Je, wezi wa Wizara ya fedha wameshafahamu aina ya Rais tuliyenaye?

Je, wezi wa Wizara ya fedha wameshafahamu aina ya Rais tuliyenaye?

Mama hawezi.

Sio kuyamudu haya pekee, lakini sioni atakavyoweza kuondoa uozi mwingi sehemu mbalimbali serikalini na kwenye mashirika yake.

Mama hana uthubutu na sina uhakika kama anajua ni kipi akifanye kuyaondoa haya na hayo mengi yaliyozagaa kila upande serikalini na kwenye mashirika.

Siyo ajabu, yeye mwenyewe ndiye atakaye yachochea yaongezeke zaidi na zaidi.
Mama aliaminiwa na Hayati aliyeweza na alikuwa sehemu ya mema na mabaya ya Awamu iliyopita.

Aina ya utendaji ni tofauti na kipindi hiki hiyo inayoitwa mifumo ndio ipo kazini.
 
Naona hapa umeleta ushabiki na uzandiki
Ushabiki upi sasa?hata kipindi cha jiwe pesa inakuwa ikiliwa tu, lakini nani alikuwa na uwezo wa kusema?kwani sasa ukiibuka upigaji utasikia "wapigaji wameanza"!!! Kwani waliisha lini?wapigaji wapo tu na wataendelea kupiga kutokana na mfumo wa kulindana uliopo ndani ya ccm.
 
Wewe uwe Rais anayokuja. Utawanyoosha kweli kweli. Mama Samia delegate most everything to Majaliwa.
Ukimsikiliza Majaliwa, anazungumza kwa mipaka. Hasemi lolote juu ya Katibu mkuu, hasemi juu ya Waziri, why? Ndo PM tuliyenaye. Enzi ya Sokoine angelala nao mbele.

Huenda pia PM anaelewa katibu mkuu na Waziri wana nafasi ipi kwenye furaha ya rais. Tuko kwa Viongozi wanaodeka kwa urafiki binafsi.
 
Kwa wakulima wa mahindi na mpunga, tunaelewa uharibifu wa nyani na tumbili na ndege. Huwa tunaanza kuweka matambala na kichwa cha bandia ili wanyama hawa waamini huyo ni mlinzi.

Wanyama polepole huanza kuzoea na kugundua kwamba hayo ni matambala na hakuna kichwa, ni chungu cheusi. Hapo sasa mazao huanza kuliwa.

Tumeanza kuona wizi na ulaji wa hovyo. Tena ndani ya wizara mama yenye kushikilia hazina ya taifa na nchi. Wizara ya Fedha wanaanza kuiokomba nchi kweupeee! Hisia yangu hawa ni nyani waliogundua kwamba hatuna tena mlinzi wa fedha ya umma. Rais wetu utajua mwenyewe! Kama nawe una maneno yale ya kusema nchi hii utaiacha kama alivyoiacha Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Magufuli. Aliyesema simtaji.

Ingekuwa ni huko China wote wangepigwa risasi, na wengine wengijiua wenyewe kuliko 'aibu' ya kuuawa na serikali...
 
Ushabiki upi sasa?hata kipindi cha jiwe pesa inakuwa ikiliwa tu, lakini nani alikuwa na uwezo wa kusema?kwani sasa ukiibuka upigaji utasikia "wapigaji wameanza"!!! Kwani waliisha lini?wapigaji wapo tu na wataendelea kupiga kutokana na mfumo wa kulindana uliopo ndani ya ccm.
Unaandika kama mtu asiyejua sababu ya JPM kuchukiwa na waajiliwa wa serikali. Tangu siku yake ya kwanza JPM aliwafinya Wizara ya fedha na BOT. Bandarini na makontena, TRA, nk. Sasa kama upigaji ulikuwepo ni sawa, kwamba haukuonekana, lakini hadithi za kuzuiwa kuusema ni hisua zako binafsi bila ushahidi.

Watu walifukuzwa hadi majukwaani. Wengine wakalalama eti wezi wafukuzwe kwa staha! Ikaitwa ni uonevu. Nadhani umeshindwa kukumbuka yaliyofanyika, ukatunga yasiyokuwepo
 
Mama aliaminiwa na Hayati aliyeweza na alikuwa sehemu ya mema na mabaya ya Awamu iliyopita.

Aina ya utendaji ni tofauti na kipindi hiki hiyo inayoitwa mifumo ndio ipo kazini.
Sasa hivi "MIFUMO" inafanya kazi; eti Eeeh Bhwanah!

Mama alikuwa ni msindikizaji tu wakati wa hayati, kama anavyoonekana kuwa msindikizaji tu wakati huu hiyo "MIFUMO" unayoongelea ikimwendesha.
 
Sasa hivi "MIFUMO" inafanya kazi; eti Eeeh Bhwanah!

Mama alikuwa ni msindikizaji tu wakati wa hayati, kama anavyoonekana kuwa msindikizaji tu wakati huu hiyo "MIFUMO" unayoongelea ikimwendesha.
Hayati aliufahamu vyema usindikizaji wake kuanzia 2015. Dharau zetu kwa jinsia ya like haziwezi kutufikisha popote.
 
Ukimsikiliza Majaliwa, anazungumza kwa mipaka. Hasemi lolote juu ya Katibu mkuu, hasemi juu ya Waziri, why? Ndo PM tuliyenaye. Enzi ya Sokoine angelala nao.

Huenda pia PM anaelewa katibu mkuu na Waziri wana nafasi ipi kwenye furaha ya rais. Tuko kwa Viongozi wanaodeka kwa urafiki binafsi.
Tukuweke wewe Uwe Rais, tupe mikakati yako.
 
Hayati aliufahamu vyema usindikizaji wake kuanzia 2015. Dharau zetu kwa jinsia ya like haziwezi kutufikisha popote.
Sasa hapa nashindwa kukuelewa.

"Dharau zetu kwa jinsia ya kike"?

Nani amedharau, hayati? Kwa nini iwe "zetu". Unanihusisha nami pia kwenye hiyo 'zetu'?
 
Mi nimekaa hapa pembeni nasubiri hatma ya hao ngedere waharibifu wa shamba letu,je wataachwa waendelee Kula au watafukuziwa mbali na ikibidi kuwanyang'anya mahindi walioficha?
 
Sasa hapa nashindwa kukuelewa.

"Dharau zetu kwa jinsia ya kike"?

Nani amedharau, hayati? Kwa nini iwe "zetu". Unanihusisha nami pia kwenye hiyo 'zetu'?
Tumpe muda Mama afanye kazi, kuliko kumjazia negativity zetu za kila siku.
 
Tumpe muda Mama afanye kazi, kuliko kumjazia negativity zetu za kila siku.
Kwa hiyo tunyamaze ndipo kazi itafanyika..., tukimjazia 'negativity' hatafanya kazi?

Watu hawawezi kuacha kutoa mawazo yao kwa sabau za aina hiyo. Uliona wapi hilo likitokea?

Watu wata'assess' kazi anazofanya kwa mwndelezo sio kwa kusubiri muda maalum.

Mwelekeo hadi sasa ni kwamba anayo matumaini kidogo sana ya kuwa atakuwa kiongozi wa kukumbukwa kwa kazi zake.
 
Back
Top Bottom