Je, wezi wa Wizara ya fedha wameshafahamu aina ya Rais tuliyenaye?

Je, wezi wa Wizara ya fedha wameshafahamu aina ya Rais tuliyenaye?

Hoja za kipuuzi kabisa, endeleeni kucheka na kima. Safari hii majizi ndio yatashamiri kila kona.
Kwani safari iliyopita ya Mwendazake hakukuwa na majizi? Tena majizi yenyewe yalikuwa yanaanza na yeye mwenyewe. Au umesahau hoja ya ukaguzi ya Tsh 2.4 Trilion
 
Wee Kama sio mjinga si ukamuulize aliyeiunda , majaaliwa ndo ameiiunda yeye anafanya yaliyondani yake

Huko serikalini, hakuna collective responsibility? Ama kila mmoja anakuja na lake?
 
Mama akitaka legacy nzuri aende na katiba mpya
Baaasss
 
Mbowe na Lisu meno yote nje kwa furaha
20210529_084552.jpg
 
Kwa wakulima wa mahindi na mpunga, tunaelewa uharibifu wa nyani na tumbili na ndege. Huwa tunaanza kuweka matambala na kichwa cha bandia ili wanyama hawa waamini huyo ni mlinzi.

Wanyama polepole huanza kuzoea na kugundua kwamba hayo ni matambala na hakuna kichwa, ni chungu cheusi. Hapo sasa mazao huanza kuliwa.

Tumeanza kuona wizi na ulaji wa hovyo. Tena ndani ya wizara mama yenye kushikilia hazina ya taifa na nchi. Wizara ya Fedha wanaanza kuiokomba nchi kweupeee! Hisia yangu hawa ni nyani waliogundua kwamba hatuna tena mlinzi wa fedha ya umma. Rais wetu utajua mwenyewe! Kama nawe una maneno yale ya kusema nchi hii utaiacha kama alivyoiacha Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Magufuli. Aliyesema simtaji.

Yeye mwenyewe kasafiri kwenda USA kupasua tezi dume imagine matibabu ambayo angepata Nairobi kama aliona shida kuoneka nyumbani kwake
Shamba la bibi
 
Haya madudu ndiyo yanayowafanya waandike kwamba sasa hivi wana furaha zamani hawakuwa na furaha.

Lakini sauti ya Majaliwa ina mamlaka ndani yake ndiyo maana wako bize kumfundisha rais Samia kuwa amtoe kwenye uwaziri mkuu kwa sababu eti ni masalia ya JPM!

Kwani SAMIA ni masalia ya nani?
 
Kwa wakulima wa mahindi na mpunga, tunaelewa uharibifu wa nyani na tumbili na ndege. Huwa tunaanza kuweka matambala na kichwa cha bandia ili wanyama hawa waamini huyo ni mlinzi.

Wanyama polepole huanza kuzoea na kugundua kwamba hayo ni matambala na hakuna kichwa, ni chungu cheusi. Hapo sasa mazao huanza kuliwa.

Tumeanza kuona wizi na ulaji wa hovyo. Tena ndani ya wizara mama yenye kushikilia hazina ya taifa na nchi. Wizara ya Fedha wanaanza kuiokomba nchi kweupeee! Hisia yangu hawa ni nyani waliogundua kwamba hatuna tena mlinzi wa fedha ya umma. Rais wetu utajua mwenyewe! Kama nawe una maneno yale ya kusema nchi hii utaiacha kama alivyoiacha Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Magufuli. Aliyesema simtaji.

Wakati wa Magufuli wezi walikuwa wanalindwa na kulelewa, sasa hivi wanachukuliwa hatua

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Kinachofurahisha zaidi, ni wale wenye smart phone na pesa ya bando tu ndo wanamsifia mama ukiacha wanasiasa version TZ.

Kimtaa mtaa, hakuna anayefuatilia tena nini kinaendelea serikalini, kama ikulu imerudi kuwa lango la walanguzi au kuwa takatifu, hakuna anayejali, pengine walimvia mama kwenye hotuba mbili muhimu, wakahitimisha.

Pengine wanahisi tumeingia kwenye AUTO PILOT mode.
"Auto pilot mode " nimekuelewa Sana mkuu
 
Rais SSH yuko vizuri. Yeye kaibiwa na kagundua kabla hata ya CAG kukagua mahesabu. Kuibiwa huwezi kuzuia bali kutambua wizi ndiyo akili

Lakini huyo Mwendazake wenu alikuwa anaiba yeye na genge lake halafu CAG akihoji anamfukuza kazi.

Sukuma Gang, mtahangaika sana kutafuta kasoro
Hoja dhaifu Sana hii.Ngoja nikuambie kipindi Cha Mwendazake pesa ya serikali ililiwa kwenye miradi hata ripoti ya CAG imekuja kutuambia hasara hasara hasara .means Kuna biashara serikali imefanya ,uwekezaji ikatokea hasara tofauti na upigaji huu wa kiboya Sana eti watu wanalipana posho ndani ya miezi 2 tu milioni 500 hii ni disrespect .
 
Kwani mkuu lini wizi uliisha?kama ungekuwa umekwisha ripoti ya CAG, isingekuwa vile ilivyo kwa 2019/2020!sema tu ilikuwa ni marufuku kuu ripoti, kwa kumuogopa jiwe, hivyo watu wakaaminishwa kuwa hakukuwa na pesa ya serikali iliyoibiwa!!sasa awamu ya sita inaamini ktk uwazi ndio maana mtaanza kusema hivyo kuwa hawamuogopi kumbe ni uwazi ambao jiwe hakuupenda!!kinachotakiwa hao wabadhirifu ikibainika kweli wamekula pesa ni adhabu kali sana wapewe.Tena hakuna kipindi ambacho pesa imeliwa kama cha awamu ya tano kwa taarifa yako.yaani ingetokea ikafanyika special audit ya miaka 5, iliyopita watu watazimia kwa kutoamini ubadhirifu mkubwa wa pesa.
Naona hapa umeleta ushabiki na uzandiki
 
Serikalini vitengo vingi watu wanapiga mpunga, Sio TRA, BOT, wizara ya fedha, hazina nk
 
Hii sijui ni Kweli
WIZARA YA FEDHA POSHO ZAO TOKA MWEZI WA TATU TU 1: 251,000,000/= (31/03/2021)kazi maalum
2:198,000,000/=(31/03/2021)
3:44,500,000/=(08/04/2021)
4:155,295,000/=(13/04/2021)
5:43,900,000/=kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira (30/04/2021)
6:14,400,000/=siku ya wanawake(30/04/2021)
7: 43,000,000/=(30/04/2021)
8:184,100,000/=(meimosi asubuhi 01/05/2021)
9:264,000,000/=(meimosi mchana 01/05/2021)
10:146,500,000/=( Kuandika mpango Kazi wa manunuzi watu 125 03/05/2021)
11:171,200,000/=(kuandaa nyaraka za bunge)
 
Unafikiri mkwere kile kijiji alichojenga kwao Msoga kilitokana na mshahara wake? Hiyo VOTE ya ikulu Ndio kichaka chenyewe na Ndio maana MNIKULU mara zote anakuwa mtu wa karibu sana/ ndugu wa Rais!!! Mkwere alikuwa na binamu yake!!!!
Jina lake nadhani ni Maneno.
 
Hii sijui ni Kweli
WIZARA YA FEDHA POSHO ZAO TOKA MWEZI WA TATU TU 1: 251,000,000/= (31/03/2021)kazi maalum
2:198,000,000/=(31/03/2021)
3:44,500,000/=(08/04/2021)
4:155,295,000/=(13/04/2021)
5:43,900,000/=kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira (30/04/2021)
6:14,400,000/=siku ya wanawake(30/04/2021)
7: 43,000,000/=(30/04/2021)
8:184,100,000/=(meimosi asubuhi 01/05/2021)
9:264,000,000/=(meimosi mchana 01/05/2021)
10:146,500,000/=( Kuandika mpango Kazi wa manunuzi watu 125 03/05/2021)
11:171,200,000/=(kuandaa nyaraka za bunge)
Siku zote sababu za matumizi ya pesa huwa hazikosekani.

Wamesomea uhasibu miaka na miaka hawawezi kukosa sababu ya kuvuta mpunga.
 
Kwa wakulima wa mahindi na mpunga, tunaelewa uharibifu wa nyani na tumbili na ndege. Huwa tunaanza kuweka matambala na kichwa cha bandia ili wanyama hawa waamini huyo ni mlinzi.

Wanyama polepole huanza kuzoea na kugundua kwamba hayo ni matambala na hakuna kichwa, ni chungu cheusi. Hapo sasa mazao huanza kuliwa.

Tumeanza kuona wizi na ulaji wa hovyo. Tena ndani ya wizara mama yenye kushikilia hazina ya taifa na nchi. Wizara ya Fedha wanaanza kuiokomba nchi kweupeee! Hisia yangu hawa ni nyani waliogundua kwamba hatuna tena mlinzi wa fedha ya umma. Rais wetu utajua mwenyewe! Kama nawe una maneno yale ya kusema nchi hii utaiacha kama alivyoiacha Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Magufuli. Aliyesema simtaji.

Wewe uwe Rais anayokuja. Utawanyoosha kweli kweli. Mama Samia delegate most everything to Majaliwa.
 
Back
Top Bottom