Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

Je, Watoto wanaolelewa bila vipigo hawana maadili?

Hili huwa mnalipimaje? Maadili yanaendana na ustaarabu , kitu ambacho waafrica ni 0.

Ukiwaondoa wahindi, wathailand, wamexico na wa brazili na mataifa machache. Most of watu weupe wana maadili . Anza na wajapani, wachina na wazungu wenyewe, hapo ondoa black americans maana nao ni kama sisi tu isipokuwa kuna mifumo fulani fulani inawabana inawataka kuact accordingly.
Africa tunaonekana hatuna maadili kwa sababu tumeiga maisha ya wenzetu na tamaduni zao , zile njia zetu za asili na za tangu kale zinamafunzo mazuri sana ya kimaadili ndio maana kulikua na jando na unyago.
 
Ninyi mliolelewa kwa vipigo mnajiona mna maadili? Mnataka kusemaje kizazi cha 80’ 90’ mliopigwa kama ngoma si ndio ninyi maadili yenu 0 wazee wa chini kwa chini?

Kinachomtofautisha mtoto aliyezoea kupigwa na yule ambaye hajapigwa ni confidence, Ukipigwa sana ile unayoiona wewe ni confidence si confidence bali ni arrogance, Ambae hajapigwa mara nyingi huwa na confidence iliyo balanced na anakuwa expressive (anaweza kujieleza) Mean while wa vipigo either akose confidence au awe arrogant.

Na most of psychopaths wamelelewa kwenye violence, think .
Maadili ya bongo ni kutokuwa shoga tu,
Wewe mradi sio shoga hata ukiwa teja, fisadi, jambazi, mkwepa kodi, malaya, mbamikiaji kesi, muongo n.k sio ishu sana.
 
Watoto wengi waliolelewa Kwa vipigo hawana maadili . wazazi wale wakali , wazee wakufoka foka wametoka 0-0 hawajafanikiwa kuandaa kizazi bora

Kuna njia za kulea mtoto ambazo zinaweza kumfanya akawa na Utii. Heshima na maadili mazuri.


Mtoto mfanye awe na usikivu mzuri na mpatie na EI
Mbinu moja wapo ni kiboko kama unabisha weka nyingine
 
Tunaishi kijamaa sana ni rahisi kuambukizana tabia tofauti na wenzetu.


Kuna siku niliokota simu katika kituo cha boda boda

Nikawauliza nani kadondosha simu hii wakamkosa

Nikawaambia hii simu isizimwe naiacha hapa mwenye simu akipiga mpokee then mwambieni aje achukue simu yake.


Baada ya muda waliniambia kuwa Leo jumapili hii ni riziki yetu tuuze hii simu tupate chochote kitu.

Nilichofanya niliwaambia fanyeni chochote Mimi sitohusika

So waliuza simu kama ya 300K Kwa 50 ili wapate elfu 10K awakuangalia kuwa aliyepoteza simu atapata hasara gani

Sisi bado Sana maadili
😁🤗🤔
 
Mnataka kuleta maisha ya kizungu mwishoni mitoto inakuwa ma bwabwa
Mtoto lazima umpitishe njia ngumu ngumu ila aje awe strong mbeleni ukimdekeza mwishowe ndio unakuta tatzo kidogo anaona bora ajiue
Hili suala la ushoga mmelishikia bango ilhali bongo ni kama halipo ila mnalitumia ili kujustfy ukatili dhidi ya watoto wenu
 
Ahsante Sana kwa mada yako. Ndiyo Iko x usiku kucha jana na inaendelea.

Naongezea; tuna wazee wengi hawatunzwi na watoto wao waliowachapq Sana kwa madai ya kuwatengeneza. Je hii siyo MOJAWAPO ya athari ya mpasuko wa mahusiano ya watoto na Wazee ? Kwamba nguvu kubwa ilitumika kuumiza mwili badala ya ku transform akili ya ndani ya mtoto? Sasa mtoto kawa mkubwa, Tabia zake zilizokandamizwa kwa hofu ya kipigo, sasa zinaanza kushamiri na kumea maana hakuna wa kumpiga tena?

Nini maoni yenu?
Napingana nawewe mh. Tofautisha uonevu kwa mtoto na adhabu kama amekosea!
sisi tumekua ukikosea wewe mwenyewe kabisa unajutia kuwa hapa nimekosea na unastahili adhabu!
hivyo mzazi anapokuja kutoa hiyo adhabu moja kwa moja unathibitisha kabisa kweli hili ni kosa na nilistahili
adhabu.

Point yako ya kusema wazazi wanatelekezwa kisa walitoa adhabu/kipigo kwa watoto wao haina mashiko.
Naweza kusema huo ni moyo wa mtu tu kwanza mtoto anatabia ya kusahau kama unatoa adhabu kwa haki
wapo wengi tu watoto wao walisomesha kwa shida wakiuza ardhi na mifugo nk ili mtoto asome matokeo yake
wazazi hao wametelekezwa na mtoto hana sababu yoyote ya maana.

Point yako yako ya pili mtoto akiwa mkubwa anafanya yale aliyokandamizwa asifanye kwa hofu ya kipigo na sasa anafanya. Hii nayo umeingia chaka vibaya mno.Hakika umelelewa vizuri huwezi kuja kukengeuka ukubwani
mtu anaye kuja kukengeuka ukubwani bado malezi yake yana uwalakini mkubwa kipindi cha makuzi yake.
{Mtoto umuleavyo ndivyo akuavyo}

Mimi nimeanza kutembea sehemu mbalimbali kusiko na ndg isipokuwa rafiki tu anakupa connection
lakini ukifika hiyo circle ina watu wenye tabia ovu kama kuvuta bangi na kutumia madawa ya kulevya.

lakini kwa sababu ya maonyo na vipigo kila tulipoonyesha viashiria vya kihuni mzee alitoa kipigo kitakatifu.
hadi leo hii mzee huwa namwambia bila kipigo nisingekuwa hapa nilipo.

Nina uhakika hata wewe madame umepokea mkong'oto wa kutosha kutoka kwa wazazi na waalimu wako ndio maana upo hapo.

kuzarau mapigo leo hii kutokuwa na shukrani hata kidogo kwa juhudi zilifanyika hadi ukafika hapa ulipo
Ulipaswa utuambia kuwa kwa hakika mapigo kiasi yana mchango kwenye maadili. Lakini leo hii ninyi
ambao wazazi wenu hawakuwa maprofesa waliwalea ninyi mmekuwa ma professor cha ajabu wewe professor katika uzao wako unaweza ukakoswa kabisa professor!

Ukiangalia kila kitu unacho elimu ya kutosha unayo maisha mazuri unayo
mtoto ada sio ya kuuliza bima ya afya mtoto anayo. cha ajabu anaweza kujitahidi sana na kufoji mno akapata
phd. Haya siyasemi kwa bahati mbaya kama wewe hufanyi wenzio wanafanya.

NI MAONI YANGU BINAFISI. ahsante.
 
Viboko muhimu ila visizidi kipimo. Si kila kosa mtoto apigwe anaelekezwa kwanza kama hasikii ndio viboko vitumike. Mimi binafsi viboko vimenisaidia sana vinginevyo hali ingekua mbaya sana.
 
Kupigwa tumepigwa sana tukiwa wadogo, hata kwa kosa dogo sana ambalo unaweza kulielewa unadundwa tu

Ni ujahilia na ujima tu kupiga eti mtoto ananyooka hapana
Tumeona vibaka wanapigwa kila leo na kesho anarudia kosa
Kuna watoto wana autistic ila hatuwatambui sisi ni kupiga tu na kusema litoto litundu hili, kumbe mtoto ni mtukutu kwa maradhi aliyonayo
Mimi nina watoto wengi ila sijarudia makosa ya kupiga kama unapiga nyoka bali nimekuwa na ukaribu sana na wanangu na wananipenda sana kwa kuwafundisha maadali mema
Unapokuwa na tabia ya kupiga kwa kila kosa unatengeneza uadui na chuki pia
Watoto wanakuwa wanakuogopa hata shule wakiwa wanaonewa na watoto wengine hawawezi kusema wakihofia utapiga tena na kusema lipumbavu ninapiga, wakati wewe ndio umetengeneza mtoto akuogope

Kulea sio kupiga ndio maana mpaka unaona mimba ndio unashtuka au kijana anakuja kukuuwa mwisho
 
Unaenda shule unaibiwa peni

Unaenda bweni unaibiwa kila kitu mpaka unanunuliwa sanduku la Chuma

Kiufupi maadili Africa bado tupo 0-0
Bado hujanijibu mkuu, hizo mbinu tofauti na mazingira ya kwetu ni zipi tofauti na kuadabishana kwa kiboko?
 
Kupigwa tumepigwa sana tukiwa wadogo, hata kwa kosa dogo sana ambalo unaweza kulielewa unadundwa tu

Ni ujahilia na ujima tu kupiga eti mtoto ananyooka hapana
Tumeona vibaka wanapigwa kila leo na kesho anarudia kosa
Kuna watoto wana autistic ila hatuwatambui sisi ni kupiga tu na kusema litoto litundu hili, kumbe mtoto ni mtukutu kwa maradhi aliyonayo
Mimi nina watoto wengi ila sijarudia makosa ya kupiga kama unapiga nyoka bali nimekuwa na ukaribu sana na wanangu na wananipenda sana kwa kuwafundisha maadali mema
Unapokuwa na tabia ya kupiga kwa kila kosa unatengeneza uadui na chuki pia
Watoto wanakuwa wanakuogopa hata shule wakiwa wanaonewa na watoto wengine hawawezi kusema wakihofia utapiga tena na kusema lipumbavu ninapiga, wakati wewe ndio umetengeneza mtoto akuogope

Kulea sio kupiga ndio maana mpaka unaona mimba ndio unashtuka au kijana anakuja kukuuwa mwisho
Sisapoti kupiga kila muda ila sio kuacha kabisa. Samaki mkunje angali mbichi.
 
Au unampiga Mtoto Kisa kapoteza au kuangusha Pesa uliyomtuma akanunue maandazi. Mtoto hajafanya makusudi.
Usipokuwa makini huyo mtoto hatokuwa makini kamwe. mtoto akipoteza muulize kwa upole ilikuwaje hadi akapoteza hiyo hela?
Mtoto anakwambia alipita kwa akina fln wakaanza kucheza njiani ndo ikapotea hapo siku ya kwanza umemwambia asirudie
ya pili umemugiza kwa mangi mwendo wa dk 3 anatumia dk20 halafu unaishia tu kusema usirudie sawa mwanangu?
Toa kipigo fimbo2 zinamtosha kabisa na mwambia ukitumwa kitu nunua rudi kwanza ndo aende akacheze.

Hayo malezi yenu haya ndo watoto wetu wanaenda kukutana na watoto wenu shuleni tuna haribikiwa wote
mtoto anaibwa kila kitu huko shule mwisho wa siku nayeye anaona kumbe kuibaina ndo formula ya huku
anaiba na kufukuzwa.
 
Back
Top Bottom