Augustino Mrema amefariki dunia , hili halina ubishi na sisi kama wanadamu tuliosalia hapa duniani , hatuna budi kumuombea kwa Mungu nafuu ya adhabu ya kaburi na nafuu siku ya khiyama .
Bali tunatafakari jambo moja tu linalohusu mirathi , Lyatonga Mrema "bila kushawishiwa na mtu " aliutangazia ulimwengu kwamba ANAOA MWANAMKE MPYA MZURI MWEUPE MDOGODOGO , na baada ya siku chache ndoa ikafungwa , bado hatukuelewa sababu hasa ya Mzee Mrema kunyakua ngoma mbichi katika uzee wake ule na afya aliyokuwa nayo , ilimchukua Mrema muda mwingi kusimama kanisani ili kula kiapo cha ndoa , hii ni kutokana na mgogoro wa Afya yake au Uzee .
Sasa hoja yetu ni hii hapa , huyu aliyeolewa ni mke halali kwa mujibu wa sheria za Tanzania , japo aliolewa miezi michache iliyopita , Vipi kuhusu mgawanyo wa mali za Mrema ( kama anazo ) , Je ya Reginald Mengi na K-Lyn hayatajirudia ?