Je, yaliyotokea kwenye familia ya Mengi kujirudia kwa Mrema?

Je, yaliyotokea kwenye familia ya Mengi kujirudia kwa Mrema?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Augustino Mrema amefariki Dunia, Agosti 21, 2022, hili halina ubishi na sisi kama wanadamu tuliosalia hapa Duniani, hatuna budi kumuombea kwa Mungu nafuu ya adhabu ya kaburi na nafuu siku ya khiyama.

Bali tunatafakari jambo moja tu linalohusu mirathi, Lyatonga Mrema "bila kushawishiwa na mtu "aliutangazia ulimwengu kwamba ANAOA MWANAMKE MPYA MZURI MWEUPE MDOGODOGO, na baada ya siku chache ndoa ikafungwa, bado hatukuelewa sababu hasa ya Mzee Mrema kunyakua ngoma mbichi katika uzee wake ule na afya aliyokuwa nayo, ilimchukua Mrema muda mwingi kusimama kanisani ili kula kiapo cha ndoa, hii ni kutokana na mgogoro wa Afya yake au uzee.

Sasa hoja yetu ni hii hapa, huyu aliyeolewa ni mke halali kwa mujibu wa sheria za Tanzania japo aliolewa miezi michache iliyopita, vipi kuhusu mgawanyo wa mali za Mrema (kama anazo), Je, ya Reginald Mengi na K-Lyn hayatajirudia?
 
Mke kaoewa na CCM, mahari kalipiwa na CCM watajijua,ila wazee wakichaga acheni ulimbukeni wa vibinti uzeeni mtakufa midomo wazi siku si zenu

Angetafuta nesi mstaafu akawa anamlipa kumuhudumia, miaka 77 huwezi kupeleka moto kwa binti bila mkongo au viagra, Viagra mixer kisukari changanya na presha lazima ukate moto
 
Ukiwa na watoto wakubwa na bahati mbaya mke kawahi tangulia kuepuka migogoro ya mirathi achana na mambo ya kuoa ni kuwaletea shida watoto.

We kamata sepa na sio kuweka mizizi, mabinti wanafata urithi.
 
Watoto wa Mrema sio mafala. Hakuna chochote alichochuma na Mrema. Ataondoka na nguo zake tu.
Mirathi is not about ulichochuma na marehemu, bali uhusiano wako na marehemu. If all conditions remains constant. Warithi wa asili wa Mzee Mrema kwa mjibu wa Sheria kama wapo hai ni;
1.Mke wake halali kwa mjibu wa Sheria.
2.Watoto wake
3. Mama yake mzazi
4.Baba yake mzazi.
 
Back
Top Bottom