo.
c. Lengo hilo lazima liwe wazi, linalowezekana, linalovutia na linaloweza kushawishi akili ya mtu yeyote yule. Kwa maneno mengine, lazima liwe lengo lenye kufanya watu waone matumaini, wajawe na shauku, na watambue sababu ya wao kulifikia lengo hilo.
d. Lengo hilo lazima lishawishi fikra za watu wengi zaidi na kati yao lazima wawepo wana CCM. Bila kushawishi idadi ya wana CCM (crossovers) kuiondoa CCM ni njozi isiyotimilika. Ndio maana wenzetu hapa hawategemei kura za watu wa chama chao tu bali wanategemea pia crossovers na independents. Ni lengo gani linaweza kuwashawishi wana CCM na watu wasio na vyama?
e. Wale wanaotaka kuiondoa CCM lazima waonekane kuwa ni bora kuliko siyo sawa au dhaifu kuliko. Hadi watu waone kuwa wale wanaotaka kuingia badala ya CCM ni BORA kwa kila hali hawataweza kuibadilisha CCM. Hivyo, haitoshi kuonesha ubovu wa CCM, bali pia UBORA wa wanaotaka kuingia madarakani.
f. Kwa upande wangu naamini njia ya msingi ya kuonesha ubora wa wanaotaka kuiondoa CCM ni kujenga fikra zenye mvuto na kushinda katika uwanja wa fikra unaothibitishwa na vitendo vya kuvutia.
g. CCM inaweza kuondolewa madarakani saa na siku yeyote pale tu lengo sahihi litakapowekwa wazi na litatimiza kifungu (c) na litakalohakikisha kuwa kifungu (e) nacho kinatimizwa. Nje ya hapo, CCM na ubovu wake itaendelea kuongoza.
h. Kila anayetaka kuona CCM inatoka madarakani lazima aanze kushiriki katika nafasi yake. Ndugu msomaji, wewe unashiriki vipi katika kuhakikisha CCM inaondoka madarakani mapema iwezekanavyo? Jibu la swali lako litakupa wazo ni mapema kiasi gani CCM itaondoka madarakani.
M. M.