Je, wezi wa Wizara ya fedha wameshafahamu aina ya Rais tuliyenaye?

Tatizo lako unazomea wanaojadili badala ya kujadili na kujiuliza kwa nini watu hawa hawakuogopa rais mpya. Uonavyo ulichoandika kinakupa nafuu yoyote?
 
Kumbuka tumesha kubaliana tuachie pesa ije mtaani,saa hizi kuna wengine wamepata bahati huko mtaani Mzigo wa Wizara ya fedha nao umewafikia! Kama kuna mafundi Ujenzi au mafundi Magari saa hizi nao wanawapiga pesa Watumishi wezi wa fedha za Umma!!
sasa pesa haichiwi hivyo mkuu, huo ni uchumi wawapi umesoma mkuu.
 

Mkuu bora umesema ukweli, hapa ukisikia hizi propaganda mfu unaweza kuamini kipindi cha Magufuli hakukuwa na wizi, kumbe ulikuwepo ila vyombo vya habari viliwekwa kapuni.
 
Hao waache na sarakasi zao. Hainisaidii maana hata ruzuku za vyama sihitaji kujua matumizi yao. Ni bure tu!

Mkuu mbona hujahoji ile ripoti ya BoT ya januari to March ambayo mama aliunda tume? Ifahamike wakati huo Magufuli bado alikuwa hai.
 
Kama waziri anasema wameanza tarehe 30 march basi wamekua rais tuliyenae ni DHAIFU
Huyo waziri Mkuu anadhani sisi ni wajinga, ripoti ya BoT ya januari to March mbona mama haiweki hadharani, tujue uadilifu wa hapo kabla? Maana ile 1.5t tulipigwa hivi hivi.
 
Majaliwa au hussein mwinyi, huyu mama anatupotez
Kweli kabisa magufuli aliingia mkenge kumpa huyu mama umakamo wa rais, nadhani ni kutaka kufurahisha watu kwa kigezo eti usawa wa kijinsia lakini ukweli ni kwamba huyu mama hakufaa, haendani kabisa na Ile kasi tuliyokua tumeizoea ya magufuli ..
 
Tusipoamka usingizini mapema, Nchi inaweza kuangukia mikononi mwa Fisi zaidi ya hata ilivyokuwa wakati wa Awamu ya Nne.
TUTAMKUMBUKA.
 
Tatizo lako unazomea wanaojadili badala ya kujadili na kujiuliza kwa nini watu hawa hawakuogopa rais mpya. Uonavyo ulichoandika kinakupa nafuu yoyote?
Kama akili yako ni finyu sina msaada, hicho nacho ni kilema. Nimeandika kitu kiko wazi wala siyo tafsida
 
Wanasiasa wana tabia moja kuu, nayo ni kwamba, mwizi, mla rushwa, fisadi ni yule wa kundi la mlengo au chama tofauti.
 
Mimi kwenye wizi wa fedha za serikali na mali ya umma sitakuwa mpole(sauti ya aliyekuwa mwenye wizara..)
 
Maza apige 15 hata kama tutaibiwa lakini tuna amani hakuna mauji wala kesi za uhujumu uchumi za kipumbavu, kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
wezi utawajua tu.wale kwa urefu wa kamba zao hao wahuni wanatakiwa kurudisha fedha hizo mara moja hawa wahuni wanaoshabikia kitendo hiki nao waache mara moja.
 
Maza apige 15 hata kama tutaibiwa lakini tuna amani hakuna mauji wala kesi za uhujumu uchumi za kipumbavu, kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Umesema kweli kabisa, kwanza kufanya uchaguzi tunaongeza gharama tuu.

SSH OYEEEEEE Mambo yaendelee tupumzike
 
Hoja za kipuuzi kabisa, endeleeni kucheka na kima. Safari hii majizi ndio yatashamiri kila kona.
 
Ndio kusema PM anaongea na suspect...
Nakumbuka kwenye ishu kama hio, huo sio uongeaji wake kabisaaa.

Binadamu version Tanzania hawana umbile maalumu kama virusi nadhani, ku-switch ni dk sifuri nukta kadhaa.
 
Katibu mkuu wa wizara anatakiwa kupanda kwa succession planning kama ilivyokuwa kwa Dr Gwajima (yeye alitakiwa kuwa katibu mkuu au waziri) huo ndio utaratibu duniani.

Serikali ina mfumo mzuri Dr Gwajima (as a case study for succession planning), sasa sijui huwa wanaboronga wapi? Mamlaka ya raisi kuteua inaboronga utaratibu wao wa kutengeneza vipanga kuwa makatibu wakuu au tatizo ni nini hasa.

Ni aibu kama nchi hatuna watu dizaini ya Dr Gwajima kwenye kila wizara and spares ambao uwezi kuwaongopea wanafahamu taratibu zote juu mpaka chini kwenye wizara husika.

Unapomtoa kipanga kutoka kwenye work floor na kumpandisha vyeo taratibu kila hatua unampa training ya kupata skills sahihi za nafasi yake. Na kwenda juu kila unapofikiria kusogeza watu unafikiria na uwezo wao ikibidi tafuta na manuscripts za matokeo yao tangia primary skills.

Ndio maana mtu kama Dr Gwajima anaijuwa wizara ya afya kinaga ubaga, kwanza ni daktari, pili ame practice kwenye work floor, tatu amekuwa trained on management at hospital level, amekuwa DMO anajua kusimamia policy, akapelekwa wizarani kashika nafasi kadhaa za policy advisor na kupanda hadi kuwa mkurugenzi wa tiba i.e chief policy advisor.

Ukishatengenezwa kwa mtindo huo na performance appraisal yako inaridhisha nchi za wenzetu ndio unafikiriwa kuwa katibu mkuu wa wizara au hata katibu mkuu kiongozi (those are transferable skills), na hawa ndio watu wanaoongoza nchi za wenzetu technically.

Ndio maana Dr Gwajima uwezi kumuongopea wizara ya afya yaani yule ananyuti tu kwa sababu hampo tayari kwa mabadiliko, hila ni mtaalamu wa hali ya juu.

Katibu mkuu wizara ya fedha hana ufahamu wa kusimamia ile wizara atachezewa tu, kigezo sio kuwa economist tu; experience ya kufanya kazi serikalini na wizarani also matters a lot.

Mama Samia amuangalie katibu mkuu kiongozi wake ni bomu, hana uwezo katika nafasi ya kumshauri.
 
Hoja za kipuuzi kabisa, endeleeni kucheka na kima. Safari hii majizi ndio yatashamiri kila kona.
Kinachofurahisha zaidi, ni wale wenye smart phone na pesa ya bando tu ndo wanamsifia mama ukiacha wanasiasa version TZ.

Kimtaa mtaa, hakuna anayefuatilia tena nini kinaendelea serikalini, kama ikulu imerudi kuwa lango la walanguzi au kuwa takatifu, hakuna anayejali, pengine walimvia mama kwenye hotuba mbili muhimu, wakahitimisha.

Pengine wanahisi tumeingia kwenye AUTO PILOT mode.
 
Katibu ni nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…